Naombeni ajira, kibarua au fursa

The Salt

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
390
1,024
Mara ya mwisho nilipata Mtu humu akaniamini akanishika mkono na kunipeleka Porini/Hifadhini kwenye shughuli zinazohusiana na Utalii, nilijitahidi kufanya kwa uaminifu na kupata Exposure na Experience ya vitu tofauti tofauti hadi janga la COVID-19 lilipopelekea kila kitu kusimama huko Mbugani kwa kiasi kikubwa,nikiwa na maana kwamba toka mwaka 2020 sijawahi kuingiza chochote kama Ujira ikabidi nirudi Nyumbani kwanza kuona nazikabili vipi changamoto za kujikimu kimaisha.

Hadi sasa nabangaiza ili familia yangu ipate chochote,na sioni dalili tena ya kurudi porini labda itokee nipate mwekezaji mpya. Kwa wenye familia wanaelewa ugumu uliopo kuhakikisha basic needs zinapatikana wakati huna kazi maalumu,ndo nachopitia and as a man,hii hali inani break into pieces wakubwa! Usipokaa vizuri mentally ni SONONA kabisa.

To mention a few;
1.Nimewahi kufanya kazi kama Bar Manager
- Hii kazi niliifanya kwa muda takribani miaka mitatu na nusu,hadi pale nilipokuja kupata changamoto mpya ya kazi.
~ Eneo la kazi lilikuwa ni Dar Es Salaam
~ Bar ilihusisha pia Ukumbi wa kufanyia shughuli mbalimbali za burudani,Guest House, na Kulaza magari (Car Parking).

2. Niliwahi kuwa Msimamizi wa Biashara ya Mtu binafsi ya Bajaj (TVS KING)
~ Hizi Bajaj zilikuwa nyingi akiwa anawapa vijana waendeshe na kuleta hesabu hivyo akahitaji mtu ambaye atafutalia kwa ukaribu ili mambo yakae sawa,nikawa nipo pale huku pia na mimi nikajifunza kuendesha hizo Bajaj na Gari (Hivyo ni dereva pia in advance).
~ Eneo la Kazi lilikuwa Kibaha Pwani.

3. Curio Shops Supervisor &Airstrip Attendant
~ Hizi ni biashara ambazo huusisha uuzaji wa vitu vya asili kwa Wageni/Watalii.
~ Airstrip Attendant (Hii ilikuwa ndege zinaposhuka basi unaandika zimeshuka na wageni wangapi,zikitoka hapa zinaenda kutua wapi na zitaondoka na wangapi. Hizo taarifa unazijaza kwenye kitabu maalumu halafu baadae ndo hizo taarifa zinapelekwa kwa wahusika).
~ Eneo la Kazi lilikuwa ni Serengeti Hifadhini.

4. Niliwahi kusimamia Mradi wa Muhongo huko RUFIJI-Bungu
~ Ule mradi ulihusisha ulimaji wa Muhogo ekari nyingi sana,baada ya mavuno muhogo unapelekwa kiwandani (Mwekezaji alikuwa nacho huko huko)kwa ajili ya kuchakata na kupata bidhaa tayari kwa matumizi.

~ Changamoto kubwa ilikuwa ni usalama,maana mwekezaji alikuwa ameingia mkataba na wanakijiji kuwajengea barabara na kuwaletea huduma za jamii akapewa hekari za kutosha,ila wakati naanza kazi nilikuta kuna vuguvugu kubwa. Wafanyakazi wakawa wanaogopa kuuwawa wakaanza kuondoka mmoja mmoja,hadi mradi ukafungwa kwa muda nami nikarudi kwenye shughuli nyingine.

5. Embroidering (Kudarizi kwa kutumia mfumo wa kisasa)
~ Hii kazi nimekuja kujifunza katika harakati hizi hizi unaomba kazi hata kama huijui unaomba muda kidogo uone kama utai Master, nilikutana na mtu mwaka jana mwishoni akasema anafungua biashara ya Embroidery. Kupiga logo za aina zote kwa mfumo wa nyuzi au kufuma ila kwa kutumia mtambo wa kisasa,nadhani humu mnaijua hii.

Nikasafiri hadi mkoani ulipo uwekezaji. Nimejifunza hiyo kazi nikaijua vizuri na nikaifanya. Changamoto zikaja kati ya mwekezaji na mambo ya kifamilia (sasa hayo ni mambo ya siri maana anaweza kuwa yupo humu pia) biashara ilianza vizuri sana,unaandika majina kwenye sare za polisi,magereza,watu binafsi,logo za baa,makampuni nk.

~ Kingine biashara ilikuwa penzoni sana mwa Nchi kiasi kwamba ilihitaji nguvu kubwa kuifanyia promotion. Ila pia ni biashara ambayo kwa mtu serious na ana mikakati haswa inalipa,sema ndo hivyo tena hapa naomba nishauri kidogo; Kama wewe sio jamii ya Ki Asia, acha kuleta undugu kwenye Biashara unless otherwise kama miradi yako inahusisha ndugu, mashemeji, basi uweke bayana kuwa hapa ni kazi tu! Tena kwa herufi kubwa. Hii kitu imesababisha uwekezaji huu 'ufe' kwa nilivyoona mimi.
Hivyo ndugu zangu hii kazi ikipata mwekezaji serious inalipa.

Kwa hiyo naweza kusema nafanya kazi yoyote bila kubagua, mradi iwe halali na angalau inaweza kumfanya mtu alishe familia yake.

-Kwa wale wafugaji na wakulima wenye mashamba huko Mikoani,naweza kuwa msimamizi mzuri tu nikiwa eneo la mradi.

- Kuna Wale huwa wana miradi yao ila wanakosa uangalizi wa moja kwa moja kutokana na kutingwa na shughuli nyingine,napenda nikuhakikishie kuwa mimi ni mtu sahihi kwa hayo yote, kikubwa ni UAMINIFU na MAKUBALIANO kati ya Mwajiri na Mwajiliwa.

KUHUSU MIMI
Mimi ni kijana jinsia Mwanamme, naelekea miaka 33 na naweza kusema ni Mature enough, both mentally and physically. Sina Elimu ya Juu bali nina elimu ya kawaida ya Sekondari lakini nina uelewa wa vitu kadha wa kadha ambavyo vinahitaji zaidi kutumia exposure,akili ama nguvu kuliko vyeti.

Nipo Tayari kufanya kazi sehemu yoyote Nchi hii. Na nipo tayari kuonana na Mwajiri apajue ninapoishi na aijue familia yangu endapo itabidi kufanya hivyo. Nina uhitaji wa Kazi kwa hali na Mali.
Mengineyo:
  • Naweza kutumia Computer
  • Uwezo wa kuendana na Mazingira and loyal to hospitality issues.
  • Dereva, both Manual and Automatic Transmission.
UKIGUSWA KAMA MWAJIRI AU MWENYE KUNIKUTANISHA NA MWENYE AJIRA, NAOMBA TUWASILIANE PM ILI TUPEANE DETAILS ZAIDI.

Samahani kwa 'Gazeti'
Nitashukuru sana kwa yeyote atakayefanikisha Ombi langu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom