Mwanza: Meli ya MV Victoria yawaka moto!

Mwanza: Meli ya MV Victoria yawaka moto!

Pole sana wasafiri mliotarajia kusafiri nayo leo, lakini tushukru imeungua kabla haijaondoka maana ingeungua katikati ya maji ,Mungu ndiye anajua
 
Ingeteketea tu yote ili tupate mpya!
 
NB. Chanzo cha moto huo bado kujulikana, na hasara ya saga hilo bado kujulikana. Natawajulisha in case of any update.
Tunaendelea kuwa uvumilivu sana kungoja ahadi ya Mhe sana Dr. Alhj?? Mwenyekiti Jk aliyotupa kuwa katika awamu yake ya 2 atahakikisha anaweka meli mpya katika ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika. Tunajua mpenzi wetu Mhe sana rais anakumbuka na iko siku ataitimiza!!! Watakaokufa kabla ya kutimia kwa ahadi hiyo RIP.
 
Mchana huu nikiwa nimemaliza msosi wangu wa mchana, wali sato wa kurumangia, nikiwa nashushia juice ya maembe, nilinusa harufu nzito sana ya kama moshi wa kitu kizito kinaungua. Baada ya kuhangaika kujua moshi unatokea wapi, nikashtuka kuona moshi mkali ukitokea bandarini KEMONDO/KAMANGA kumbe meli ilikuwa inaungua moto.

Meli hiyo iliyosalia ya serikali ifanyayo safari za Bukoba Mwanza, imewasili lea asubuhi ikitokea Bukoba, nadhani walikuwa katika marekebisho madogomadgo ili kujiandaa na safari ya jioni kurudi bukoba.

Askari wa Jeshi la Polisi ndio waliokuwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kusaidia na wasimamizi wa meli, walifanikiwa kuudhibiti moto ule usilete madhara makubwa zaidi.

Fire wamefika hali ishatulizwa na moshi ukiwa hauonekani tena.

Tumezuiliwa kuingia wakihofu vibaka waliokuwa eneo la tukio kuhamisha mali zinazosombwa kwa ajili ya safari ya jioni. picha baadhi ni zifuatazo.

NB. Chanzo cha moto huo bado kujulikana, na hasara ya saga hilo bado kujulikana. Natawajulisha in case of any update.
Mkuu hapo kwenye Red mbona unatuchanganya?!!

Hizo Bandari ni vitu viwili tofauti na Mwanza. Kemondo iko Bukoba (ni bandari ya mwisho kabla hujafika Bukoba ukiwa unatokea Mwanza) na Kamanga ni Bandari ya kivuko iliyoko huko Sengerema (ng'ambo ya pili ukiwa pale Mwanza North Port).
 
Wana Mwanza na Bukoba msihofu. Rais wenu aliahidi ya kuwa atawanunulia Meli mpya, kubwa na ya kisasa. Sijui ni lini, maana aliahidi meli nyingine ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa na Chunya Mjini. Sijajua wengine kama wameshapata. lakini kikubwa amesisitiza kutimiza ahadi yake kabla hajaondoka ili tumuite mzee wa Maendeleo.
 
Wasije wakawa walikuwa wanachomelea vyuma au gesi ya kupikia jikoni, maanake Waswahili wakati mwingine tunafanya mambo ya ajabu sana.
 
Mkuu hapo kwenye Red mbona unatuchanganya?!!

Hizo Bandari ni vitu viwili tofauti na Mwanza. Kemondo iko Bukoba (ni bandari ya mwisho kabla hujafika Bukoba ukiwa unatokea Mwanza) na Kamanga ni Bandari ya kivuko iliyoko huko Sengerema (ng'ambo ya pili ukiwa pale Mwanza North Port).

Asante sana kwa kukundua huo ubabaishaji wa huyu kijana meri mv bukoba ikiwamwanza inaweka nanga kwenye bandari ya mwanza north port. Siyo bandari yoyote kati ya hizo alizotaja.
 
Wakati wa Mkapa, ajari ya MV Bukoba, treni na yeye kukoswakoswa ajalini Mza watu walisema jamaa ana gundu. Hapa tusemeje kwa JK! Gundu, mikosi, nuksi, matambiko au....au...au...
 
Wakati wa Mkapa, ajari ya MV Bukoba, treni na yeye kukoswakoswa ajalini Mza watu walisema jamaa ana gundu. Hapa tusemeje kwa JK! Gundu, mikosi, nuksi, matambiko au....au...au...

Wiki ya moto
 
hiyo meli yenyewe...imechoka jamani....! any time bomb
 
Back
Top Bottom