Pre GE2025 Mbeya: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,984
13,760
Mbeya.jpg

Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mkoa iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watukatika Mkoa wa Mbeya ni 2,343,754; wanaume 1,123,823 na wanawake 1,219,926

Mji wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni Waingereza mnamo mwaka 1927. Wakati huo dhahabu ilianza kupatikana katika milima iliyopo karibu na Mbeya hadi Chunya hivyo Mbeya ulikuwa ni mji wa mapumziko kwa Wazungu kutokana na hali yake nzuri ya hewa, hali iliyosababisha mji wa Mbeya kupewa jina la utani kama "The Scotland of Africa"

Halmashauri za Mkoa wa Mbeya

Busokelo, Chunya, Kyela, Mbarali, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini na Rungwe.

Soma Pia: Orodha ya CV za Wabunge kwa mwaka 2020 - 2025 kutoka kila mkoa Tanzania
MAJIMBO YA MKOA WA MBEYA

Lupa
: Watu 344,471
Mbarali: Watu 446,336
Mbeya Mjini: Watu 541,603
Mbeya Vijijini: Watu 371,259
Rungwe Magharibi: Watu 273,536
Busokelo: Watu 100,123
Kyela: Watu 266,426

Hali ya kisiasa

Katika uchaguzi wa mwaka 2020, Jiji la Mbeya lilishuhudia mabadiliko makubwa ya kisiasa. Ukilinganisha na chaguzi zilizopita ambapo vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, vilikuwa na nguvu kubwa, CCM ilipata ushindi mkubwa katika maeneo yote. Hali hii ilivutia mjadala wa kisiasa kwa sababu Mbeya ilikuwa mojawapo ya ngome muhimu za upinzani.

Katika jimbo la Mbeya Mjini, Tulia Ackson (CCM) alipata kura 75,225, akimshinda Joseph Mbilinyi maarufu kama "Sugu" wa CHADEMA aliyepata kura 37,591.

Majimbo mengine kama Busekelo, Kyela, Lupa, Mbalali, Mbeya Vijijini, na Rungwe yote yalichukuliwa na wagombea wa CCM.

Matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu 2025
JANUARI

FEBRUARI
MACHI
 
Okay
 
Back
Top Bottom