Hiyo ni sheria ya chama chako ila sheria ya chama cha mapinduzi ni wadhamini 30 kila mkoa..
unaropoka utadhani unatoka MSALANI
😛eep:
MASHARTI KWA KILA NAFASI YA KUOMBEA UONGOZI
1. URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
•
Kila mgombea ni lazima apate wadhamini 450 katika mikoa 15 walau 3 kati ya hiyo iwe ya Zanzibar.• Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa Taifa hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais.
• Mwanachama haruhusiwi kumdhamini mgombea Urais zaidi ya mmoja.
• Fomu ya udhamini ya wanachama ithibitishwe na Katibu wa CCM wa Wilaya kwa kupigwa muhuri wa Chama wa Wilaya husika.
• Wanachama watakao mdhamini mgombea, uanachama wao uthibitishwe na Katibu wa CCM Wilaya husika na kupiga muhuri wa Chama.
2. URAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR
• Kila mgombea ni lazima apate wadhamini 250 katika mikoa 3 kati ya hiyo angalau Mkoa mmoja toka Unguja na mmoja kutoka Pemba.
• Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa Taifa hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais.
• Mwanachama haruhusiwi kumdhamini mgombea Urais zaidi ya mmoja.
• Fomu ya udhamini ya wanachama ithibitishwe na Katibu wa CCM Wilaya kwa kupigwa muhuri wa Chama wa Wilaya husika.
• Wanachama watakao mdhamini mgombea, uanachama wao uthibitishwe na Katibu wa CCM Wilaya husika na kupiga muhuri wa Chama.