Mwanza City: The Photo Gallery

Hapana laizerg sio overland, yupo huwa anatokea mara moja moja kwa Jina jingine.
Sirg nakukumbuka.
 
lakini malumbano yao yanatuchelewesha sana.
Malumbano kaleta huyu mkuu wa mkoa yalikuwa yameisha, na sasa ansongeza mapya maana anataka TANAPA nao waingie Humo.

Ki ufupi hili jengo sio kwamba ndio litakuwa main terminal, hapana, hili jengo linajengwa ili shughuli zote zihamie hapo kwa sababu yale mabanda yanayotumika sasa ndio yanatakiwa kuvunjwa na terminal hiyo mpya itajengwa hapo kwenye mabanda.
Shughuli za Airport lazima ziendelee wakati ujenzi unaendelea.
Bila hili jengo kuisha ujenzi wa terminal mpya hautaanza, kwa hiyo inabidi liishe ili shughuli za Airport zihame kupisha site.
Advantage tuliyonayo kama Mwanza ni kwamba hili jengo kwa sababu ni zuri halitavunjwa hivyo tutakuwa na terminal 1 & 2.

Tatizo la viongozi mwanza huwa sio walafi wa opportunities,
Nssf walitaka kujenga nyumba kule Bugarika, yaani kungekuwa kuzuri kweli kule wakabishana mambo ya viwanja mpaka mradi ukafa.
Mifano ipo mingi ngoja nikae kimya.
 
Tena huyu mkuu wa mkoa wa sasa ndio yuko busy hatari kutaka kuonyesha Magu hakufanya kitu sijui katumwa hivyo.
Sasa hivi anahangaika na mambo Ya chanjo, naona kupoteza muda tu.
Ambacho sielewi kwa nini badala ya kufanya kazi wanahangaika na mtu aliyekufa?
 
Mimi namfahamu tangu akiwa mkuu wa mkoa wa Mara na Tanga. Maneno mengi sana kuliko vitendo
 
Siioni tatizo la mkuu wa mkoa ,,,yeye kama mwakilishi wa raisi .ni jukumu lake kufatilia miradi ya maendeleo hapo alipo ..
Kwa mujibu wa naibu waziri alitoa maagizo jengo kufikia December Liwe limekamilika .. bado miezi miwili kuona huo utekelezaji huo
 
Wakati anakuja mza ilikuwa imeshapitishwa taa wachukue jengo waendelee na mambo yao, yeye kaja anajiita financial adviser anawaambia halmashauri waongie ubia na Amesema ataconvince na tanapa waweke mzigo nao wawe wabia,
Huoni kwamba ameanzisha tatizo jingine jipya ambalo halikuwepo?
Angesema halmashauri zilipwe pesa zao then waache kila kitu kwa taa ningemuelewa.
Anachotaka kufanya ndicho kinachoi_cost rockcity mall Kwa sasa.
 
Huyu taarabu ingemfaa kuliko siasa.
Hivi yule aliyekuwepo kaondolewa sababu gani, au ulokole ulimponza?
Aliegemea mambo ya kichungaji japo alikuwa ana piga sana kazi mungu amtangulie huko haliko alikuwa ni moja kati wa wakuu wa mikoa jembe sana, eng Gabriel.
 
Mkuu hilo jengo nimepita leo hapo halina dalili za kuanza ujenzi, huyo mzee we mtete ni mtu wa maneno mengi sana kuliko vitendo.
 
TAA ni regulator,..umiliki wa jengo unatakiwa ubaki Kwa waliojenga ,, halmashauri,,TANAPA wanakuja kuwa promotor na branding organization..mkuu ataka kutengeneza link kati ya regulator ,mmiliki na promotor ambaye kupitia terminal hyo atabrand utalii wa mwanza .sion tatizo bado
 
Afanye mambo jengo liishe then kubrand kuje baadae๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Kama tanapa wanataka kubrand wajenge lile kubwa la 32b huko ndio watabrand, huku kwingine watabrand nini Wageni wa nje hawatashukia wala kupandia huko.
Utalii mza ni upuuzi tukazanie malighafi za ziwa.
Mwanza yenyewe wakizuia watu kujenga milimani, hayo mawe ni utalii tosha.
Kuna watu wengi huwa wanakuja kushangaa hayo mawe bure wanarudi makwao.
Ukitengenzwa utaratibu mzuri kama ilivyo London, halmashauri zitapiga pesa ndefu.
Watu wanajenga milimani wanawaangalia tu wakati hivyo ni nyanzo vya mapato.
 
Tatizo linaanzia kwetu sisi .wananchi kujiona ni wanyonge tunaonelewa na kuwa brainwashed na conspiracy theories,,,mwananchi akizuiwa msijenge sehemu flan ,tunasema nchi imeuzwa ,sijui wamepewa watu flani ..hili suala linafanya hata wataalamu wetu wenye mawazo Bora kukataliwa na wanasiasa wanaosimamia sera ili tu kuwafurahisha baadhi ya wananchi watakaowahakikishia ulaji ....

Dawa ya kuleta maendeleo hapa mwanza ni kuwaondoa watu ujinga walionao na wakubali mabadiliko yenye maumivu
 
Ccm ikitaka kujiharibia kura . viongozi watangaze bomoa bomoa pale mabatini .uone fitina za kisiasa zitakavyotawala Kila chama kitataka kupata agenda kupitia Hilo tukio ..
 
JPM angekuwepo sidhani kama RC angeweka kauli kwa TAA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