Elections 2010 Mwandosya ahujumiwa na wana CCM wenzake?

Pamoja na malengo mazuri na ushupavu anaokuwa nao Kubenea, lakini ukweli unabakia kuwa ana agenda ya siri dhidi ya Lowasa. Sioni ni kwa vipi Lowasa alistahili kubeba kichwa cha habari hii. Mi nadhani mwanahalisi wanaweza kupotosha umma kwa kuonyesha kuwa ndani ya nchi hi ufisadi=Lowasa. Wapo wengi mafisadi ambao bado wapo na nyadhifa zao ambao gazeti linaweza kuwavalia njuga, na si Lowasa tu ambaye by the way hayupo tena madarakani...
Lowassa ndiye Don Corleone wa siasa Bongo. Yeye na Rostum.
 
Mwandosya ni waziri pekee nchini (mwenye Uraia wa nchi mbili) aliyeletwa na Mkapa kinyume cha mipango ya wanaCCM - Rukwa, Mbeya..Na yawezekana kabisa uwezo wake ktk Uongozi unatishia mfumo na utaratibu mzima wa Ulaji Mbeya..Na kulingana na navyowafahamu mila na desturi za Wadanganyika wooote, chuki binafsi (inda) zinaweza kuwa sababu kubwa ya matukio yoote haya kwani mgeni yeyote unapoingia mjini toka nje, usipokwenda kuwatembelea (salimia) nyumbani kwa mtu/watu wanaokufahamu basi wewe unajenga chuki na Unalinga.
Mkandara........

Hebu tuweke sawa hapa....Mwandosya ana uraia wa nchi mbili!!!!!!!!!!!!!!!???????,ana uraia wa nchi ipi nyingine?,aliletwa na Mkapa kutoka wapi?.....Mwandosya alikuwa Mwalimu muda mrefu tu kabla hajawa Katibu mkuu wa Wizara ya Maji,Nishati na Madini......Baadae alirudi kufundisha kisha akagombea ubunge mwaka 2000 na kuteuliwa kuwa Waziri.........Sasa huyo Mkapa alimleta kutoka wapi???????????????????????

Tuweke sawa hapa mkuu..........Unatuchanganya kama sio kutupotosha
 
Asante Mkuu.
Hili bifu kati ya Kubenea na Lowassa (na swahiba mwenza Rostam) lina sababu yake, na labda nidokeze tu ninachokisikia. Unakumbuka kesi ya tindikali? Imefikia wapi?

Imekwama kwa sababu washukiwa wakubwa behind kumwagiwa Kubenea tindikali ni wawili hao, EL na RA. Imekwama kwa sababu mtuhumiwa mmoja muhimu haonekani – mtuhumiwa ambaye ndiye mhusika mkuu wa shambulio hilo la tindikali dhidi ya Kubenea.

Inadaiwa kasafirishwa nje baada ya tukio kama ilivyogundua timu ya Tibaigana iliyopewa jukumu la kupeleleza kesi tukio hilo. Mafweza mengi yalitembea kwa polisi kufanikisha hilo.

Kwa uchache kabisa habari ndo hiyo. Fikiria mtu anataka kukupofua macho unamfanyaje? But don’t quote me! Mwenye habari zaidi azitoe.

Aaah, umenifumbua macho. Thanks! Kwa matendo tu, inadhihirisha kwamba story hii ina ukweli mkubwa.
 
acheni ukweli usemwe wazi!!!!!!!!!!
Nani aisye jua namna Prof anavyowindwa usiku na mchana ili aangamizwe kisiasa????????????????
Ukweli upo pale pale tu ndugu zangu!!!!!!!!!!
 
Kwa haraka haraka naona Mkandara kachanganya watu.

Kubenea pamoja na kuombwa, bado anaandika kuwa George Mwakalinga ni MWANAFUNZI.

Mtanzania, hebu mtumie ID yako ya HUAWEI huyu Kubenea.
Labda ndiyo hapo milele atafahamu kuwa wewe SI MWANAFUNZI TENA.
Hilo lilishasemwa hapa sana tu. Sasa kama hata hilo bado Kubenea halioni, habari yake nzima inaleta utata.

