Mwanza barabara kikwazo (Ilemela imekithiri)

Mahina-VicFish/Mwatex.

Ina maana Nile perch Fisheries Ltd nayo ilishakuwa VicFish siku hizi maana kitambo sijatia maguu huko.
 
Na hii barabara ya Mkuyuni-Butimba naona tayari lami,hivi hadi ule mchepuko wake wa kuelekea Chuo cha Uvuvi/TAFIRI uliwekwa lami?

Kuna ka-beach huko ilikuwa balaa sana enzi hizo.
 
Hivi hela za kujenga stand ya nyegezi na soko kuu pamba road ziliyeyukia wapi?naona mabati tu hakuna kinachoendelea,kule ilemela nyamhongoro ujenzi wa stand mpya umeshika kasi
 
Mahina-VicFish/Mwatex.

Ina maana Nile perch Fisheries Ltd nayo ilishakuwa VicFish siku hizi maana kitambo sijatia maguu huko.
Anamaanisha Nile perch Nyakato opposite na Mwatex sio VicFish ya Igogo relini,,
 
Nitamtetea sana Mama Angel Mabula wa Ilemela kajitahidi sana mpaka hapo nafikiri ni maeneo machache sana ambayo bado yanahitaji nguvu,,

Kwa upande wa Stan Mabula wa Nyamagana namshauri ajiandae tu kufungasha vilago arudi kwenye kazi yake ya ulinzi,,
 
Wakuu hata kama sio kwa pesa za ndani ni pesa za wafadhili Ilemela kwa mwaka ulioisha imejenga Km 12 za barabara kwa kiwango cha lami. Sabasaba-Buswelu, Mjimwema-Big bite, Nera-Kigoto/ Mwaloni.

"Hatua hii imetokana na usimamizi mzuri wa miradi ya TSCP ambapo wafadhili wamekuwa wakiridhika na kuendelea kutoa fedha kila mwaka. Mpango ujao ni kujenga kwa kiwango cha lami barabara za Kahama – Kabusungu – Kayenze, Mbogamboga – Nyamadoke – Nyamhongolo, Buswelu – Cocacola na Pasiansi – Lumala – Kiseke. Tayari maandiko ya miradi hiyo yanaendelea kufanyiwa kazi na mradi wa TSCP."

Sipo kusifia kila kitu, ila ni bora kidogo kuliko kukosa kabisa, Tujiandae kwa miradi ijayo barabara za Kahama – Kabusungu – Kayenze, Mbogamboga – Nyamadoke – Nyamhongolo, Buswelu – Cocacola na Pasiansi – Lumala – Kiseke.

http://www.ilemelamc.go.tz/storage/app/uploads/public/5d7/8b0/f04/5d78b0f046dc6745412498.pdf

ILEMELA ni yetu, tushirikiane kuijenga.
 
Kuna ile barabara ukitoka airport kuelekea Malaika beach kabla hujafika malaika penyewe unakutana na barabara ndefu kwelikweli ya rami hadi ina taa za usiku,huwa inaenda wapi ile?
mkuu ile huwa inaenda aitport wameiweka vizuri maalumu kwa viongozi wakubwa wanaotoka airtport kwenda malaika hotel kwa mtazamo wangu lakini!! ngoja wadau waje waseme

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikubaliani na wewe ila nadhani imejengwa kama mbadala wa ile inayoingia ndani ya uwanja kwa waendao Igombe kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege mpya unaoendelea,,
 
Sawa kabisa na ile ya Kijeleshi mahina kakebe na Mhandu
Yaani kwa barabara za jimbo la Nyamagana kwa ujumla ni utopolo mtupu,,
Na tutaonekana wajinga kupindukia endapo tutakubali hadaa za kuwarejesha viongozi waliopo kuanzia madiwani,, mbunge hata rais kabisa maana sio kwa uduanzi huu wanaotuonanao,,
 
Wakuu hata kama sio kwa pesa za ndani ni pesa za wafadhili Ilemela kwa mwaka ulioisha imejenga Km 12 za barabara kwa kiwango cha lami. Sabasaba-Buswelu, Mjimwema-Big bite, Nera-Kigoto/ Mwaloni.

"Hatua hii imetokana na usimamizi mzuri wa miradi ya TSCP ambapo wafadhili wamekuwa wakiridhika na kuendelea kutoa fedha kila mwaka. Mpango ujao ni kujenga kwa kiwango cha lami barabara za Kahama – Kabusungu – Kayenze, Mbogamboga – Nyamadoke – Nyamhongolo, Buswelu – Cocacola na Pasiansi – Lumala – Kiseke. Tayari maandiko ya miradi hiyo yanaendelea kufanyiwa kazi na mradi wa TSCP."

Sipo kusifia kila kitu, ila ni bora kidogo kuliko kukosa kabisa, Tujiandae kwa miradi ijayo barabara za Kahama – Kabusungu – Kayenze, Mbogamboga – Nyamadoke – Nyamhongolo, Buswelu – Cocacola na Pasiansi – Lumala – Kiseke.

http://www.ilemelamc.go.tz/storage/app/uploads/public/5d7/8b0/f04/5d78b0f046dc6745412498.pdf

ILEMELA ni yetu, tushirikiane kuijenga.
Kwa project hizi naiona kabisa Ilemela ikienda mawinguni Nyamagana ikibaki matopeni,, yaani
 
Hiyo barabara inaenda Cargo terminal mpya ya Mwanza International Airport
1586282372035.png
 
Kwa project hizi naiona kabisa Ilemela ikienda mawinguni Nyamagana ikibaki matopeni,, yaani
Mkuu Nyamagana wanaproject ya Barabara kubwa Igoma-Kishiri-Fela (2 way) na hiyo ya Kishiri - Kagera / Buhongwa naona mpango wa pesa na fidia bado haujaeleweka tu. Above all Mama Mabulla na Mkurugenzi wake John Wanga nitawakubali zaidi kama wataweza kuongoza hii round ya pili mradi TSCP kwa mafanikio.

1586283185061.png
 
Hii thread kama imeanzishwa na MTU mmoja ama watu fulani kwa lengo Fulani.

Nikiangalia kwa haraka haraka ID za mleta mada na wachangiaji watano wa mwanzo naona wote ni ama Member au Senior member
 
Malengo gani unayosema,, mpaka hapa hakuna kitu cha uongo au uchochezi kilichoongewa hapo,, kama huamini jaribu kufika maeneo husika ujionee kinachozungumzwa,,
 
Mkuu Nyamagana wanaproject ya Barabara kubwa Igoma-Kishiri-Fela (2 way) na hiyo ya Kishiri - Kagera / Buhongwa naona mpango wa pesa na fidia bado haujaeleweka tu. Above all Mama Mabulla na Mkurugenzi wake John Wanga nitawakubali zaidi kama wataweza kuongoza hii round ya pili mradi TSCP kwa mafanikio.

View attachment 1411965
Angel Mabula namkubali sana anajua anachokifanya tumpe muda zaidi,,
 
Back
Top Bottom