Mwanza: Pinda aagiza waislam kuendelea kuchinja...

Pwaaaa

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2013
Posts
248
Reaction score
67
Si muda mrefu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amemaliza kikao chake na Masheikh pamoja na Maaskofu hapa Mwanza katika ukumbi wa BoT kuhusu nani achinje kitoweo.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu nani hasa mwenye uhalali wa kuchinja wanyama kati ya Wakiristo na Waislam, Waziri Mkuu, Pinda amesema mazoea ya tangu zama za kale yanayowaruhusu Waislamu kuchinja yaendelee hadi hapo maamuzi mengine yatapofikiwa na Serikali.

Ameagiza pia kuundwa kamati maalumu itakayohusisha pande zote mbili za Waislamu na Wakiristo, ambayo itashughulikia mgogoro huo, na kamati hiyo iundwe na kufanyakazi zake na kukamilisha haraka sana!.

Zaidi soma -> Pinda ‘aelemewa' mgogoro wa nani achinje nyama | Fikra Pevu
 
Mi hata sishangai kwani ni kitabu gani cha MUNGU kati ya TORATI, ZABURI, INJILI na QURAN ambacho kimeandika Mkristo achinje ? Na wapi (katika vitabu tajwa hapa juu ) wameandika kuwa UKRISTO ni dini ?
 
Nadhani iko haja ya kuangalia chimbuko la tatizo maana tukigeneralise kwa kutumia maandiko tutaingilia ibada za watu na baadae watu watachelea kula kwenye dhifa za kitaifa,misiba na shughuli mbalimbali hata kujumuika majumbani mwa watu kwani hakuna uhakika nani amechinja...tusifike huko na tusipuuzie hizi cheche ndogo za udini tayari maisha yamepotea....unanikumbusha wimbo flani 'wauguuuzi, daktari na manesi wauguzi....taratibu jamani haya! Tutaonana wabaya haya !'
 
Si muda mrefu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amemaliza kikao chake na Masheikh pamoja na Maaskofu hapa Mwanza katika ukumbi wa BoT kuhusu nani achinje kitowe.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu nani hasa mwenye uhalali wa kuchinja wanyama kati ya Wakiristo na Waislam, Waziri Mkuu, Pinda amesema mazoea ya tangu zama za kale yanayowaruhusu Waislamu kuchinja yaendelee hadi hapo maamuzi mengine yatapofikiwa na Serikali.

Ameagiza pia kuundwa kamati maalumu itakayohusisha pande zote mbili za Waislamu na Wakiristo, ambayo itashughulikia mgogoro huo, na kamati hiyo iundwe na kufanyakazi zake na kukamilisha haraka sana!.

Haya ni maamuzi ya Pinda au makubaliano ya kikao?
 
sasa jaman waziri amekoroga nini hapo? Mimi ni mkristo na katika hili ningewaomba wenzangu kuwa na hofu ya mungu maana kwetu kuchinja hakuna maana yeyote mpaka kupigana uvumulivu uko wapi? Kama tukiachana na huu mtindo wa jino kwa jino naamin tukirudi ktk vitabu vyetu vinavyotutaka kutoa na shavu langine baada ya kupigwa kofi lilotangulia!
 
Pinda ni haki ayakoroge; ana hulka ya uongo na mshirika wa dhaifu JK kuiislimisha Tz. Lo lote na liwe watu wana uhuru wa kula nyama iliyochinjwa kwa imani yao. Sili makafara ya kuchinjwa kiislamu.
 
Wewe mleta mada ni mchochezi na una matatizo, alipoharibu Pinda ni wapi? Mwanzoni alilaumiwa Wassira kwa kuwa alisema kuchinja ni Ibada kwa waislam, hivyo sio rahisi kwa Wakristo kushiriki ibada isiyowahusu. Mizengo amesema ni mazoea na utaratibu uliopo hadi hapo Serikali itakapo badirisha, sasa alipoharibu ni wapi? Mbona nyie Wakristo hamueleweki mnataka nini
 
kwa style hi, nchi zenye wakristu watupu itabidi ziwe zina-import wachinjaji kutoka nchi za kiislamu

This is a non issue na serikali ilitakiwa kukaa pembeni kabisa from the beginning

community yangu itaamua yenyewe, sitakiwi kupangiwa mchinjaji.............

