Hauwezi kununua bandari, tutakuwa wajinga kukataa uwekezaji huu

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
MWEKEZAJI: HAUWEZI KUNUNUA BANDARI, TUTAKUWA WAJINGA KUKATAA UWEKEZAJI HUU

Nazir Karamagi, mmoja wa watu ambaye ametajwa muda mrefu kuwa mmiliki wa Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Bandarini (TICTS), iliyokuwa ikifanya kazi ya kupakia na kupakua makontena ya mizigo katika Bandari ya Dar Es Salaam, amekiri kuwa uwezo wa TICTS kuhudumia bandari hiyo hauwezi kumudu mahitaji ya sasa, huku akionesha umuhimu wa Tanzania kuchangamkia fursa ya mwekezaji mwingine, atayakeboresha utendaji kazi na ufanisi wa bandari hiyo na kuitumia kimkakati kuongeza mapato ya nchi.

Akizungumzia kwa mlengo wa falsafa ya biashara na uwekezaji wenye manufaa, ambao utasaidia nchi kuitumia bandari kimkakati kuwa mojawapo ya vyanzo vitakavyoongeza mapato, ambayo hatimae yatasaidia Serikali kuacha kutoza kodi nyingi wananchi wake, Mzee Karamagi amesisitiza kuwa uwekezaji wa bandari ni tofauti na maeneo mengine, ambapo bandarini kinachowekezwa ni uendeshaji, huku miundombinu ikiendelea kubakia mikononi mwa Serikali.

“Sisi tulikaa pale (Bandari ya Dar Es Salaam) kwa miaka 22, tulinunua bandari? Si mkataba umekwisha, tunamwachia mwenye bandari, anatafuta wengine. Tulipokuwa pale tunaweza kusema bandari ni ya kwetu? Miundombinu ya bandari inabaki mikononi mwa Serikali. Kwa hiyo, hilo mtu asipolijua atachanganya uwekezaji, auchanganye na ununuaji kama ilivyokuwa katika mashirika mengine.

"Mimi ni Karamagi ambaye ni mwasisi wa Kampuni ya TICTS. Wameizungumzia saaana. Ukiangalia, inaonesha kwamba Serikali zetu zote hazijafanya makosa katika uwekezaji ili taifa letu linufaike. TICTS imefanya kazi vizuri, ingawa kwa sasa tulipofikia Serikali imesema basi hebu tujaribu na wengine, ambalo si baya. TICTS wakati inaingia, bandari yetu ilikuwa makontena elfu sabini (70,000) kwa mwaka. Sasa hivi ni laki saba (700,000) kwa mwaka. Lakini tulipofika, mkataba wetu ukafika pale mwisho. Sisi hatuna matatizo na hilo, nchi kwanza. Kwa sbaabu kuna mkakati mkubwa, ambao ni uchumi,” amesema Karamagi na kuongeza;

"Kabla sijakupa maiki (Mhe. Katibu Mkuu Chongolo) naomba nikwambie kwanini mimi naunga mkono DP World, mimi sio mwanasheria, sitazungumzia vifungu vya sheria, nitazungumzia falsafa ya biashara. Naungana kwa hilo na Profesa Kitila. Serikali imewekeza zaidi ya trilion 1 kwenye uboreshaji wa bandari gati 0 mpaka namba 7. Mpaka leo hii eneo hili linachangia kwa makontena asilimia 15% tu ya makontena yote yanayotoka Bandari ya Dar es Salaam.”

Kampuni hiyo ya TICTS imekuwa ikifanya kazi ya kupakia na kupakua makotena katika Bandari ya Dar Es Salaam, kwenye magati ya makontena, tangu mwaka 2000, kwa mkataba uliodumu kwa miaka 22, hadi ulipofikia tamati mwishoni mwa mwaka jana na Serikali, kupitia Bodi ya Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), kufikia uamuzi wa kutoiongezea muda mwingine na kuamua kutafuta wawekezaji wengine watakaoboresha utendaji kazi na ufanisi wa Bandari ya Dar Es Salaam.

