Mimi nadhani ni wakati muafaka kwa viongozi wa serikali mmoja mmoja kuwa na washauri wa mambo ya kidini kama walivyo na washauri wa mambo ya kisiasa.Hii itawasaidia kupata ushauri wa mambo husika kabla hawajajitumbukiza kufanya maamuzi.Kila jambo lina lugha yake ya kulishughulikia.Kuna lugha ya kisiasa pia kuna lugha ya ki-roho.Unapoenda kushughulikia mambo ya kiroho kwa mtizamo wa kisiasa lazima utakwama tu.
Naamini kama Wasira angekuwa na washauri wa kiroho asingewasha moto huu mwanza.Mimi kama mkristo mwenye ndugu upande wa waislam,nikiwa na mnyama wa kuchinja tulizoeshwa na baba yetu kuwaita hao ndugu zetu upande wa mama ambao niwaislam waje wachinje,siyo kwa sababu ni sheria bali UPENDO ulichukua nafasi kubwa,kwamba tukichinja sisi wao hawatakula hiyo nyama na hivyo tutajiona wachoyo,tukawa tunashirikiana hivyo mpaka sasa. NARUDIA TENA,TULISUKUMWA NA UPENDO NA WALA SI SHERIA.
Pia naamini ni watanzania wengi wanaofanya hivyo kwa upendo tu na si vinginevyo.Lugha hii alitakiwa kuitumia Wasira,alipoenda mwanza akiwa kiongozi wa kwanza kujitosa kushughulikia tatizo hili,lakini badala yake akatumia ubabe waliozoea kuutumia bungeni na huo ubabe ndo umetufikisha hapa tulipo.
Ktk historia hakuna mahali ubabe uliwahi kumaliza tatizo bali huamishia chuki kutoka usoni kuamia moyoni,ambapo mtu husema nikipata mwanya nitafanya azma yangu.
Nimuulize mh.Waziri mkuu ambaye amesema kwa sasa tutaendelea na utaratibu wa waislam kuchinja kama ilivyokuwa tokea mwanzo mpaka hapo serikali itakapoamua vinginevyo,je una uhakika kwamba waislam ndio wanachinja? kama ndiyo,wale ng'ombe wa maziwa wanaoibiwa kila siku hasa Dar na tunakuta wamechinjwa na nyama imechukuliwa,wanachinjwa na waislam na hivyo umma uamini kuwa waislam ni wezi wa mifugo? Kama siyo waislam hiyo nyama inauzwa wapi wakati siyo utaratibu wetu watu wengine kuchinja? Nadhani angesema ktk kikao cha leo tumakubaliana........Hii ingetuonyesha kuwa ni mawazo ya kikao na ni muafaka.
Mimi ningetegemea wale viongozi wa dini ambao huwa nawaona kwenye runinga wakifanya makongamano ya dini zote mbili wakristo na waislam wangekuwa mstari wa mbele kushughulikia jambo hili,badala ya viongozi wa kisiasa.Wao wanajua lugha ya kiroho itakayong'oa dhana potofu kutoka mioyoni mwa waumini na siyo usoni.
Naishauri serikali ijifunze kuwatumia hao.Na pia Viongozi wa dini wanaohubiri chuki,kuanzia anayeanzisha mjadala mpaka yule wa mwisho serikali iwafutie usajili mapema,hii ndiyo kazi ya serikali na siyo kuja kusuluhisha migogoro iliyozalishwa na mambo wanayoyafumbia macho.