Hili ni tatizo LA kitaifa hususani maeneo ya mijini Tanzania nzima .
NEMC hili tatizo wameshindwa kulitatua
Makanisa yanapiga makelele , mabar nayo yanapiga makelele.
Nilihamaga maeneo ya kirumba kutokana na makelele ya hapo villa park kabla hajatengeneza soundproof club enzi hizo na bar ya pembeni ilikuwa inamilikuwa na jamaa alikuwa mhasibu wa jiji Jina nimemsahau .
Yaani glass zilikuwa zinagongana Kwenye kabati kutokana na mtetemo wa mziki.
Sasa hivi nimekumbana na hiyo kero , kuna sehemu nimehamia tokea 2017 ( nyumbani kwangu ) kuna mshakji tena namfahamu kafungua Lounge Ina Kama mwezi hivi ni shida kuanzia Jumatano hadi Jumapili full mziki Polisi wanapita kuchukua posho wanaondoka yaani hapa jumatatu na jumanne ndio tunalala .
Jamaa mwenyewe mcheshi nikifika Kwenye lounge yake hiyo kama yupo lazima anifate anisalimie na kumuelekeza muhudumu bili yangu yote atalipa .
Majirani wenzngu nao hivyo hivyo anawakirimu fresh hadi anatuweka dilemma ya kumwajibisha .
Ingawaje tumeamuwa tumwambie anatukera na mziki wake mkubwa hata Kama ni mkarimu aupunguze watoto wanashindwa hata kusoma au kuangalia TV kwa utulivu