Mkuu.
Kama huelewi Content ya Hii Thread ni Bora ukakaa Kimya.
Thread ime pose a Challenge to TCRA based on Facts nilizo Mention na Sio kwa Mwarabu
Kama hujui ni Bora ukaomba Kuelimishwa, Vitu nilivyoleta ni very Basics kueleweka.
Uliza Mkuu, sio Ujinga, Acha Ulofa
Huyu gamba Mkirindi umemjibu nilivyotaka sijui katoka kunywa mapuya(Pombe ya mahindi) haina ustaarabu hata kidogo!i was about to answer then.....!Mkuu.
Kama huelewi Content ya Hii Thread ni Bora ukakaa Kimya.
Thread ime pose a Challenge to TCRA based on Facts nilizo Mention na Sio kwa Mwarabu
Kama hujui ni Bora ukaomba Kuelimishwa, Vitu nilivyoleta ni very Basics kueleweka.
Uliza Mkuu, sio Ujinga, Acha Ulofa
Mleta mada heshima mbele.
Huo mtambo ni moja ya "rural telecomms stations" na huyo mwarabu atakuwa amenunua huo mtambo wa BTS na kuuweka hapo ulipo kwa kuwa inawezekana.
Pia atakuwa ama aliomba na kapewa ama kibali cha "network facility" au "network service" ambacho ni cha miaka 25 na kodi yake hulipwa kila mwaka pamoja na "royalty fee" ambayo kwa huyo mwarabu ni vijisenti tu kidogo.
Kwa kutegemea na mfumo au "structure" yake huo mtambo, unaweza kutumika maeneo ya vijijini, kwenye kamji kadogo au kwenye mji kamili.
Pia atakuwa anatafuta namna ya kupata subscribers walipo karibu nae ili afanya biashara kama ya kutoa huduma ya video au data.
Ila maswali yako ni ya msingi kwamba amepataje kibali cha kuweka mtambo huo mahali hapo.
Sasa kama kuna mobile operator ambae kwa namna moja au nyingine anashirikiana na mtambo huo, basi huo utakuwa ni wizi na dhuluma kwa kuwatoza wananchi shs 1000 bila wananchi kuwa na taarifa.
Ushauri kwa wamiliki wa mobile users ni kwamba inabidi wazime data roaming option pale wanapokuwa hawatumii huduma hiyo mpaka pale unapoihitaji hasa kwenye kupakua na kusoma emails na texts.
TCRA haipo kwa ajili ya wananchi wa kawaida ila kwa watu fulani wasio na nia njema kwa watanzania kwani huwezi kumtoza mtu pesa nyingi kwa ajili tu ya kupokea simu ilhali yupo hapohapo nchini mwake na anatumia mtandao tofauti.
Vema Mkuu
Ni Kweli Kabisa, ila inategemea Profile ya Mteja (SIM card) iko na Status gani kwenye HLR (Samahani kama nazidi Kukupoteza)
Kama iko on, Uta Roam tu utake usitake,nina uhakika kwa wale wanaolalamika, Profile zao ni Roamer = YES, kama iko off, kamwe hautaweza Ku Roam, hata kama uko Mbele ya Antenna.
Swali Jingine kwa TCRA...
Huyu Mwarabu ana Transimit kwenye Frequency gani??? na nani Kampa???na nani ana m Regulate???
UAE Communications Regulatory Authority ama????
Kama ni kweli, hii si ni sawa Mtu anakuja Ku Mregulate Mke wake Ndani ya Chumba Chako???
TCRA ni Member hapa JF nashangaa mpaka sasa wako kimya kama vile hawapiti hapa.
Hoja ni za msingi tu maana kwakweli watu wana
shangaa Nchi hii kila kitu usanii,sasa Usomi
pamoja na wasomi kwenye nafasi hizi nazo ni
mzigo kwa wananchi.
Mods tunaomba ufanye utaratibu wa haraka
kuwajulisha TCRA waje kujibu hoja.
Yaani naamini hata Twiga wakiondoka
hivi hivi sasa tunadanganywa hatua zina
chukuliwa mpaka leo.