Ila tu si kuwa kila anachoandika ni UONGO. Si hapa JF mnasema "Hata saa mbovu pana wakati husema ukweli...?"
 
Kwa haraka haraka naona Mkandara kachanganya watu.

Kubenea pamoja na kuombwa, bado anaandika kuwa George Mwakalinga ni MWANAFUNZI.

Mtanzania, hebu mtumie ID yako ya HUAWEI huyu Kubenea.
Labda ndiyo hapo milele atafahamu kuwa wewe SI MWANAFUNZI TENA.
Hilo lilishasemwa hapa sana tu. Sasa kama hata hilo bado Kubenea halioni, habari yake nzima inaleta utata.

Ila tu si kuwa kila anachoandika ni UONGO. Si hapa JF mnasema "Hata saa mbovu pana wakati husema ukweli...?"

Mkuu Sikonge,

Mimi Kubenea nilishaamua kuachana naye pale alipokataa offer yangu ya kusahihisha habari yake juu yangu.

Kuna watu hata walimpigia simu na akasema atapita kusoma JF lakini hakutoa comments zake tena. Mimi niliajiriwa na Lucent Technologies tarehe 01/09/1997 na mpaka leo sijawahi kutokuwa kazini hata siku moja. Sasa hayo ya uanafunzi mpaka leo yanatoka wapi? Miaka 13 baada ya kumaliza shule bado unaitwa mwanafunzi tu?

Wacha tuendelee na mengine maana haya ya waandishi wa habari wa TZ yatatupotezea muda bure.
 
Kwa haraka haraka naona Mkandara kachanganya watu.

Kubenea pamoja na kuombwa, bado anaandika kuwa George Mwakalinga ni MWANAFUNZI.

Mtanzania, hebu mtumie ID yako ya HUAWEI huyu Kubenea.
Labda ndiyo hapo milele atafahamu kuwa wewe SI MWANAFUNZI TENA.
Hilo lilishasemwa hapa sana tu. Sasa kama hata hilo bado Kubenea halioni, habari yake nzima inaleta utata.

Ila tu si kuwa kila anachoandika ni UONGO. Si hapa JF mnasema "Hata saa mbovu pana wakati husema ukweli...?"

Nkwingwa........Tunakuhitaji Sikonge bana..........Said keshajichokea
 
Asante sana Nkwingwa. Ila mie labda mwaka 2015 kwani kwa sasa mambo mengi sana kichwani. Nitakuwa tayari kushirikiana na mtu yeyote atakayekuwa na malengo mazuri kwa Sikonge. Ngoja kwanza nimsukume kijana wangu Mwakalinga. Akishaingia ulingoni basi mashambulizi tunahamishia Sikonge. Ila ntaanza kujiandaa mapema sana sana ili isije fika siku ya uchaguzi, ndiyo mzee unashuka vijiji vya watu ukiwa na SUTI ?!??!?! Mhhh, nasikia kuna jamaa alishinda kwa kuvaa sijui kata mbunga na kula mihogo mibichi. Kahhh, yaani sisi Wanyamwezi tunanunuliwa kwa vitu vya ajabu sana.

Nkwingwa........Tunakuhitaji Sikonge bana..........Said keshajichokea
 
Ikiwa ni kweli Mwandosya ni raia wa nchi mbili kama Mkandara alivyosema, anaruhusiwa na sheria kugombea uraisi na kuwa waziri wakati nchi yetu haina uraia wa iana hiyo? Na nchi ipi nyingine ambayo Mwandosya ni raia wake? Aliungwa mkono na watu wengi alipogombea uraisi 2005. Wangejua ukweli huo, kama ni kweli kwamba ni raia wa nchi mbili, wengi wao wasingemuunga mkono.
 
