JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
‘Hatujui Watoto wetu tunawapeleka wapi tunamlilia Rais wetu Samia Suluhu huko aliko atuangalie kwa hii shule ya Thaqafa sisi wengine ni wajane tunahangaika na Watoto wetu wa kike tunawapeleka wapi sisi Watoto hawa"
Afisa Elimu sekondari wa halmashauri ya jiji la Mwanza Allan Said amefika katika shuel hiyo na kuzungumza na wazazi wa wanafunzi hao na kuwataka kufuata taratibu zote za madai yao.
"Serikali inafanya kazi kwa kutumia makaratasi wewe ukisema mimi mtoto wangu amefutiwa utalizwa Ushahidi uko wapi nyie chukueni barua muende nazo mkaulize vizuri kuhusu hayo matokeo ya Watoto wenu."
Chanzo: EATV
====
UFAFANUZI WATOLEWA
Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Allan Said amesema “Matokeo ya Wanafunzi hao yamefutwa na chanzo ni udanganyifu wa matokeo, kuna barua mbazo zinaeleza wazi sababu ya matokeo yao kufutwa zilizoelekezwa kwa wazazi lakini wakakataa kuzipokea.
“Udanganyifu uliobainika ni katika majibu, mfano kuna maswali ambayo kila mwanafunzi alijibu tofauti, lakini baadaye wakaanza kukata na kjibu majibu ya aina moja, hiyo pekee inaonesha kulikuwa na mawasiliano na ndio maana wakafuta na kuandika majibu sawa.
“Huo ni uchunguzi wa awali, shule au uongozi wa shule wenyewe haujapata adhabu nyingine yoyote lakini kama ikibainika wamehusika kwa lolote nao watachukuliwa hatua kulingana na ukubwa wa kosa.
“Hatma ya Wanafunzi waliofutiwa mitihani wanaweza kuamua kujisajili tena wakiwa ‘private candidates’ na usajili bado unaendelea na unaisha mwezi huu wa pili (2023), akifaulu anapata haki sawa kama yule ambaye amefauu kawaida."