Imagine kuna watu walitaka eti sgr ikomee fela eti tunapanua mji, nilipinga sana kaka.
Uzuri trc kumbe huwa wanaangalia na wao kwenye mitandao maana nilikuja sikia wameligusia siku moja.
Nikawauliza watu imagine unatoka shy kuja mza kwa treni sgr unatumia chini ya Lisaa kufika fela, then kutoka fela kuja mwanza unatumia masaa labda 2.
Ukichukua taxi Unaweza jikuta unalipa nauli sawa na nauli ya treni. Niliwaambia fela iwepo Station na mwanza mjini iwepo Station
Nchi za wenzetu wanajaribu kuweka hizi huduma ndani ya mji na ziko karibu karibu,
Uzuri wa Station kuwa mwanza mjini ni kuwa hapo baadae ni rahisi kufanya usafiri wa treni za mjini.
Mfano mtu anaweza kuishi kwimba na akafanya kazi mwanza mjini.
Kuna mwingine akasema eti kuna foleni kubwa sana kutoka mjini kuja nyegezi, kwahiyo stendi ikihamushwa itapunguza foleni.
Nikamjibu kumbe mabasi hayasababishi foleni maana hayafiki mjini na ukiweka stendi usagara foleni itaanzia mjini mpaka usagara maana vipanya vitaongezeka nk.
Niko UK wameanza kujenga high speed train 320km/hr hii itaunganisha miji yote ile mikubwa 3 yaani London, Birmingham na Manchester,
Pamoja na kwamba hii miji ni mipana na ina usafiri wa kila aina na barabara nyingi nzuri lakini wamehakikisha vituo vya treni vina kuwa mjini kabisa.
Mchina alishaga jaribu hsya mambo ya kupanua mji wakati anaanza kujenga reli, wakaja gundua wanachemsha kuweka vituo nje ya mji, ikabidi wajenge tena kuingiza ndani ya mji.