Mwandosya tuliambiwa asiye na Wizara maalum, Mkuchika kazi maalum. Kazi zipi hizo?

Serikali ina mipango mingi.....

Haijiendei tu kama kilabu cha MBEGE....

#KaziIendelee
 
Hata Mwandosya wakati anaumwa alipewa Waziri asiye na Wizara Maalum ili aendelee kupatiwa matibabu na Serikali.
 
Wanasiasa wanajitengenezea ulaji tu, Kama mambo ndiyo hayo ya kutafuna hela za walala Hoi wa nchi hii, bora tusiwe tunapiga kura.Wachache Sana wanafaid nchi hii.
 
Nafikiri lengo ni kumpa nafasi ya kuingia katika cabinet kama mshauri wa RAIS.Kutompaa Portfolio kunampa access ya kufanya kazi na RAIS moja kwa moja.Lakini zaidi ya yote nafikir hio wizara ya bila wizara huwa wanapewa Seniors katika Cabinet ambao RAIS anaona bado anaweza kuwatumia katika utumishi hasa katika ushauri na utekelezaji.Kwa kupewa uwaziri inamaana anakuwa na uwezo wa kuingia katika Baraza la mawaziri na kunyimwa wizara inaama anakuwa anawajibika kwa RAIS na anakuwa hana majukumu mengine zaidi ya kuwepo kwa ajili ya RAIS.

Fahamu kwamba Ni mawaziri tu wanaoingia kwenye CABINET
 
Mkuchika ni mzoefu kweli kweli kwenye how to run the government machinery. Baraza la kwanza la Magufuli, Mkuchika hakuwepo.... baadae naona Magufuli mwenyewe aliona pengo lake akamrudisha.
 
Watu husahau WIZARA MAALUM kwamba KINGUNGE NGOMBALE alikuwa yumo.
Enzi za Kingunge ali deal zaidi na usalama wa taifa. Ndio maana Kama mtakumbuka enzi zile kumjua mtu wa usalama ilikua Ni issue. Sio siku hizi mtu anashindwa kulipa bili ya pombe anajitangaza Yuko usalama au takukuru.
Yuko jamaa yangu wa karibu nilikuja kumjua kwamba Yuko usalama baada ya jamaa kustaafu.
 
Nimeamini ule usemi wa kuwa hata saa mbovu kuna muda inasema ukweli, kongole sana mkuu
 
Ngoja waje wenyewe
 
Meanwhile PM Majaliwa kasimamisha kazi watu pale Wizara ya fedha kisa wamejilipa pesa kwa maelezo ya "Malipo ya kazi maalum" pasipo kuitaja kazi husika.

Haya mambo ya kazi maalum au "asiye na wizara maalum" huwezi kuyakuta kwa wenye akili timamu.

#Shithole country.
 
Nyerere ndio anapenda sana kuwa na position kama hizo.
 
Wanasema Kuna vizee bado ni asset Kwa taifa
Na Mkuchika ni mmoja wao. Ni TISS wa miaka mingi tangu jeshini mpaka sasa. Ashafanya missions kibao kwa mafanikio makubwa na anayajua mengi so hawawezi mtema. 2015 alipigwa chini kwa kura nyingi sana ila ndo akiyetangazwa mshindi.
 
JK alitambua wazi alihitaji akili za mtu kama Mwandosya kuendesha nchi wakati anaitwa dhaifu nk. Kama uligundua, mwishoni JK alionekana kuwa na busara sana za uongozi - nyuma ya hilo ilikuwa ni akili za Prof. Mwandosya.
Majibu ya maswali yako yako hapa
 
Mkuu umemaliza kila kitu na kama kuna mtu bado atakuwa na swali basi akili yake itakuwa na mushkeli
 
Tuliza wenge mteuaji anazijua hizo kazi maalumu....
 
Nimekuelewa sanaa Chief!
 
1. Kuroga
2. Kufitinisha
3. Kufundisha Chipukizi Umbea
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…