Mwanza: Meli ya MV Victoria yawaka moto!

Mwanza: Meli ya MV Victoria yawaka moto!

afadhali kama akuna madhara kwa binadam..ivi vyombo vyetu vya majii..Mungu atusaidie
 
Mwenyezi mungu tuepushie majanga nchini mwetu!
 
duh poleni wahuska wajpange upya mwakyembe aache vsasi kwenye ulaji bandarin aangalie ununuzi wa meli mpya bandarin anataftia ndugu zake ulaji tu cz hili kabla linafahamika ata mwalimu analijua
 
binafsi kwangu ni habari njema sana kusikia kuwa m.v victoria inaungua moto,nikiwa muwazi watanzania wanaotumia meli hizi,m.v victoria,clarias na butyama na serengeti wanasubiri majanga tu kama ya m.v bukoba.hizi meli zimechoka sana lakini kama mjuavyo hapa kwetu mpaka iue ndo hapo inakuwa out of service.binafsi nimezitumia baadhi ya meli hizi hasa clarias,serengeti na butyama,kuna wakati meli inazumika katikati ya bahari,na kuna wakati m.v clarias ilikuwa inatoka ukerewe kwenda mwanza,ilipotoka tu bandarini baada kama ya robo saa hivi ikawa inarudi,baada ya kutia nanga ndo watu wakaambiwa kuwa meli ilikuwa imtiboka,hebu imagine huo mfarakano wa kutoka ndani ya meli.so kwa ujumla ni bora kuziuza kama chuma chakavu.
Tuziuze kwa TZS 500,000/= kama zile ndege..
 
kweli afadhali imeungua kwa kuwa sana sana tutapoteza vyuma, ikizama ndo tutawapoteza watanzania, ni vema kama serikali haina mpango wa kununua nyingine, hizi zingine zikatiwa kibiriti badala ya kusubiri kuzamisha watu.
 
Kama ni hivyo bora safari ya leo usiku isiwepo kwanza mpaka wapate uhakika wa chanzo cha moto
 
Wakuj,

Ninapoandika hapa ni kuwa Meli ya MV Victoria ifanyayo safari zake kati
ya Mwanza na Bukoba inaungua moto bandarini Mwanza. Zimamoto ndio
wanaelekea eneo la tukio na nitajitahidi kuwafahamisha kinachojiri na
hata kupandisha picha.

Zimamoto wamefika, moto umetokea sehemu ya chini wanakoweka mizigo.
Moshi unafuka mwingi, wakifanikiwa au kuchemsha kuuzima nitawajuza.

More updates to follow

taarifa za uhakika moto umedhibitiwa. ulitokana na cheche za mafundi waliokuwa wakichomelea. inajiandaa kwa safari ya bukoba.
 
daha utasikia zima moto hawakuwa na maji
 
Hii nchi ina mengi ya ajabu na ya kusimulia, baadae utasikia mara ooohh ilikuwa imesimamishwa kutoa huduma lakini wakakaidi!!
 
Taarifa nilizosikia moto umeshazimwa na safari ya leo usiku ipo kama kawaida
 
HII meli si imechoka sana??
th

dah! Inawaka moto ziwani? Hatari!
 
JK ataleta nyingine hakuna shida ............... Singapore sasa wanaunda meli mbili za TZ, moja ya ziwa Tanganyika na Nyingine ziwa Malawi opps ziwa Nyasa kama Manifesto ya CCM inavyosema!!
 
Nijuavyo mimi meli huwa zina Automatic fire fighting system. Hii imekuaje hadi wanasubiri magari ya faya yaje tena na maji kutoka mjini wakati meli yenyewe iko majini.

Hii inanikumbusha meli moja ilikuwa inawaka moto pale bandarini, magari ya faya yakawa yanatoka mjini yakifika ferry yanapakiwa kwenye pantoni halafu pantoni inayapeleka kuzima moto kwenye ile meli bandarini. Maji yakiisha pantoni inarudi hadi kivukoni, magari yanashushwa yanaenda kufuata maji, yanarudi tena...mzunguko unaendelea.

Mambo mengine ni kama hadithi za kusadikika lakini ndo hivyo yanatokea Bongo. Ukimsimulia mtu mwerevu huenda asiamini.

Hii yako kali, magari yanarudishwa ngambo na pantoni ili yakafuate maji mjini..!!!?
 
Hii yako kali, magari yanarudishwa ngambo na pantoni ili yakafuate maji mjini..!!!?
Mkuu hii ni bongo...Ukiwa ni mtu wa kushangaa basi utajikuta kila siku we ni mtu wa kushangaa tu. Maajabu hayaishi.
 
Back
Top Bottom