TANZIA Mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo afariki dunia

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,958
3,885
Mwanasiasa mkongwe na mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar, Hassan Nassor Moyo amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mkoani Tanga

Mzee Moyo ambaye pia ni Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar

Inna lillah wainna ilayhi rajiuna.


moyo.jpg


moyo.jpg

Hassan Moyo enzi za uhai wake akiwa na Hayati Nyerere na Karume

======

Mzee Moyo alikuwa mwanachama wa Chama cha Afro Shirazi (ASP) tangu kilipoanzishwa Februari 5, 1957 baadaye Februari 5, 1977 akajiunga na chama cha Mapinduzi akiwa na kadi namba 7.

Mzee Moyo ndiye alikuwa Mratibu Mkuu wa Maridhiano ya Zanzibar ya Novemba 5, 2009 yaliyowakutanisha Rais Mstaafu wa Zanzibar (awamu ya sita), Dk Aman Abeid Karume na Maaalim Seif Sharif Hamad katika kutafuta mbinu ya kuondoa tofauti iliyokuwepo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.

Mwaka 2015 Mzee Hassan Nassor Moyo alivuliwa uanachama wa chama cha mapinduzi CCM, hatua iliyofikiwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Magharibi, Unguja viswani Zanzibar kwa madai ya kukisaliti chama hicho kwa kukiuka maadili na kutoa matamshi yasiyokubaliana na sera za chama chao.

Mzee Moyo alidaiwa kutumia majukwaa ya siasa katika mikutano iliyoandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kuisaliti CCM huku akijua kuwa yeye ni kiongozi wa kutolewa mfano ikitolewa mwaka 2014 ambapo alitamka kwenye jukwaa la CUF kwamba Serikali tatu ndiyo msimamo wa Wazanzibari wote.


Mada mbalimbali zinazomhusu Mzee Moyo

- Mzee Hassan Nassor Moyo: Kauli yake juu ya Muungano na hatma ya Uanachama wake ndani ya CCM
- CCM yamvua Uanachama Mzee Hassan Nassor Moyo
- RAI: MASWALI na MAJIBU; HASSAN Nassor Moyo: Sio rahisi kuuvunja Muungano huu
 
MZEE HASSAN NASSOR MOYO AFARIKI

Innalillah Wainna Ilaiyh Rajioun Allah ampe kauli thabit amsamehe makosa yake.View attachment 1540837

Sent from my ANE-LX1 using JamiiForums mobile app
View attachment 1540852View attachment 1540853
RIP Mzee Nassor Moyo.
Ni huyo wa kulia.
Alikuwa ni wale wazee waliokuwa mstari wa mbele katika harakati za mapinduzi ya Zanzibar na pia alishakuwa waziri wa mambo ya ndani kipindi cha Nyerere.
Ni hayo machache toka kwangu kabla ya mtoa mada kutujuza zaidi.
 
Back
Top Bottom