Salamu wakuu!
Naomba mchango wenu kimawazo maana nina muwekezaji anatafuta shamba kubwa maeneo ya Morogoro. Angependa sehemu inayostawisha machungwa, malimao, machenza (Citrus) na mananasi. Pia Iringa kwa ajili ya ngano, matunda na mboga.
Wataalamu, wenye uzoefu na wenye contact naomba ushauri wenu. Tunahitaji kujua shamba liko eneo gani, ukubwa, bei, jinsi panavyoingilika, ukaribu wa maji, upatikanaji wa mvua na masharti ya uuzaji. Lengo ni kuwekeza kwenye kilimo kwa muda mrefu na hata mikataba itajali maslahi ya majirani na wanavijiji.
Shukurani.
Salamu wakuu!
Naomba mchango wenu kimawazo maana nina muwekezaji anatafuta shamba kubwa maeneo ya Morogoro. Angependa sehemu inayostawisha machungwa, malimao, machenza (Citrus) na mananasi. Pia Iringa kwa ajili ya ngano, matunda na mboga.
Wataalamu, wenye uzoefu na wenye contact naomba ushauri wenu. Tunahitaji kujua shamba liko eneo gani, ukubwa, bei, jinsi panavyoingilika, ukaribu wa maji, upatikanaji wa mvua na masharti ya uuzaji. Lengo ni kuwekeza kwenye kilimo kwa muda mrefu na hata mikataba itajali maslahi ya majirani na wanavijiji.
Shukurani.
<br />Mkuu nashukuru kwa mwongozo! Maswali zaidi: <ol class="decimal"><li>Naweza kupata namba ya Mahenge? Hayo mashamba anauza au kukodisha? Tatizo siwezi kwenda Iringa kumtafuta ila ningempata kwa simu tungeanza mazungumzo ndio tupange kukutana.</li><li>Isele na Ng'ang'ange ni Iringa pia?</li></ol>Asante!
vipi maeneo ya Dar es Salaam?
Kuna shamba lipo maeneo ya kibwegere, kama kilomita 11 toka barabara kuu ya dar - moro. ukubwa wa zaidi ya ekari 10, lipo karibu na mto mpiji.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba hii 0718 096981.
Mama EE wewe upo wapi sasa ? Nauliza kwa sababu maybe I can help...
Kuna kijiji ktk jimbo la Ismani kinaitwa isele, kipo tarafa ya pawaga sasa sijui mjumbe hapo juu anamaanisha kijiji hicho au la.
Mkuu nashukuru kwa mwongozo! Maswali zaidi:Asante!
- Naweza kupata namba ya Mahenge? Hayo mashamba anauza au kukodisha? Tatizo siwezi kwenda Iringa kumtafuta ila ningempata kwa simu tungeanza mazungumzo ndio tupange kukutana.
- Isele na Ng'ang'ange ni Iringa pia?
Wakuu mbarikiwe! Hapa napata mwongozo muruwa. Kwa mwenye contact naomba anipatie hapa au kwa pm.
Kuhusu ukubwa wa shamba, tunaangalia ya eka 200+ kwa sasa. Nahitaji pia mwongozo wa bei.. najua huwa ni makubaliano hasa ukizingatia masharti nk... lakini naomba kama kuna mwenye uzoefu wa mauzo ya siku za karibuni anijulishe hayo mashamba yanakwenda kwa bei zipi.
Kwa sasa niko nje ya nchi.
Haya mashamba ya huyu mzee ni makubwa kwa maana ya ukubwa na yana t.deed,hata mwalimu aliwahi kufika kuyashangaa, sasa si rahisi kuyauza kienyeji, hapa ni kufika Iringa na kuonana naye uso kwa macho,ili kama unaweza kukodi au akauza mmoja ya milima, mi sijui. Kuna mtu mmoja yupo Dar,aliyeniunganishia mimi huko, naamini anaweza kujua kinachoendelea pale. Si vizuri kutaja jina lake hapa, nikirudi Dar naweza kumtafuta ili nikusaidie. Haya ni mashamba ambayo inabidi uwe na trecta za maana, yapo tambalale safi.
Bei za mashamba mengine zinatofautiana toka location moja hadi nyingine. Bei ya juu kabisa ambayo mimi nilichomoa kule Kimara Iringa ni laki moja na ishirini kwa eka na ya chini ni 40 elfu kwa eka. Maeneo mengine unashuka mpaka 30 elfu kwa eka. Maeneo yasiyo na barabara mpaka 20 elfu kwa eka unapata. Haya ni maeneo yenye mvua za kutosha, manpower ya kuaminika.
Kazi ni kwako !!!!!!
Ni kweli, sio yote yanafaa kuwa hadharani. Pia bei za kukodisha zinaendaje na ni kwa muda gani?
Nitashukuru sana kwa msaada mkuu... hapa tu umeshanifumbua macho. Ngoja tuangalie akiona inalipa tunaweza ku-formalize hizi consultation. Unlifikiriaje hilo?
Ndio kuna mzee mmoja huko TZ, ana hektra nyingi kule morogoro nadhani maeneo ya matombo if not mistaken, .. labda ni inbox nikupe contact zake..