Rajab Endless
Senior Member
- Oct 2, 2019
- 121
- 167
Kuna siku pia nilipiga ruti ya Airport - Nyansishi lakini nilishuka Stand ya Igombe nikaunga ruti ya Luchelele Mzunguko nilipofika pale malimbe wakagoma kwenda hadi Luchelele ikabigi nichukue boda nikashuka nayo hadi chini kule boda akaniambia hapa ndio Luchelele,
Nikashuka kwenye boda kuna center flani imechangamka pale akaniambia ukiende mbele zaidi unakutuna na sehemu ya ziwa ambako ndio daladala za Luchelele zinatakiwa kuishia huko, nikasema poa nikasubilia kama robo saa hivi nikaona hiace ya Luchelele inaenda huku boda alikoniambia,
Nikaipiga mkono nikashuka nayo hadi inapoishia, Dah nilistaajabu baada ya kukutana na mwalo flani hivi jamaa wanasema huwa kuna mitumbwi inakuja kuleta mkaa na mazao ya nafaka kutoka Geita pia wakaniambia viongozi kibao wa mkoa wa Mwanza wanamiliki viwanja maeneo hayo....