Kwa mujibu wa Makubaliano ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai yanayoweka msingi wa kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uboreshaji wa uendeshaji wa Bandari ya Dar Es Salaam, mwekezaji atawekeza katika magati namba 0 hadi 7, pekee katika bandari hiyo, tofauti na upotoshaji ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanaopinga uwekezaji huo, wakipotosha kuwa atapewa maeneo yote ya bandari.
 
Attachments

  • VID-20230804-WA0195(1).mp4
    38.6 MB
Siku hizi nikiona hizi mada za kuunga mkono huu mkataba mbovu wa DP World huwa naangalia kwanza mwanzishaji wa thread ni nani. Basi kama siyo Faiza, Ze Loss, Mvunja Barafu au Ze Big Shooo basi lazima jina litakuwa lina asili ya huko huko DP World....

Tuseme mara ngapi kwamba hakuna anayepinga uwekezaji? Kinachopingwa na kupigiwa makelele ni huu mkataba mbovu na wa kinyonyaji unaochukua bandari zote za bara kwa muda usiojulikana bila faida zetu kuwekwa wazi. Kipi kigumu hapo kuelewa?

Rekebisheni vipengele vinavyopigiwa makelele na mwekezaji aanze kazi mara moja. Na mkumbuke kwamba hili siyo suala la kidini....😬😬😬
 
MWEKEZAJI: HAUWEZI KUNUNUA BANDARI, TUTAKUWA WAJINGA KUKATAA UWEKEZAJI HUU

Nazir Karamagi, mmoja wa watu ambaye ametajwa muda mrefu kuwa mmiliki wa Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Bandarini (TICTS), iliyokuwa ikifanya kazi ya kupakia na kupakua makontena ya mizigo katika Bandari ya Dar Es aadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanaopinga uwekezaji huo, wakipotosha kuwa atapewa maeneo yote ya bandari.
Mpuuzi sana mhaya mwenzangu huyu. Yeye anasema amekaa pale miaka 22 mkataba ukaisha akaondoka. Sasa DP world mkataba wao ni wa miaka mingapi? Utaisha lini??
 
Mimi nataka mtu wa kujibu hoja moja baada ya nyingine. Huyo atakuwa ni kidume. Ila Hizi lugha za kwamba msikatae sijui DP wapo hadi marekani hamna kitu. Pia kwa nini tushindwe kuendesha bandari? Kwamba hatuna mitaji, hatuna wataalamu au shida nini.
 
Siku hizi nikiona hizi mada za kuunga mkono huu mkataba mbovu wa DP World huwa naangalia kwanza mwanzishaji wa thread ni nani. Basi kama siyo Faiza, Ze Loss, Mvunja Barafu au Ze Big Shooo basi lazima jina litakuwa lina asili ya huko huko DP World....

Tuseme mara ngapi kwamba hakuna anayepinga uwekezaji? Kinachopingwa na kupigiwa makelele ni huu mkataba mbovu na wa kinyonyaji unaochukua bandari zote za bara kwa muda usiojulikana bila faida zetu kuwekwa wazi. Kipi kigumu hapo kuelewa?

Rekebisheni vipengele vinavyopigiwa makelele na mwekezaji aanze kazi mara moja. Na mkumbuke kwamba hili siyo suala la kidini....😬😬😬
Faizafoxy kapigwa chini bado The Boss
 
Filosofia ya Biashara maifut.....mfyuuuuuuu​

Watanzania hawajaridhika na uwekezaji wa bandari, serikali isione aibu kuachana na Waarabu.​

saba nane
 
Siku hizi nikiona hizi mada za kuunga mkono huu mkataba mbovu wa DP World huwa naangalia kwanza mwanzishaji wa thread ni nani. Basi kama siyo Faiza, Ze Loss, Mvunja Barafu au Ze Big Shooo basi lazima jina litakuwa lina asili ya huko huko DP World....