I was in Sudan about 10 years ago na katika discussions hili suala lilikuja na jamaa ambaye ni muislamu safi alijibu kwamba anayetakiwa kuchinja ni mtu anayeamini kuna Mungu, na wapo waislamu wengi sana hawastahili hata kuchinja
 
Mi hata sishangai kwani ni kitabu gani cha MUNGU kati ya TORATI, ZABURI, INJILI na QURAN ambacho kimeandika Mkristo achinje ? Na wapi (katika vitabu tajwa hapa juu ) wameandika kuwa UKRISTO ni dini ?

unajua maana ya neno DINI????
 
Kati ya vitabu hivyo ni kipi kimeagiza Waislamu wachinje kwa niaba ya serikali.

Vitabu vyoote vimeagiza MUISLAM achinjee kwani yeye ndiye mwenye kibali kutoka kwa MUNGU na pia wamefundishwa wakichinja wasemeje..!

Soma Agano la kale utapata majibu
Sio maandiko yenu yanayochapishiwa Dodoma hayoo !
 
Si muda mrefu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amemaliza kikao chake na Masheikh pamoja na Maaskofu hapa Mwanza katika ukumbi wa BoT kuhusu nani achinje kitowe.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu nani hasa mwenye uhalali wa kuchinja wanyama kati ya Wakiristo na Waislam, Waziri Mkuu, Pinda amesema mazoea ya tangu zama za kale yanayowaruhusu Waislamu kuchinja yaendelee hadi hapo maamuzi mengine yatapofikiwa na Serikali.

Ameagiza pia kuundwa kamati maalumu itakayohusisha pande zote mbili za Waislamu na Wakiristo, ambayo itashughulikia mgogoro huo, na kamati hiyo iundwe na kufanyakazi zake na kukamilisha haraka sana!.

duh kumbe serikali ndiyo inaamua nani achinje! Basi wapendekeze wapagani wafanye hiyo kazi.
 
Mimi nashauri waendelee kuchinga wachinjaji wa siku zote. Lakini naonya kwamba kuchinja nguruwe, ng'ombe, mbwa, ngamia, n.k. hakumpeleki mtu yeyote mbinguni. Usipomwamini Yesu Kristo, upo safarini kwenda jehanam kwenye mateso ya milele, regadless umeua viumbe wangapi.
 
Vitabu vyoote vimeagiza MUISLAM achinjee kwani yeye ndiye mwenye kibali kutoka kwa MUNGU na pia wamefundishwa wakichinja wasemeje..!

Soma Agano la kale utapata majibu
Sio maandiko yenu yanayochapishiwa Dodoma hayoo !

Naomba aya ya agizo hilo la Waislamu wachinje kwa niaba ya serikali
 
kwangu nachinja mwenyewe, kila weekend. msiniletee upuuzi wa kupuuzi. iam a christian, na kila weekend unakuja kula kuku kwangu, hujui anayechinja au unajifanyisha? kama vipi usije kwangu.
 
kwa style hi, nchi zenye wakristu watupu itabidi ziwe zina-import wachinjaji kutoka nchi za kiislamu

This is a non issue na serikali ilitakiwa kukaa pembeni kabisa from the beginning

community yangu itaamua yenyewe, sitakiwi kupangiwa mchinjaji.............

I was in Sudan about 10 years ago na katika discussions hili suala lilikuja na jamaa ambaye ni muislamu safi alijibu kwamba anayetakiwa kuchinja ni mtu anayeamini kuna Mungu, na wapo waislamu wengi sana hawastahili hata kuchinja
Heheehee tz utapata tenda ya kusafirisha wachinjaji nyama kwa wingi sana,
 
Mi hata sishangai kwani ni kitabu gani cha MUNGU kati ya TORATI, ZABURI, INJILI na QURAN ambacho kimeandika Mkristo achinje ? Na wapi (katika vitabu tajwa hapa juu ) wameandika kuwa UKRISTO ni dini ?
njoo unichinjie mbuzi katoliki kwani nyie mmekazwa kula, sio kumchinja uyo mkuu wa meza
 
Vitabu vyoote vimeagiza MUISLAM achinjee kwani yeye ndiye mwenye kibali kutoka kwa MUNGU na pia wamefundishwa wakichinja wasemeje..!

Soma Agano la kale utapata majibu
Sio maandiko yenu yanayochapishiwa Dodoma hayoo !

Wewe unaota? Dini ya kiislamu imekuwepo baada ya Yesu kristo. Ina maana kabla ya dini ya kiislamu kuwepo ilikuwa hakuna uchinjaji? Acha kuiiaibisha hiyo avatar yako!!!

Tiba
 
Back
Top Bottom