Mwekezaji anatafuta shamba

MamaEE

Member
Jun 2, 2011
99
57
Salamu wakuu!

Naomba mchango wenu kimawazo maana nina muwekezaji anatafuta shamba kubwa maeneo ya Morogoro. Angependa sehemu inayostawisha machungwa, malimao, machenza (Citrus) na mananasi. Pia Iringa kwa ajili ya ngano, matunda na mboga.

Wataalamu, wenye uzoefu na wenye contact naomba ushauri wenu. Tunahitaji kujua shamba liko eneo gani, ukubwa, bei, jinsi panavyoingilika, ukaribu wa maji, upatikanaji wa mvua na masharti ya uuzaji. Lengo ni kuwekeza kwenye kilimo kwa muda mrefu na hata mikataba itajali maslahi ya majirani na wanavijiji.

Shukurani.
 
Anahitaji shamba lenye ukubwa kiasi gani?
 
Kubwa... hana limit ya ukubwa hasa kama ni mahala penye rotuba na kustawisha zao zaidi ya moja kati ya hayo hapo juu. Pia nitamuuliza na kurudisha jibu ASAP.
 
Salamu wakuu!

Naomba mchango wenu kimawazo maana nina muwekezaji anatafuta shamba kubwa maeneo ya Morogoro. Angependa sehemu inayostawisha machungwa, malimao, machenza (Citrus) na mananasi. Pia Iringa kwa ajili ya ngano, matunda na mboga.

Wataalamu, wenye uzoefu na wenye contact naomba ushauri wenu. Tunahitaji kujua shamba liko eneo gani, ukubwa, bei, jinsi panavyoingilika, ukaribu wa maji, upatikanaji wa mvua na masharti ya uuzaji. Lengo ni kuwekeza kwenye kilimo kwa muda mrefu na hata mikataba itajali maslahi ya majirani na wanavijiji.

Shukurani.

Kama ni mwekezaji anayemaanisha, aende Iringa kwa Rodrick Mahenge, huyu mzee ana mashamba makubwa sana ambayo hayatumiki kwa sasa, haya mashamba yana barabara zinazopitika mwaka mzima, barabara hizi zina usafiri wa basi kila siku, manpower ipo, mvua za kutosha, vijito kadhaa ndani ya mashamba hayo. Haya mashamba yanafaa kwa kilimo cha ngano na hata yy kuna wakati alikuwa analima ngano na mahindi. Anaishi Iringa mjini, kwa sasa halimi.

Kwa ajili ya Matunda nenda kijiji cha Isele, huko Matunda ndio kwake, huko ardhi ipo kubwa. Ng`ang`ange kuna ardhi inafaa kwa matunda na chai.
 
Mkuu nashukuru kwa mwongozo! Maswali zaidi:
  1. Naweza kupata namba ya Mahenge? Hayo mashamba anauza au kukodisha? Tatizo siwezi kwenda Iringa kumtafuta ila ningempata kwa simu tungeanza mazungumzo ndio tupange kukutana.
  2. Isele na Ng'ang'ange ni Iringa pia?
Asante!
 
Wazo zuri
Mkuu nashukuru kwa mwongozo! Maswali zaidi: <ol class="decimal"><li>Naweza kupata namba ya Mahenge? Hayo mashamba anauza au kukodisha? Tatizo siwezi kwenda Iringa kumtafuta ila ningempata kwa simu tungeanza mazungumzo ndio tupange kukutana.</li><li>Isele na Ng'ang'ange ni Iringa pia?</li></ol>Asante!
<br />
<br />
 
Mama EE wewe upo wapi sasa ? Nauliza kwa sababu maybe I can help...

Kuna kijiji ktk jimbo la Ismani kinaitwa isele, kipo tarafa ya pawaga sasa sijui mjumbe hapo juu anamaanisha kijiji hicho au la.
 
vipi maeneo ya Dar es Salaam?
Kuna shamba lipo maeneo ya kibwegere, kama kilomita 11 toka barabara kuu ya dar - moro. ukubwa wa zaidi ya ekari 10, lipo karibu na mto mpiji.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba hii 0718 096981.
 
Nadhani huyu anatafuta shamba kuanzia eka 300 kwenda mbele.
 
Mama EE wewe upo wapi sasa ? Nauliza kwa sababu maybe I can help...

Kuna kijiji ktk jimbo la Ismani kinaitwa isele, kipo tarafa ya pawaga sasa sijui mjumbe hapo juu anamaanisha kijiji hicho au la.

Kama Isele ya Pawaga kuna maeneo yenye sifa anazotaka mjumbe ni vizuri ukimsaidia, lakini Isele ninayosema mimi ni ya Kilolo karibu na kijiji cha Lulanzi, ni majina tu, kama ilivyo Itimbo ya Kilolo na Itimbo ya Mfindi.
 
