Mwanya, Uzuri wa asili

I like mwanya.ukiongezea na uchesi, tabasamu. Wee! Hata Mwamvita haoni ndani!
 
Akiwa na mwanya na dimples anakuwa mrembo zaidi!

...e bana wee! halafu umeshtukia wengi wenye mwanya lazima watakuwa na Dimples hata kwa mbali? Chunguza!

Haha jamani mbona mwanichekesha; sisi kwetu mwanya ni trade mark; bibi yangu mzaa mama alikuwa na mwanya mdogo san, alipozaliwa mama yangu mwanya ukaongezeka maradufu. Akatuzaa watoto 7, wavulana 5 na wasichana 2 wote mwanya kwa kwenda mbele wakatii baba hana mwanya. Mimi nikaolewa na mwanaume asiiye na mwanya, watoto wangu wote wawili kike/kiume mwanya wa nguvu.

Ninachotaka kusema sijaona huu mwanya umetufanyia nini. Hata kwenye usichana wangu sikuwahi kutongozwa mtu akasifia mwanya wangu walinipenda tu kwa sababu wananipenda ila mwanya haukuwa subject ya kupendwa.

Nafikiri kila mtu ana upeo wake kuhusu mwanya au hao waliousifia kwa ndani wanaweza kutusaidia.

...woowww, lazima kwenye familia yenu ni urembo kwa kwenda mbele. Big Up!

Olalaa..mimi sina mwanya Mbu!..ila wanapendeza wenye mianya hiyo!!
Haya tusio na mwanya ndo tunatengwa hivyo.
Kesho kutwa miguu nayo itasemewa...na mikono...na kiuno.Tusio navyo vyote tulie tu!:disapointed:

...Jamani BJ na Lizzy mbona mmeninyong'onyesha hivyo? Naamini kama hujajaaliwa mwanya, basi uwe umejaaliwa unywele wa singa-asilia kichwani! ...me luv it sooo much, ...if you have it, flaunt it!
 
Kuna watakaokuambia hii ni kero na wanafanya mazoezi kuondoa au hata operation kabisa. Hivyo ndio tujue kuna individual preferences jamani.
Bottomline - nobody can say kuna kipimo standard cha uzuri.Kila binadamu ni mzuri kwa jinsi alivyoumbwa na mola wake.Majadiliano ya kuponda maumbile ya watu iwe ni mitaani au kwingineko huweza kuwafanya watu wakakosa confidence.Kumbe basi inapotokea kwamba watu wanaongelea kwa namna chanya basi hupandisha kujiamini na hii imejidhihirisha hapa.Tunaona wengi wakifurahi kuona kumbe mwanya ni kitu kizuri!

Hongera Mbu kwa ku boost confidence za watu.Ingependeza ukaanzisha mada kama hizi ili tujadili more appreciatively, mathalani uzuri wa watu tipwa tipwa, weusi tii, wembamba sana, warefu, wafupi, wenye miguu myembamba nk.

...Oh Noo! ...WoS hapa I reserve my comments :tape:

Mbu wengine wana mwanya utadhani mapengo

..mnh, huo ndio tunaouita "uchochoro!," Lol!

Bwana me huwa napata shida sana, mwanya nnao ila nadhani unawafaa sana dada zetu lakini wanaume kuwa na mwanya hapana, kila nkicheka na mtu akanambia "una mwanya" jamani nafumba mdomo haraka sana hata sijui kwanini. Ila wanawake wenye mwana mnapendeza!

...flaunt it bana, jivunie urembo asilia huo!

Itabidi nikachonge meno pale Butiama kwa Mwalimu Nyerere kama ndo hivi ....Mbu

...usijali 1stLady, hiyo singa kichwani ni kivutio tosha na mwenyewe uiachiavyo mpaka mabegani, mnh!
You are blessed!

Okay, sasa mimi nataka kuona vidole vyako vya miguu na vya mikononi

...Lahaula! No Comment.
 
Mbu kama nywele za singa kwa lugha ya kwetu ni kipilipili nimefurahi sana na kesho napaka mafuta niziache wazi bila kufunga kilemba.
 
Watu wenye dimples nilokutana nao wengi wako so loving, sina maana ya opposite sex ila wote wananivutia sana. Dimples inafanya mtu aonekane innocent fulani, yaani kama mtoto vile. Tulivyokuwa wadogo tulikuwa tuna amini dimples zinatokana na mtoto kupendwa sana na wazazi na wakubwa wake. Na tuliamini wanapata last borns. Msidhani najisifia mwenyewe. Kwa ufupi sina mwanya wala dimples. Ila najiamini bado ninalipa!
 
...If you have it, flaunt it!...Kina dada na nyie mna maoni gani kwa wanaume wenye Mwanya?

eddie_murphy.jpg
maisha47022a53b2a02.jpg
bobbay.jpg
 
Back
Top Bottom