Wakuj,
Ninapoandika hapa ni kuwa Meli ya MV Victoria ifanyayo safari zake kati ya Mwanza na Bukoba inaungua moto bandarini Mwanza. Zimamoto ndio wanaelekea eneo la tukio na nitajitahidi kuwafahamisha kinachojiri na hata kupandisha picha.
Zimamoto wamefika, moto umetokea sehemu ya chini wanakoweka mizigo. Moshi unafuka mwingi, wakifanikiwa au kuchemsha kuuzima nitawajuza.
More updates to follow
Hii meli ijichokea sana kiasi kwamba hata kufanya safari mto pangani haiwezi achilia mbali ziwa victoria ambalo ni kubwa na vimbwanga vya kutosha.
Lakini ndo hivyo tutaishia kusema kazi ya Mungu haina makosa.
Kama ni hivyo bora safari ya leo usiku isiwepo kwanza mpaka wapate uhakika wa chanzo cha moto
MV Victoria is a Lake Victoria ferry operated by the Marine Services Company Limited of Tanzania.[SUP][2][/SUP] Until Kenyan independence from the United Kingdom in 1963 she was the Royal Mail Ship RMS Victoria.[SUP][4][/SUP]Hii meli inanizidi umri kwa mbali sana. Nimezaliwa nimeikuta na sasa nazeeeka yenyewe bado imo tu inabeba abiria!!!!
Tiba
Bora iungue labda tutapata meli nyingine. Meli moja tangu nikiwa mtoto ni MV Victoria. Shame kwetu Tanzania. Kikwete alihaidi meli mpya Ziwa Victoria wakati wa kampeni, tunapata sababu nyingine ya kuikataa CCM
Mchana huu nikiwa nimemaliza msosi wangu wa mchana, wali sato wa kurumangia, nikiwa nashushia juice ya maembe, nilinusa harufu nzito sana ya kama moshi wa kitu kizito kinaungua. Baada ya kuhangaika kujua moshi unatokea wapi, nikashtuka kuona moshi mkali ukitokea bandarini KEMONDO/KAMANGA kumbe meli ilikuwa inaungua moto.
Meli hiyo iliyosalia ya serikali ifanyayo safari za Bukoba Mwanza, imewasili lea asubuhi ikitokea Bukoba, nadhani walikuwa katika marekebisho madogomadgo ili kujiandaa na safari ya jioni kurudi bukoba.
Askari wa Jeshi la Polisi ndio waliokuwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kusaidia na wasimamizi wa meli, walifanikiwa kuudhibiti moto ule usilete madhara makubwa zaidi.
Fire wamefika hali ishatulizwa na moshi ukiwa hauonekani tena.
Tumezuiliwa kuingia wakihofu vibaka waliokuwa eneo la tukio kuhamisha mali zinazosombwa kwa ajili ya safari ya jioni. picha baadhi ni zifuatazo.
Nadhani jamaa alipata matatizo ya kufokas kamera yake!mbona naona picha za mrembo tu,au ndio m.v victoria yenywe
Nadhani jamaa alipata matatizo ya kufokas kamera yake!
Kuna mfanyakazi wa pale nimeongea nae safari ya leo ipo kama kawaida tatizo lilikuwa minorsi rahisi kwa leo kuwa na safari hiyo, mpaka watengeneze. kwa moto ulivyokuwa mkubwa, pamoja na kwamba umedhibitiwa, lazima kuna vitu vimeungua tu. na vitahitaji matengenezo ya kweli kurudi kwenye hali yake.