Mwanza: Meli ya MV Victoria yawaka moto!

Mwanza: Meli ya MV Victoria yawaka moto!

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,028
Reaction score
2,734
Wakuj,

Ninapoandika hapa ni kuwa Meli ya MV Victoria ifanyayo safari zake kati ya Mwanza na Bukoba inaungua moto bandarini Mwanza. Zimamoto ndio wanaelekea eneo la tukio na nitajitahidi kuwafahamisha kinachojiri na hata kupandisha picha.

Zimamoto wamefika, moto umetokea sehemu ya chini wanakoweka mizigo. Moshi unafuka mwingi, wakifanikiwa au kuchemsha kuuzima nitawajuza.

Wamefanikiwa kuuzima moto kwa kutumia vizima moto vilivyokuwa ndani ya meli, lakini bado mali iliyoharibika haijaweza kutajwa na thamani yake.

More updates to follow
 
Mkuu n00b nakuaminia sana!! Ubarikiwe tunasubiri picha na updates!!
 
HII meli si imechoka sana??
th
 
Hii meli ijichokea sana kiasi kwamba hata kufanya safari mto pangani haiwezi achilia mbali ziwa victoria ambalo ni kubwa na vimbwanga vya kutosha.
Lakini ndo hivyo tutaishia kusema kazi ya Mungu haina makosa.
 
Engine ni ya diesel. Cha ajabu ipo majini. Inashindwa ku-pump maji ya ziwa na kujizima huo moto. Hivi haya ndio maendeleo ya miaka 51 ya uhuru.
 
Ni KWA SABABU RAISI TULIE NAE HAKUWA CHAGUO LA WA TANZANIA HATA KIDOGO!
umenitoa usingizini mkuu, kumbe kuna 'chaguo la miungu' na 'chaguo la watanzania'!!

Hiyo meli leo inapakia kuja kwetu huku, Mungu apishe mbali, au ndio hawa magmb wanaendelea kutumia haya majanga ya moto kudivert attention ya Gesi na Bunge!!?

 
wiki ya moto bado inanaendelea?HALI ENEO LILILOKUWA LIWA MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO PALE SAYANSI NYUMA YA ttcl ROSE GARDEN,MAMA ANA MKAPA ALIMUUZIA NDUGU YAKE zadoK KWA BEI YA KUTUPA 300M,KWA KUPITIA KAMPUNI FEKI YA SIM2000
 
Nijuavyo mimi meli huwa zina Automatic fire fighting system. Hii imekuaje hadi wanasubiri magari ya faya yaje tena na maji kutoka mjini wakati meli yenyewe iko majini.

Hii inanikumbusha meli moja ilikuwa inawaka moto pale bandarini, magari ya faya yakawa yanatoka mjini yakifika ferry yanapakiwa kwenye pantoni halafu pantoni inayapeleka kuzima moto kwenye ile meli bandarini. Maji yakiisha pantoni inarudi hadi kivukoni, magari yanashushwa yanaenda kufuata maji, yanarudi tena...mzunguko unaendelea.

Mambo mengine ni kama hadithi za kusadikika lakini ndo hivyo yanatokea Bongo. Ukimsimulia mtu mwerevu huenda asiamini.
 
Kuna kifaa kinaitwa dspa 5

Walisha tangaziwa kununua kuanzia watu wa zima moto wenyewe wawe navyo lakini Nyambacha na wengine wako bize na safari na kujilipa .Majengo kama PPF kuungua walitakuwa na dspa automatic lakini watanzania wamefanya zengwe hadi wazungu wamerudi kwao na mtanzania alye waleta tanzania kavuna aibu .Hata baada ya Katibu mkuu kusema wanunue wawe navyo kwa ajiili ya moto Mh.Abdulwakil lakini watu wa Fire wakaingia mitini hata sasa .Adhabu sasa na wanawezaje kuzima moto ?

ingia hapa

YouTube

search neno dspa

utaona kazi yale lakini serikali hata kuwazia hakuna hadi moto ufike ndiyo hasara ya kuuzima mwa maji inaanza .
Nyenzo za kuzima moto zipo ila umimi na 10% inaumiza na urasimu .Waambie wawapigie jamaa wa vifaa vya moto namba zao ni 0767 554433 wapate msaada .
 
Hii meli ijichokea sana kiasi kwamba hata kufanya safari mto pangani haiwezi achilia mbali ziwa victoria ambalo ni kubwa na vimbwanga vya kutosha.
Lakini ndo hivyo tutaishia kusema kazi ya Mungu haina makosa.

Wataunda tume badae huenda tukasikia ni Cdm wamehusika na hujuma hiyo
 
Mchana huu nikiwa nimemaliza msosi wangu wa mchana, wali sato wa kurumangia, nikiwa nashushia juice ya maembe, nilinusa harufu nzito sana ya kama moshi wa kitu kizito kinaungua. Baada ya kuhangaika kujua moshi unatokea wapi, nikashtuka kuona moshi mkali ukitokea bandarini KEMONDO/KAMANGA kumbe meli ilikuwa inaungua moto.

Meli hiyo iliyosalia ya serikali ifanyayo safari za Bukoba Mwanza, imewasili lea asubuhi ikitokea Bukoba, nadhani walikuwa katika marekebisho madogomadgo ili kujiandaa na safari ya jioni kurudi bukoba.

Askari wa Jeshi la Polisi ndio waliokuwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kusaidia na wasimamizi wa meli, walifanikiwa kuudhibiti moto ule usilete madhara makubwa zaidi.

Fire wamefika hali ishatulizwa na moshi ukiwa hauonekani tena.

Tumezuiliwa kuingia wakihofu vibaka waliokuwa eneo la tukio kuhamisha mali zinazosombwa kwa ajili ya safari ya jioni. picha baadhi ni zifuatazo.


DSC_00220.jpg

DSC_00221.jpg

DSC_00222.jpg

DSC_00223.jpg

NB. Chanzo cha moto huo bado kujulikana, na hasara ya saga hilo bado kujulikana. Natawajulisha in case of any update.
 
binafsi kwangu ni habari njema sana kusikia kuwa m.v victoria inaungua moto,nikiwa muwazi watanzania wanaotumia meli hizi,m.v victoria,clarias na butyama na serengeti wanasubiri majanga tu kama ya m.v bukoba.hizi meli zimechoka sana lakini kama mjuavyo hapa kwetu mpaka iue ndo hapo inakuwa out of service.binafsi nimezitumia baadhi ya meli hizi hasa clarias,serengeti na butyama,kuna wakati meli inazumika katikati ya bahari,na kuna wakati m.v clarias ilikuwa inatoka ukerewe kwenda mwanza,ilipotoka tu bandarini baada kama ya robo saa hivi ikawa inarudi,baada ya kutia nanga ndo watu wakaambiwa kuwa meli ilikuwa imtiboka,hebu imagine huo mfarakano wa kutoka ndani ya meli.so kwa ujumla ni bora kuziuza kama chuma chakavu.
 
Back
Top Bottom