Viongozi hawa watoe msaada wa kujibu:-
Mh JJ Mnyika
Mh J Makamba
Mh M Mbalawa
Mh Zito K
Mh Nnauye
Mh Kugwangala
Tanzania sasa umebaki mifupa mitupu.
cc TCRA
Kulingana taarifa na rekodi zetu, tatizo hili lilikuwepo miaka mitatu iliyopita (2009) na lilitatuliwa baada ya leseni ya mawasiliano kutolewa na kuzuia kutumika kwa mtambo uliopelekea wakazi Wa Loliondo kufanya roaming ndani ya nchi yao. Mmhusika alipewa leseni na tangu wakati huo hakuna taarifa yeyote ya roaming kwa wananchi wa loliondo kwa sasa. Ofisi yetu ya kanda pamoja Na maafisa toka Makao Makuu wakati huo walithibitisha kuwa kulikuwa na tatizo hilo wakati huo na lilitatuliwa. Kama hii taarifa ni sahihi kwa sasa, Mamlaka itafanya uchunguzi Na kuchukua hatua za kisheria kwani ni kosa kufanya hivyo. Tunaahidi kuleta taarifa hii mara ikithibitika pamoja Na hatua zitakazochukuliwa. Jambo hili linakatazwa Kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki Na Posta No. 3 ya Mwaka 2010 pamoja Na Kanuni zake.
Endapo itabainika kuwa hali hii imejirudia tena, basi TCRA itachukua hatua kali kama ilivyofanya mwanzo. Tunaahidi kutoa taarifa baada ya uchunguzi.
Asante Kwa taarifa hizi.
Safi sana TCRA kwa kuja na ufafanuzi kuhusu
hili suala maana ktk mchango wangu niliwataja
nikijua wazi ninyi ni Member hapa jamvini.
Hala hala msichelewe kija na majibu yenye
ufumbuzi kumaliza kero Loliondo.
Unajua kuna watu wanapita huko Loliondo
njia ya kufikisha ujumbe kwa haraka ni hapa
Tunaamini tatizo litakwisha.
TCRA waliuliza wakajibiwa kwamba jamaa wanafanya mawasiliano na familia za kwao kwa sababu wakitumia mitandao ya hapa ni ghali sana wakaruhusiwa....wamasai wakasema simu zao kuwapigia wenzao inachaji pesa nyingi sana maana inakuwa international call TCRA hawakutoa majibu ya hilo, sasa mwarabu ni bora kuliko mzawa aliyemruhusu kukaa pale....
Mkuu Bramo
Binafsi mimi nimefanya kazi kwenye Telecom Industry miaka ile ya "Tri-tel" & "MIC-mobitel" kwa miaka mitatu, kwa hiyo unapoongelea terminology the HLR na BTS na ... unakuwa upo uwanja wa nyumbani..!
Frequency gani ana-operate huyu mwarabu
Mkuu, Sidhani Jamaa Kama anamilki Kihalali, tuje kwenye PLMN, namaanisha MNC na MCC, natumia zipi???
Nimeangalia kwenye website ya TCRA, na nimeona wapo "Network Service Licensee" takribani kumi na saba (17), na ukiangalia "Ownership/Shareholding Structures" utaona kuwa "inawezekana" sana kuwa "Mwarabu wa Loliondo" anaweza kuwa anamiliki mojawapo ya hayo makampuni...! (hamna details za kutosha though)
Kwa mfano:-
Zantel - part of Etisalat
Smile Telecom - part of Al-Nahla & Atheeb
Hits-Telecom - part of Alsalam & Ekteetab
Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa ana-operate ndani ya Tanzania kisheria - as far as Telecom is concerned...!
Ahsante sana Wakuu TCRA kwa ufafanuzi wenu mzuri, endeleeni kutoa ElimuKulingana taarifa na rekodi zetu, tatizo hili lilikuwepo miaka mitatu iliyopita (2009) na lilitatuliwa baada ya leseni ya mawasiliano kutolewa na kuzuia kutumika kwa mtambo uliopelekea wakazi Wa Loliondo kufanya roaming ndani ya nchi yao. Mmhusika alipewa leseni na tangu wakati huo hakuna taarifa yeyote ya roaming kwa wananchi wa loliondo kwa sasa. Ofisi yetu ya kanda pamoja Na maafisa toka Makao Makuu wakati huo walithibitisha kuwa kulikuwa na tatizo hilo wakati huo na lilitatuliwa. Kama hii taarifa ni sahihi kwa sasa, Mamlaka itafanya uchunguzi Na kuchukua hatua za kisheria kwani ni kosa kufanya hivyo. Tunaahidi kuleta taarifa hii mara ikithibitika pamoja Na hatua zitakazochukuliwa. Jambo hili linakatazwa Kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki Na Posta No. 3 ya Mwaka 2010 pamoja Na Kanuni zake.
Endapo itabainika kuwa hali hii imejirudia tena, basi TCRA itachukua hatua kali kama ilivyofanya mwanzo. Tunaahidi kutoa taarifa baada ya uchunguzi.
Asante Kwa taarifa hizi.