Mwandosya: Makinda anafaa kuwa rais 2015!

Mwandosya: Makinda anafaa kuwa rais 2015!

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2010
Posts
8,397
Reaction score
7,979
Ninasikiliza vichwa vya habari magazeti ya LEO eti Mzee Mwandosya amempendekeza Anna Makinda kwa urais 2015.

----------------------
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, asiyekuwa na wizara maalumu, Profesa Mark Mwandosya, amempigia debe Spika wa Bunge, Anne Makinda, akisema kuwa anafaa kuwa rais kutokana na sifa zake.

Profesa Mwandosya alimwaga sifa hizo bungeni jana, wakati akiunga mkono Azimio la Bunge la kumpongeza Makinda, kutokana na kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA).

Profesa Mwandosya, ambaye miaka ya nyuma alijitosa katika kinyang'anyiro cha urais, alisema Spika Makinda ana sifa zaidi ya kumi ambazo zinamtosheleza kuwa rais na kwamba ni watu wachache wenye sifa kama hizo.

Akitaja sifa hizo, Profesa Mwandosya alisema Makinda ni mtu anayejiamini, mtenda haki, mchapakazi, mzoefu, msikivu, mbunifu, mwelewa, mvumilivu, mnyenyekevu na pia ni mtu mwenye msimamo.

Alisema kutokana na sifa hizo, Makinda anafaa kuwa kiongozi wa ngazi ya juu katika nchi, huku akimtazama kuwa ni mwanamke tishio katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

"Kwa namna ninavyomfahamu Spika Makinda ni tishio kwa uchaguzi wa rais mwaka 2015, kutokana na jinsi alivyokuwa na uwezo na mambo aliyowahi kulifanyia taifa hili.

"Kuchaguliwa kwake kuwa rais wa CPA ni hatua muhimu na nzuri kwa wanawake wengi kuongezeka katika Bunge la mwaka 2015 kwa kufikia asilimia 55, kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka," alisema Profesa Mwandosya.

Profesa Mwandosya, ambaye amekuwa serikalini kwa muda mrefu, mwaka 2005 alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza kuwania urais.Hata hivyo, kutokana na mchujo, Mwandosya alifanikiwa kuingia katika tatu bora. Wengine walikuwa ni Dk. Salim Ahmed Salim, Rais Jakaya Kikwete.

Naye Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah (CCM), alimwaga sifa kwa kiongozi huyo wa Bunge na kusema kuwa ni mwanamke shupavu atakayekuwa tishio katika uchaguzi mkuu ujao.

Akichangia mjadala huo wa kumpongeza Spika, Anna Abdallah, alisema Makinda ni mwanamke mwenye uwezo wa kuongoza nafasi yoyote ya juu, ikiwemo urais wa nchi.

Alisema kutokana na uzoefu wake katika uongozi hapa nchini, ameweza kuaminika hata nje ya nchi, jambo ambalo limemfanya kuchaguliwa kuwa Rais wa CPA.

"Kwa muda mrefu nchi yetu imekuwa ikihubiri juu ya mwanamke kupewa fursa na hasa kama ana uwezo, sasa wenzetu CPA wameweza kuliona hili wamemchagua," alisema.

Mbunge huyo aliwataka wanawake kutojali maneno ya pembeni na sasa ni lazima jamii ikubali kumuamini mwanamke kwa kumpa nafasi ya juu ya uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Awali akisoma Azimio hilo la Bunge, Mwenyekiti wa CPA-Tanzania, Mussa Azzan Zungu, alisema Spika Makinda alishika wadhifa huo baada ya kufanyika kwa mkutano wa 44 wa chama hicho.

Zungu, ambaye ni Mbunge wa Ilala, alisema katika mkutano huo Bunge la Tanzania liliwakilishwa na wabunge wanane, akiwemo Spika Makinda na baadaye ulifanyika uchaguzi huo.