Tuseme mara ngapi kwamba hakuna anayepinga uwekezaji? Kinachopingwa na kupigiwa makelele ni huu mkataba mbovu na wa kinyonyaji unaochukua bandari zote za bara kwa muda usiojulikana bila faida zetu kuwekwa wazi. Kipi kigumu hapo kuelewa?

Rekebisheni vipengele vinavyopigiwa makelele na mwekezaji aanze kazi mara moja. Na mkumbuke kwamba hili siyo suala la kidini....
Hata mimi namshangaa Karamagi. Kasema wao walikodishwa kwa miaka 22. Je, DP World wanakodishwa kwa miaka mingapi?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
MWEKEZAJI: HAUWEZI KUNUNUA BANDARI, TUTAKUWA WAJINGA KUKATAA UWEKEZAJI HUU

Nazir Karamagi, mmoja wa watu ambaye ametajwa muda mrefu kuwa mmiliki wa Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Bandarini (TICTS), iliyokuwa ikifanya kazi ya kupakia na kupakua makontena ya mizigo katika Bandari ya Dar Es ezaji huo, wakipotosha kuwa atapewa maeneo yote ya bandari.
Mfanya biashara gani anakubali kumsifia mfanya biashara mwenzake (mshindani) anayekuja kuwachukua wateja wake??

Ni series ya kutengeneza tu Kama series za kikorea
 
Nisamehe, nilipoona tu jina Juma Juma a.k.a Shehe Ubwabwa nikahamia mada zingine.

Sijui ni kwanini lakini nisamehe sana
 
Mpuuzi sana mhaya mwenzangu huyu. Yeye anasema amekaa pale miaka 22 mkataba ukaisha akaondoka. Sasa DP world mkataba wao ni wa miaka mingapi? Utaisha lini??

..Karamagi anatukosea kufananisha Ticts na mkataba wake na Dp World.

..na ukimsoma vizuri, anazungumza kwa kujihami, kwa kusema yeye sio mwanasheria.

..mtu akitetea jambo fulani huku akiweka tahadhari kwamba yeye sio mwanasheria, mwanasiasa, au kitu kingine, jua mtetezi huyo hana imani 100% na anachokitetea, au hasemi ukweli.

..kauli za Mzee Karamagi zinamsuta kwamba hana uhakika na anachokitetea, au haamini anachokitetea.
 
MWEKEZAJI: HAUWEZI KUNUNUA BANDARI, TUTAKUWA WAJINGA KUKATAA UWEKEZAJI HUU

Nazir Karamagi, mmoja wa watu ambaye ametajwa muda mrefu kuwa mmiliki wa Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Bandarini (TICTS), iliyokuwa ikifanya kazi ya kupakia na kupakua makontena ya mizigo katika Bandari ya Dar Es Salaam, amekiri kuwa uwezo wa TICTS kuhudumia bandari hiyo hauwezi kumudu mahitaji ya sasa, huku akionesha umuhimu wa Tanzania kuchangamkia fursa ya mwekezaji mwingine, atayakeboresha utendaji kazi na ufanisi wa bandari hiyo na kuitumia kimkakati kuongeza mapato ya nchi.

Akizungumzia kwa mlengo wa falsafa ya biashara na uwekezaji wenye manufaa, ambao utasaidia nchi kuitumia bandari kimkakati kuwa mojawapo ya vyanzo vitakavyoongeza mapato, ambayo hatimae yatasaidia Serikali kuacha kutoza kodi nyingi wananchi wake, Mzee Karamagi amesisitiza kuwa uwekezaji wa bandari ni tofauti na maeneo mengine, ambapo bandarini kinachowekezwa ni uendeshaji, huku miundombinu ikiendelea kubakia mikononi mwa Serikali.