Mkuu nashukuru kwa mwongozo! Maswali zaidi:
  1. Naweza kupata namba ya Mahenge? Hayo mashamba anauza au kukodisha? Tatizo siwezi kwenda Iringa kumtafuta ila ningempata kwa simu tungeanza mazungumzo ndio tupange kukutana.
  2. Isele na Ng'ang'ange ni Iringa pia?
Asante!

Nafahamu yupo Iringa mjini, simu yake sina, kutafuta inawezekana, ni mtu maarufu. Ndio vijiji hivyo vyote viko wilaya ya Kilolo Iringa na viko karibu karibu. Kama ni mahindi ningemwelekeza Mawambala kwa Wadosi wenzake, pale Mawambala mahindi na ngano vinakubali.
 
Wakuu mbarikiwe! Hapa napata mwongozo muruwa. Kwa mwenye contact naomba anipatie hapa au kwa pm.

Kuhusu ukubwa wa shamba, tunaangalia ya eka 200+ kwa sasa. Nahitaji pia mwongozo wa bei.. najua huwa ni makubaliano hasa ukizingatia masharti nk... lakini naomba kama kuna mwenye uzoefu wa mauzo ya siku za karibuni anijulishe hayo mashamba yanakwenda kwa bei zipi.

Kwa sasa niko nje ya nchi.
 
Mkuu - ntashukuru sana. Niko nje ya nchi kwa sasa lakini nisingependa nisubiri hadi niwe nchini. Kama haina usumbufu kwako, tafadhali niunganishe na huyo Mzee.
 
Wakuu mbarikiwe! Hapa napata mwongozo muruwa. Kwa mwenye contact naomba anipatie hapa au kwa pm.

Kuhusu ukubwa wa shamba, tunaangalia ya eka 200+ kwa sasa. Nahitaji pia mwongozo wa bei.. najua huwa ni makubaliano hasa ukizingatia masharti nk... lakini naomba kama kuna mwenye uzoefu wa mauzo ya siku za karibuni anijulishe hayo mashamba yanakwenda kwa bei zipi.

Kwa sasa niko nje ya nchi.

Haya mashamba ya huyu mzee ni makubwa kwa maana ya ukubwa na yana t.deed,hata mwalimu aliwahi kufika kuyashangaa, sasa si rahisi kuyauza kienyeji, hapa ni kufika Iringa na kuonana naye uso kwa macho,ili kama unaweza kukodi au akauza mmoja ya milima, mi sijui. Kuna mtu mmoja yupo Dar,aliyeniunganishia mimi huko, naamini anaweza kujua kinachoendelea pale. Si vizuri kutaja jina lake hapa, nikirudi Dar naweza kumtafuta ili nikusaidie. Haya ni mashamba ambayo inabidi uwe na trecta za maana, yapo tambalale safi.

Bei za mashamba mengine zinatofautiana toka location moja hadi nyingine. Bei ya juu kabisa ambayo mimi nilichomoa kule Kimara Iringa ni laki moja na ishirini kwa eka na ya chini ni 40 elfu kwa eka. Maeneo mengine unashuka mpaka 30 elfu kwa eka. Maeneo yasiyo na barabara mpaka 20 elfu kwa eka unapata. Haya ni maeneo yenye mvua za kutosha, manpower ya kuaminika.

Kazi ni kwako !!!!!!
 
Ni kweli, sio yote yanafaa kuwa hadharani. Pia bei za kukodisha zinaendaje na ni kwa muda gani?

Nitashukuru sana kwa msaada mkuu... hapa tu umeshanifumbua macho. Ngoja tuangalie akiona inalipa tunaweza ku-formalize hizi consultation. Unlifikiriaje hilo?
 
Hapa tumejadiliana kwa ujumla, nakushauri tutenganishe, kama ni shamba la matunda bora ununue lako, kwa sababu unaweza kukuta gharama za kukodi ni sawa na kununua. Kama uko na simu hapo mtwangie mtu huyu 0768941703 anaweza kukwambia mashamba hayo kama hayajauzwa. Ni diwani wa eneo hilo. Akikuuliza sema malila kanielekeza.
 
Ndio kuna mzee mmoja huko TZ, ana hektra nyingi kule morogoro nadhani maeneo ya matombo if not mistaken, .. labda ni inbox nikupe contact zake..

Morogoro pako vizuri,
Nilifika Mabana Mvomero, kuna ardhi ya kutosha na nzuri, maji yapo ya kutosha kabisa. Tatizo wakati wa masika,gari halipiti, mpaka uwe na trecta. Nimechemsha kwa sababu hela zangu ni za mawazo, nafaka,matunda na mifugo vyote vinakubali, bei ziko vizuri sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom