Mwanza City: The Photo Gallery

Mwanza City: The Photo Gallery

Majaliwa kufanya Ziara ya Kikazi ya Siku nne Mwanza

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) anatarajiwa kuwasili Mkoani Mwanza Jumamosi ya Oktoba 15, 2022 Majira ya saa 10 jioni kwa ziara ya kikazi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Kighoma Malima wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkoa mapema leo alhamisi Oktoba 13, 2022.

Mhe. Malima ametumia wasaa huo kuwakaribisha wananchi wa Mwanza na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kandokando ya barabara na kwenye Miradi atakayoitembelea kumlaki na kumpokea Kiongozi huyo ambaye atakuwepo mkoani humo kwa ziara ya siku nne.

"Nawaomba wakaazi wa Mwanza tuoneshe uzalendo wa dhati, sote tuungane kumpokea Mgeni wetu na tumwoneshe mapenzi ya dhati huku tukiishukuru Serikali kwa kutuletea Maendeleo kama tunavyoona Miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa kwenye maeneo yetu." Mkuu wa Mkoa.

Akizungumzia ratiba ya ziara amesema ,siku ya jumapili ya Oktoba 16, 2022 kuanzia Majira ya saa 2 asubihi Mhe. Majaliwa atakagua Maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Magufuli Kigongo-Busisi pamoja na kusalimia wananchi wa Busisi kabla ya kuelekea wilayani Kwimba ambako atakagua Maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa (SGR).

Malima amefafanua kuwa katika siku hiyohiyo, kuanzia Majira ya saa 7 mchana Mhe. Waziri Mkuu atazindua Jengo la Huduma ya Macho kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye uwanja wa Mahafali hospitalini hapo.

"Siku ya tatu ya ziara ya Mhe. Waziri Mkuu itaanzia Wilayani Ukerewe kwenye visiwa vya Irugwa majira ya saa 3 asubuhi ambako atakagua ujenzi wa Kituo cha Afya na Maendeleo ya Shule ya Sekondari ya Irugwa kabla ya kuelekea kisiwani Gana ambako akiwa huko atakagua maendeleo ya Ujenzi wa Zahanati pamoja na kusalimia wananchi." Amesema Mhe. Malima.

Ameongeza kuwa mara baada ya shughuli za visiwani Mhe. Waziri Mkuu atarejea Mjini Mwanza ambako anatarajiwa kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya Nyegezi kuanzia Majira ya saa 9 alasiri na baadae atawasili bandari ya Mwanza Kusini kwa ajili ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Meli ya MV Mwanza 'Hapa Kazi Tu'.
bora majaliwa aje labda baadhi ya vitu vitafichuka kama la uwanja wa ndege
 
Nkupongez umewaz vzur ila nje ya dar pia mwanz ndo jiji kubw kwhio litakua na uitaj mkubw kulingan na ukubw wake afu pili hilo daraj ukiangalia me jicho la kawaid utaon n la kawaid ila n muhmu san lkn pia ilo daraj I inshu ya mkoa sio city council city counci nayo una maitaj yke ata ivo Ilo daraj lilijengw kwa kufoc na mzee bab tu izo gharam zisngetok tu kw kiongoz mwngne nakkmbuk kikwete alitak kujeng ila sio kwa fedha za nch bal kutok nje wakakaz kua hawatowez hawatounfaika ila Jpm amefoc city ving vifanyike kw harak bil kutk kutegmea nje tatu ivo vtu vingejengw kw pmoj badal ya daraj ungeonekn ameend kujeng kwao tu nchi imehamia mwanz ivo vtu lazm vijengwe kwa awamu na kutegmea pesa iliopo na mgawanyo wa fedha nchin....lkn ata ivo izo barabr zingejengw harak zaid km th kungekuw na Jam san ila kua honesty hamn jam ivo inavoongelew ndo kitu kikubw jpokua n vzur kua na plan as badae sio lazma jam ila sera ya nch yetu ina idad ya magar yanayopita kwen njia ili ipanue barabr...ukiend dar unaon kwel kun umhum wa kupanua njia fulan n jam kwel bro sera zetu zilivo ndo maan Jpm alikua tofaut coz alifany nje ya hayo mawazo coz alion n kuchelewesh maendeleo
Tanzania tunajenga barabara Hadi tatizo Liwe kubwa ... tunajenga Kwa sababu ya jam...wenzetu wanajenga barabara Kwa ajili ya kurahisisha mfumo wa usafiri ndani ya mji .......tunapoomba njia sita lengo ni kuondoa kEro zinazoweza kutokea njiani mfano msafara wa viongozi,gari za dharula ,na mabasi ya abiria......hatuombi Kwa sababu ya jam ...isitoshe miji ya kisasa ishaacha kuwa na mono carriage...mingi Ina dual carriage,njia sita na njia nane ili kutengeneza space na mfumo salama wa usafiri
 
Na Premier hawezi kuhaidi miradi mipya zaidi ya kuhakikisha iliyopo inafanyika kwa wakati, tusitegemee ahadi ya miradi mpya zaidi ya hii iliyopo mezani
 
Halafu hata barabara ya nyerere road nayo jam imeanza kurud kama zaman kiukweli mwanza sasa hv kuna jam sana unatoka kisesa saa 12 kamili jion buhongwa unakuja kufika saa 3 kasoro uck yan mtu anatoka nyamhongolo huo mda kwenda Bunda anafika ww bado hujafika buhongwa
Nyerere road ni bomu na soon litalipuka ... hyo barabara inapokea ruti nyingi za daladala kuliko barabara zote mwanza,na idadi kubwa ya watu wenye magari wanaishi hyo road ....
 
Na Premier hawezi kuhaidi mradi mipya zaidi ya kuhakikisha iliyopo inafanyika kwa wakati, tusitegemee ahadi ya miradi mpya zaidi ya hii iliyopo mezani
Premier sio mwanasiasa
 
Kuna kiwanja changu kipo mwanza mkolani lelini pale nakiuza kama unahitaji nicheki dm yangu ukapaone
Kipo barabarani kabisa
 
Majaliwa kufanya Ziara ya Kikazi ya Siku nne Mwanza

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) anatarajiwa kuwasili Mkoani Mwanza Jumamosi ya Oktoba 15, 2022 Majira ya saa 10 jioni kwa ziara ya kikazi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Kighoma Malima wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkoa mapema leo alhamisi Oktoba 13, 2022.

Mhe. Malima ametumia wasaa huo kuwakaribisha wananchi wa Mwanza na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kandokando ya barabara na kwenye Miradi atakayoitembelea kumlaki na kumpokea Kiongozi huyo ambaye atakuwepo mkoani humo kwa ziara ya siku nne.

"Nawaomba wakaazi wa Mwanza tuoneshe uzalendo wa dhati, sote tuungane kumpokea Mgeni wetu na tumwoneshe mapenzi ya dhati huku tukiishukuru Serikali kwa kutuletea Maendeleo kama tunavyoona Miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa kwenye maeneo yetu." Mkuu wa Mkoa.

Akizungumzia ratiba ya ziara amesema ,siku ya jumapili ya Oktoba 16, 2022 kuanzia Majira ya saa 2 asubihi Mhe. Majaliwa atakagua Maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Magufuli Kigongo-Busisi pamoja na kusalimia wananchi wa Busisi kabla ya kuelekea wilayani Kwimba ambako atakagua Maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa (SGR).

Malima amefafanua kuwa katika siku hiyohiyo, kuanzia Majira ya saa 7 mchana Mhe. Waziri Mkuu atazindua Jengo la Huduma ya Macho kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye uwanja wa Mahafali hospitalini hapo.

"Siku ya tatu ya ziara ya Mhe. Waziri Mkuu itaanzia Wilayani Ukerewe kwenye visiwa vya Irugwa majira ya saa 3 asubuhi ambako atakagua ujenzi wa Kituo cha Afya na Maendeleo ya Shule ya Sekondari ya Irugwa kabla ya kuelekea kisiwani Gana ambako akiwa huko atakagua maendeleo ya Ujenzi wa Zahanati pamoja na kusalimia wananchi." Amesema Mhe. Malima.

Ameongeza kuwa mara baada ya shughuli za visiwani Mhe. Waziri Mkuu atarejea Mjini Mwanza ambako anatarajiwa kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya Nyegezi kuanzia Majira ya saa 9 alasiri na baadae atawasili bandari ya Mwanza Kusini kwa ajili ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Meli ya MV Mwanza 'Hapa Kazi Tu'.
Mbona hapelekwi kuangalia Airport?
 
Leo mkuu wa wilaya ya nyamagana na kamati yake walikuwa stand ya nyegezi Moja Kati ya vitu alivyosema ni kuwa pale magari yanaposimama kama unaenda mjin wanapaita kituo cha stand ya zaman watajenga stand ya daladala so wale wenye vibanda wameambiwa wasogeze vibanda vyao pia Sasa hv jamaa pale stand wanapiga kaz sana had uck huu wazur mkuu akija akute mambo yapo sawa
 
Je umepata fununu zozote kuhusu ufunguzi wa stendi ya nyegezi?
 
Nyerere road ni bomu na soon litalipuka ... hyo barabara inapokea ruti nyingi za daladala kuliko barabara zote mwanza,na idadi kubwa ya watu wenye magari wanaishi hyo road ....
Hivi ule mpango wa kuupanua umefikia wapi au ndio mambo ya siasa?
 
Hizi data zinafikirisha sana ... haiwezekani asilimia 86 ya mapato yote ya nchi yapo dar ...this sounds uninteresting.kinachoniuma zaidi mwanza mapato ya TRA kuwa chini ya arusha,na dodoma wanatukaribia Kwa digit pamoja ...Kuna kitu hakipo sawa ...View attachment 2386224
Bandari mkuu hayo magari au bidhaa nyingine mnayoagiza kupitia bandari ya dar, TRA wanachukua chao japo hizo bidhaa au magari ni ya watu wa mikoani, hapo Mapato halisi ya Dar(actual) utakuta ni 1 trilion, bandari ni kila kitu mkuu, kila bidhaa unayoagiza mapato ya tra yanakatiwa Dar.
 
Hii isikupe mawazo mkuu.
Ni hatari sana Kwa nchi kucentralize uchumi wake kwenye eneo Moja ......,,,,, ikitokea la kutokea dar kukatokea machafuko ,,,,nchi itayumba pakubwa sana ...tuchukulie mfano nchi za wenzetu mapato yako diversified MAENEO tofauti tofauti ,.mfano south Africa wamediversfy mapato Yao kwenye majiji ya Durban,johansburg, Capetown,na port Elizabeth...hata ikitokea johansburg imetekwa serikali inaweza kuendesha nchi tokea Capetown na mambo yakaenda
 
Nilishasema ndio maana hii nchi ina uchumi hafifu kwasababu ya Dar.
 
Leo mkuu wa wilaya ya nyamagana na kamati yake walikuwa stand ya nyegezi Moja Kati ya vitu alivyosema ni kuwa pale magari yanaposimama kama unaenda mjin wanapaita kituo cha stand ya zaman watajenga stand ya daladala so wale wenye vibanda wameambiwa wasogeze vibanda vyao pia Sasa hv jamaa pale stand wanapiga kaz sana had uck huu wazur mkuu akija akute mambo yapo sawa
Wanatakiwa wakiamua kujenga stendi wajenge na hizo frame za maduka kuliko kuacha watu wsjijengee kila mtu kwa style yake.
 
Ni hatari sana Kwa nchi kucentralize uchumi wake kwenye eneo Moja ......,,,,, ikitokea la kutokea dar kukatokea machafuko ,,,,nchi itayumba pakubwa sana ...tuchukulie mfano nchi za wenzetu mapato yako diversified MAENEO tofauti tofauti ,.mfano south Africa wamediversfy mapato Yao kwenye majiji ya Durban,johansburg, Capetown,na port Elizabeth...hata ikitokea johansburg imetekwa serikali inaweza kuendesha nchi tokea Capetown na mambo yakaenda
Tiba ni serikali za majimbo, huu ujinga wa kuamini kila kitu lazima kiwepo dar utaisha la sivyo mapato ya sehemu nyingine yataenda Dar kama ilivyo hapo.
 
Back
Top Bottom