“Sisi tulikaa pale (Bandari ya Dar Es Salaam) kwa miaka 22, tulinunua bandari? Si mkataba umekwisha, tunamwachia mwenye bandari, anatafuta wengine. Tulipokuwa pale tunaweza kusema bandari ni ya kwetu? Miundombinu ya bandari inabaki mikononi mwa Serikali. Kwa hiyo, hilo mtu asipolijua atachanganya uwekezaji, auchanganye na ununuaji kama ilivyokuwa katika mashirika mengine.

"Mimi ni Karamagi ambaye ni mwasisi wa Kampuni ya TICTS. Wameizungumzia saaana. Ukiangalia, inaonesha kwamba Serikali zetu zote hazijafanya makosa katika uwekezaji ili taifa letu linufaike. TICTS imefanya kazi vizuri, ingawa kwa sasa tulipofikia Serikali imesema basi hebu tujaribu na wengine, ambalo si baya. TICTS wakati inaingia, bandari yetu ilikuwa makontena elfu sabini (70,000) kwa mwaka. Sasa hivi ni laki saba (700,000) kwa mwaka. Lakini tulipofika, mkataba wetu ukafika pale mwisho. Sisi hatuna matatizo na hilo, nchi kwanza. Kwa sbaabu kuna mkakati mkubwa, ambao ni uchumi,” amesema Karamagi na kuongeza;

"Kabla sijakupa maiki (Mhe. Katibu Mkuu Chongolo) naomba nikwambie kwanini mimi naunga mkono DP World, mimi sio mwanasheria, sitazungumzia vifungu vya sheria, nitazungumzia falsafa ya biashara. Naungana kwa hilo na Profesa Kitila. Serikali imewekeza zaidi ya trilion 1 kwenye uboreshaji wa bandari gati 0 mpaka namba 7. Mpaka leo hii eneo hili linachangia kwa makontena asilimia 15% tu ya makontena yote yanayotoka Bandari ya Dar es Salaam.”

Kampuni hiyo ya TICTS imekuwa ikifanya kazi ya kupakia na kupakua makotena katika Bandari ya Dar Es Salaam, kwenye magati ya makontena, tangu mwaka 2000, kwa mkataba uliodumu kwa miaka 22, hadi ulipofikia tamati mwishoni mwa mwaka jana na Serikali, kupitia Bodi ya Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), kufikia uamuzi wa kutoiongezea muda mwingine na kuamua kutafuta wawekezaji wengine watakaoboresha utendaji kazi na ufanisi wa Bandari ya Dar Es Salaam.

Kwa mujibu wa Makubaliano ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai yanayoweka msingi wa kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uboreshaji wa uendeshaji wa Bandari ya Dar Es Salaam, mwekezaji atawekeza katika magati namba 0 hadi 7, pekee katika bandari hiyo, tofauti na upotoshaji ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanaopinga uwekezaji huo, wakipotosha kuwa atapewa maeneo yote ya bandari.
Huyu mlisema kawahonga CHADEMA na kina Tibaijuka, imekuwaje tena mnamwamini Hadi kumualika kwenye mikutano yenu?
 
Kwahio mtu akitaja kupata ufahamu / ushauri au mustakabari wa Bandari; anasema ngoja nikamuulize Karamagi ?

Nadhani kutokana na upuuzi aliofanya akiwa pale itakuwa sawa kufanya opposite ya kila anachosema huyu hakufaa kukaa pale wiki moja let alone muda wote aliokaa pale (na kukaa kwake kulikuwa kwa kucheza faulo)
 
Kwahio mtu akitaja kupata ufahamu / ushauri au mustakabari wa Bandari; anasema ngoja nikamuulize Karamagi ?

Nadhani kutokana na upuuzi aliofanya akiwa pale itakuwa sawa kufanya opposite ya kila anachosema huyu akufaa kukaa pale wiki moja let alone muda wote aliokaa pale (na kukaa kwake kulikuwa kwa kucheza faulo)
 
Back
Top Bottom