Kumbe wanawake wanapenda mahusiano yenye mikikimikiki

Kumbe wanawake wanapenda mahusiano yenye mikikimikiki

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
3,577
Reaction score
5,663
Baada ya zaidi ya miaka kama 14 nikitoa huduma inayohusiana sana na wanawake — kuwahudumia katika mazingira mbalimbali ya kijamii na kiafya — nimekuja kugundua jambo moja ambalo haliniingii vizuri akilini, lakini kila siku ushahidi wake unazidi kujionyesha: WANAWAKE WENGI HAWAPENDI MAHUSIANO YENYE UTULIVU. Ndio, nasema hivi kwa sababu kwa macho yangu mwenyewe, masikio yangu binafsi, na ushuhuda kutoka kwa mamia ya wanawake niliowahudumia kwa miaka yote hiyo, nimeona na kusikia vilio vya ajabu ajabu.


Wanawake wengi — hasa walio kwenye umri wa miaka 30 na kuendelea — wamewahi kuwa kwenye mahusiano mazuri, yenye amani na utulivu, lakini kwa namna fulani wanayaacha au wanayasababisha yavunjike. Ukiwauliza kwa nini, hakuna sababu ya msingi wanayoweza kutoa. Mwingine atasema “nilimchoka”, mwingine “hakuni-excite”, mwingine “yule alikuwa mpole sana”, au “sijui tu... sikuwa na furaha.” Lakini huwezi kupata majibu ya msingi au yenye mantiki ya kweli. Unagundua kwamba wamejizoesha mahusiano yenye mikikimikiki — ugomvi, drama, kulia kila wiki, kuchunguzana simu, kulazwa na presha ya mapenzi.


Kuna wanawake niliowahi kukutana nao, ambao ni warembo, wenye kazi nzuri au biashara, wenye malengo maishani, lakini mpaka sasa wana miaka zaidi ya 10 kwenye safari ya kutafuta mwenza wa kudumu. Wengi wana watoto, lakini hawako kwenye ndoa, na bado wanaendelea kulia, “wanaume hawaeleweki” au “sijampata yule wa kunistahili.” Lakini ukiwa karibu nao, unagundua kwamba mara nyingi wao wenyewe ndio chanzo cha machungu yao.


Inauma kusema, lakini ni kweli: baadhi ya wanawake hawataki mahusiano yenye utulivu kwa sababu hawajazoea. Wamezoea giza kiasi kwamba mwanga unawaumiza macho. Wamezoea vurugu kiasi kwamba amani inawapa wasiwasi. Wamezoea kusumbuliwa kiasi kwamba wakipewa mapenzi ya kweli wanahisi hawastahili au wanadhani kuna kitu kinajificha.

Mwanamke ni kiumbe kisichoeleweka......
 
Kuna sehemu nilikuwa napanga zamani DAR niliona jamaa mmoja gentleman ambaye nilikuwa namuheshimu Sana .

Ila siku moja nilimshuhudia anapigwa vibao na mkewe .

Nilichojifunza usije ukaoa mwanamke kwa kusema utambadilisha hiyo haipo MTU anabidi awe amenyooka ndo umuoe na sio unaoa ili umbadilishe

"Ukiokota tunda jalalani usilalamike kuwa limeoza"
 
Sio kaukweli bali ni ukweli mkubwa. Wengi wao wanapenda sana drama. Ndio maana watu tulionyooka tunapata shida kuishi nao
Wanaongozwa na hisia sasa ukimpa hisia nzuri ujue kumpa na hisia mbaya pia ili mzani wa hisia ubalansi. Ukijua kumpa amani na furaha pia ujue kumpa hofu na ugomvi ili awe stable ki hisia. Ni kama Mmea hauwezi kukua mchana tu unahitaji na usiku ili ukue vema (mwanga & giza) kikikosekana kimojawapo mmea hufa na penzi ni hivyo hivyo
 
Wanaongozwa na hisia sasa ukimpa hisia nzuri ujue kumpa na hisia mbaya pia ili mzani wa hisia ubalansi. Ukijua kumpa amani na furaha pia ujue kumpa hofu na ugomvi ili awe stable ki hisia. Ni kama Mmea hauwezi kukua mchana tu unahitaji na usiku ili ukue vema (mwanga & giza) kikikosekana kimojawapo mmea hufa na penzi ni hivyo hivyo
Hii nakubaliana nayo inabidi unamfurahisha muda huu dakika mbili mbele unampiga tukio
 
Imagine mtu hujaonyesha dalili zozote za kuchepuka lakini analazimisha akague simu. Unampa uhuru akague, anakagua na hakuti kitu chochote kibaya. Kisha anaamua kuingia mpaka kwenye deleted message kukusaka.

Unajiuliza huyu ndugu anatafuta nini kama sio vurugu
 
Hii jamiiforums ni sehem ya wanaume kuja kulia Lia et wanawake wanawatesa kimapenzi ubinafsi umewajaa utadhan wao ni wakamilifu kumbe..... Mwanamke ivi mwanamke vile aloooh wengine hatuwez expose mambo ya mahusiano humu ila wanaume ni viumbe vya ovyo kutokea kuumbwa
 
Back
Top Bottom