Wakuu nimeingia mwanza leo, honestly nimeona mabadiliko makunwa sana, pengine kwa mnaoishi hapa mnaweza msinielewe.
1: ukiliguru na nyang'holongo zimeshaungana na Kuna viwanda vimeshajengwa maeneo hayo. Na pia Kuna fence kuashiria watu wameshanunua kwa ajili ya uwekezaji.
2. Missungwi nayo imechanganya kwa nyumba za makazi tofauti na ilivyokuwa miaka kadhaa nyuma.
3. Nyashishi na usagara kama hauko makini huwezi kujua mpaka wake na nyumba zinaifuata ilipo fela. Hatari sana.
4. Nyegezi ni baba lao, nafikiri hakuna sehemu nyingine huko mbeleni itakuja kuamka kama kuizidi nyegezi. Kuna ujenzi wa majengo marefu ya ghorofa mengi sana na pamechangamka vibaya na uzuri Barabara zilizokuwa na vumbi miaka kadhaa zimeshapigwa Rami na baadhi zimewekwa mkeka wa mawe. Kamanga medics wanazidi kujitanua kwa kujenga jengo jingine refu. Pembeni mwa kituo Cha SOS Kuna kiota kinapanda, na viota vingine vingi. Nyegezi itakuwa babu kubwa na nahisi itakuwa CBD nyingine very soon kama halmashauri ya Jiji ikiamua kutawanya msongomano wa watu mjini kwa kuwasogeza huduma zingine hapo nyegezi. Hata hivyo Bado Kuna maeneo yanayofaa kwa uwekezaji mkubwa kama machinga complex, mall, low scale shopping centes, recreation parks etc.
USHAURI.
_Kuna foleni Barabara zote za mjini hivyo Kuna haja ya kuzipanua.
_afisa miji wasimamie kuzuia ujenzi holela kwa maeneo yanayoendelezwa.
_milima ya bugando na mabatini haiko poa sana raia wangerasimishwa ardhi na wapewe sharti la kuendeleza maeneo Yao.
NB. Kuna siku nitakuja na picha maana nilikuwa kwa basi tu nashangaa