Mwanza City: The Photo Gallery

Inawezekana kwa kujenga majengo kama ya kapri point na uwekezaji wa mahotel
Tatizo siasa zimejazwa kwenye akili ya watanzania ..juzi wawekezaji wamekuja kuulizia lakini tumesikia kelele za watu ,hadi jiji wameghairi ..yaana ujinga ni kikwazo cha maendeleo
Wakati ukienda china wao wanawaondoa wananchi wao kwenye maeneo mabaya na kuwajengea nyumba nzuri ...sisi imekuja ofa ya kutolewa mlimani ukapewe kiwanja kizuri maybe nyanshishi na ulipwe na fidia bado watu hawataki ..
Mimi nikija kuwa meya au mkurugenzi kweli wangetoka nisingekubali
 
Nyamagana hata mimi huwa siwaelewi, hata miradi yao wakijenga ni ya kiwango cha chini labda iwe ya serikali
 
Kaka Barabara si zinajengwa maeneo yenye watu?
 
Dah hii inasikitisha sana aiseee
Watu wanapewa stahiki zao bado wanalalamika
 
Huo mlima ni msitu umezungukwa na barabara, upande upi watahamishwa
Nilikuwa nasikia hizi nyumba zinazotazamana na na Shule Msingi Nyanza, na hizi Nyumba zinazotazamana na Nyakahoja Hostel. Kwa ule upande wa Sekou Toure kuna chuo na huu upande wa Nyakabungo kuna vinyumba nyumba nahisi ndio hao wataondolewa, ibakie mlima umezungukwa na barabara tu kwa pande zote.
 
Milima ina uoto wa asili
Ilitakiwa na milima mingine hususana pale town nayo ingekua kama huo wa balewa
Hapa ndio nasema nyamagana wamezubaa, utalii sio wanyama tu hii milima ya mza tukijipanga ni utalii tosha. Kuna milima ina mawe yanavutia balaa si vizuri watu waachwe wajenge.
Milima ambayo haija jengwa ilindwe na wawe wanaitembelea kila baada ya miezi 3 kuona kama kuna ujenzi kuliko kukaa ofsini tu.
Ipandwe miti na hata ile ambayo watu wanaishi wahimizwe kupanda miti.
Mlima kama huu wa balewa au kule bwiru inavutia sana sababu ya miti.
Pia itungwe sheria kuzuia watu kujenga milimani, ukijenga unavunjiwa, tubaki na hawa waliokwisha jenga tuone tunafanya nini.
 
HV Barabara ya nyerere haiko kwenye mpango wa upanuzi au ...au ndo mwisho njia 3 hadi Nyakato
 
Ndio shida ipo hapo, hata hawa ilemela tunaowasifia wamefeli kwa hili, yaani recreational Parks zetu tunawaza beach tu, kusingekuwa na ziwa ingekuwa je?
Kila eneo wazi tunawaza kupima viwanja watu wajenge basi kwisha.
Ilemela wangeweza tenga hata eneo kwa ajili ya CBD yao hakuna mtu kujenga unless ni ghorofa 10 kwenda juu, makampuni au mashirika au watu binafsi wakija kujenga maghorofa wanakuta viwanja vipo sio mpaka ulipe watu fidia.

Kuwe na recreational parks kila kata.
Kumiliki gari sasa hivi sio Big deal wanapopima viwanja wakumbuke kupima barabara ziwe kubwa na ziwe na njia za train, tram, brt nk baadae mji utakuwa mkubwa huu usafiri wa vipanya na mabasi hautafaa tutahitaji treni, wawaite trc wsone ni wapi panafaa kupita reli ili wslinde hayo maeneo.
Mfano inahitajika reli inayotoka nyegezi au buhongwa ije stendi ya Nyamhongolo mpaka airport.
Hii treni inaweza kuwa leta mjini kati watu wa pembezoni kwa kuunganisha na hii sgr inayojengwa sasa.
Maeneo mengine kama ni mazuri kwa kilimo si lazima vipimwe viwanja kisa mji unapanuka tutakosa sehemu za kulima baadae, watu wakajenge hata Magu huko tulinde baadhi ya maeneo kwa kilimo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…