Chanzo:Mtanzania

My Take:
Uraisi sasa imekuwa ni JOKE na inaonekana kila mtu anaweza kuwa rais wa Tanzania. Inaelekea nchi hii haina hata JOB DESCRIPTION YA URAIS
 
Makinda ni mwanamke wa shoka, we utabaki na wivu wako hapo
 
Uwezo wa makinda kiuongozi ni mkubwa sana. Unaweza kulinganishwa viongozi kumi wa upinzani wakiunganishwa kwa pamoja, ie 1 makinda = 10 opposition men leaders tena wa huku bara.
 
Kama Rais mwanamke basi atakuwa Prof Tibaijuka!......!au ikishindikana basi Bi Salma!hahaha maana atapata ushauri wa kuweka auto pilot tu!
 
Ninasikiliza vichwa vya habari magazeti ya LEO eti Mzee Mwandosya amempendekeza Anna Makinda kwa urais 2015.

My Take:
Uraisi sasa imekuwa ni JOKE na inaonekana kila mtu anaweza kuwa rais wa Tanzania. Inaelekea nchi hii haina hata JOB DESCRIPTION YA URAIS

ni haki kwa mtanzania yeyote kufikiria kuwatumikia watz kwa nafasi ya urais. Wananchi ndio watapima uwezo wake
 
Uwezo wa makinda kiuongozi ni mkubwa sana. Unaweza kulinganishwa viongozi kumi wa upinzani wakiunganishwa kwa pamoja, ie 1 makinda = 10 opposition men leaders tena wa huku bara.

sina hakika na hili mkuu!
 
ni haki kwa mtanzania yeyote kufikiria kuwatumikia watz kwa nafasi ya urais. Wananchi ndio watapima uwezo wake

Na hao wnanchi ndio sisi hapa baadhi endelea kupima upepo hapa ila kaa nyuma ya strong pivot maana waeza chukuliwa na.upepo unaoupima
 
ifweero...
Kweli tunatofautiana kufikiri, nathibitisha toka kwako! LMAO!
 
Last edited by a moderator:
Lazima ampigie chapuo mnyanda za juu mwenzake kama wilson mukama alivyosema
 
Uwezo wa makinda kiuongozi ni mkubwa sana. Unaweza kulinganishwa viongozi kumi wa upinzani wakiunganishwa kwa pamoja, ie 1 makinda = 10 opposition men leaders tena wa huku bara.

You mean:
MAKINDA = Lisu, Lema, Mnyika, Nassari, Mdee, Safari, Arfi, Chiku, Leticia, Kamili.
Hapo kweli sidanganyiki kamwe.!!!
 
You mean:
MAKINDA = Lisu, Lema, Mnyika, Nassari, Mdee, Safari, Arfi, Chiku, Leticia, Kamili.
Hapo kweli sidanganyiki kamwe.!!!

Una mpango wa kuanzisha thread ndani ya thread..!?
 
Uwezo wa makinda kiuongozi ni mkubwa sana. Unaweza kulinganishwa viongozi kumi wa upinzani wakiunganishwa kwa pamoja, ie 1 makinda = 10 opposition men leaders tena wa huku bara.
Mkuu jenga hoja kwa nini anafaa, sio kulinganisha bila vigezo vya msingi.
 
Uwezo wa makinda kiuongozi ni mkubwa sana. Unaweza kulinganishwa viongozi kumi wa upinzani wakiunganishwa kwa pamoja, ie 1 makinda = 10 opposition men leaders tena wa huku bara.

You're so amazing human being..!! Maoni yako unayotoa kila wakati yabalindwa kwa mujibu wa Ibara ya 18(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa;

18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati..."

Kwahiyo, hata kama ni mawazo ya hovyo au uwongo au upotoshaji au hayana uchambuzi bora, tutakubali kusoma lkn hatuwezi kuamini kuwa ndio ukweli wa jambo unalosema.
 
Back
Top Bottom