Mwandosya: Makinda anafaa kuwa rais 2015!

Mwandosya: Makinda anafaa kuwa rais 2015!

hivi, Mbowe, Mnyika, Rose Kamili, Halima Mdee, Sugu, Msigwa, Ndesamburo na wengine ndani ya CHADEMA, wana uwezo wa kumzidi Mama Makinda? acheni dharau jamani

Uliowataja hata moja hajasikika akiutamani urais, Mbowe toka ashindwe vibaya kipindi kile cha nyuma hajasikika tena hadharani akitamani hio kitu! Lizaboni, kichwa cha kuku hakistahimili kilemba! Tuwe wa-wazi, bi Mkora hio kitu ni sawa na ile methali maarufu ya kiswahili isemayo maji ya kifuu, ni bahari ya chungu!
 
Ewiiiiiii! Tumekwishaaaaaa! Anashindwa kuongoza bunge. Matusi bungeni kama vijiweni leo apewe nchi? Ccm mpitisheni wapinzani wapate njia ya kuingia ikulu! Asante mwandosya
 
hakuna haja ya kwenda mbali simply ni kwamba huyu mama hafai maana kama pale mjengoni pamemshinda urais ndo atauwezaje. Hebu kaeni chini fikirieni mtu anayetufaa maana mkiweka kituko kwenye hiyo nafasi na mambo yote yatakuwa kituko.
 
makinda ameshindwa familia licha ya kushindwa pia kuwaongoza watu mia tatu (300) hapo, atawezaje kuiongoza tanzania yenye watu 44million.
 
makinda ameshindwa familia licha ya kushindwa pia kuwaongoza watu mia tatu (300) hapo, atawezaje kuiongoza tanzania yenye watu 44million....
 
Kikwete kaufanya urais uwe kama nyanya
Kutokana na uongozi wa Jk watu wanaona urais ni rahisi sana hivyo kila mmoja anaona anauweza kama JK kauweza. Yaani hata walioshindwa umonitor darasani wanautaka urais. Ingekuwa urais ni kama alivyo ongoza Nyerere kwa weledi mkubwa na kwa maadili ya hali ya juu sana, hawa tunaowasikia wakiutaka wangejificha mbali. Wakati ule watu walikuwa wanatafutwa na kuombwa kugombea kwasababu uongozi ilikuwa ni utumishi. Sasa hivi wanautaka kwa kila mbinu hata ikibidi kumwaga damu kwasababu sasa hivi uongozi ni utajiri na kujilimbikizia mbali na kutumikiwa na wananchi. Wakati wa Nyerere kiongozi alitegemewa awe na busara, akili, hekima na maono. sasa hivi hakuta ukiwa kichwani sifuri unakuwa rais ili mradi una pesa za kuhonga na kuanzisha mitandao.
 
hakuna haja ya kwenda mbali simply ni kwamba huyu mama hafai maana kama pale mjengoni pamemshinda urais ndo atauwezaje. Hebu kaeni chini fikirieni mtu anayetufaa maana mkiweka kituko kwenye hiyo nafasi na mambo yote yatakuwa kituko.

Kama ni huyo mama hiyo nafasi ni bora ibaki wazi mpaka atakapopatikana anayefaa.Mbona hata sasa nchi iko autopilot na inakwenda tu.
 
alikuwa amekosea ukweli ni kwamba makinda anasifa na kustahili kuwa bibi bomba
 
Nadhani sasa Prof Mwandosya inabidi arudi India akamalizie matibabu.
 
Back
Top Bottom