Anyway sijui kuhusu sakata hili undani wake naogopa kukomenti maana ....ila huyu mwakipesile huyu duh ni kama huwa simuelewi elewi.....
ila tu namuona amekaa kama silaha zaidi katika kiti chake kuliko kazi ya kuwahudumia wananchi wa mbeya...na hahamishwi wala haondolewi hata baada ya wananchi wa mbeya kumuomba JK aondoke nae siku ile...ana jeuri fulani huyu...yes anayo
mix with yours
 
Ikiwa ni kweli Mwandosya ni raia wa nchi mbili kama Mkandara alivyosema, anaruhusiwa na sheria kugombea uraisi na kuwa waziri wakati nchi yetu haina uraia wa iana hiyo? Na nchi ipi nyingine ambayo Mwandosya ni raia wake? Aliungwa mkono na watu wengi alipogombea uraisi 2005. Wangejua ukweli huo, kama ni kweli kwamba ni raia wa nchi mbili, wengi wao wasingemuunga mkono.

Usiwe na wasiwasi bro! Prof. Mwandosya hana uraia wa nchi mbili. Nashangaa mheshimiwa Mkandara ametoa wapi hayo maneno?

Muda pekee ambao prof. Mwandosya amekaa nje ya nchi ni wakati alipokuwa anasoma UK kuanzia 1971 mpaka 1977 aliposoma bachelor mpaka Ph.D. Hiyo miaka ilikuwa sio rahisi kwa mgeni kupata uraia wa UK tena mgeni mwenyewe akiwa mwanafunzi.

Labda Mkandara amewahi sikia kwamba Prof ana mke kutoka Uganda na ndio kachanganya na uraia wa nchi mbili. Nina uhakikia wa asilimia 99 kwamba prof. hana uraia wa nchi mbili.

Ninapojua Mkandara kachanganya, ni pale aliposema prof. aliletwa na Mkapa, hapana prof. alikuwepo UDSM akifundisha baada ya kuamua yeye mwenyewe kuacha kazi ya katibu mkuu wa wizara na kurudi kushika chaki UDSM.
 
Nina wasiwasi sana na ukweli wa habari hii. Kubenea anatumiwa na kundi la Mengi na wafuasi wake akiwemo Dr. Mwakyembe.................

Kwa muda mrefu Mwakyembe anafanya juhudi kubwa kutumia Nipashe na Mwanahalisi kuwagonganisha kati ya Mwakipesile na Prof. Mwandosya.....................

Hawa watu wawili sio marafiki lakini pia sio maadui kama gazeti linavyotaka kuonyesha. Ila Mwakipesile na Mwakyembe ni maadui wakubwa.

Unadhihirisha wazi kuwa huifahamu Rungwe, Huifahamu Tukuyu, Huifahamu Kyela na Huzifahamu siasa za maeneo hayo. Mbaya zaidi huzifahamu hulka binafsi za watu hao watatu.
 
Prof. Mwandosya alichukua uamuzi wa maana wa kutokumshambulia Mwakipesile waziwazi pamoja na kwamba alikuwa anajua kwamba aliachwa pale Mbeya ili amwangalie prof. Mwandosya.

Sasa kama unafahamu hilo unamshangaa vp Kubenea?

. Mwakyembe hakufurahia hilo, yeye alitaka kuendelee kuwa na mikiki mikiki kati ya hao viongozi ili ile vita yake na Mwakipesile nayo ipambe moto.
Kwa taarifa yako, nyuma ya Dk Mwakyembe, yupo Mwandosya na Hilda Ngoye sasa kama Mwakyembe hakufyrahia elewa na Mwandosya= Ngoye nao hawafurahii.

mama yake prof. Mwandosya, mkuu wa mkoa alienda na prof alimpokea bila vinyongo vyovyote.
Alivyofariki mama wa Mwakipesile, prof. Mwandosya naye alienda kumwona.
Mkuu, Siasa ni Unafiki. Bifu za Mwandosya zimekaa kisayansi sio kama za kina EL et al (Mwakipesile akiwamo) Na ndio maana Mwakyusa anatambua kuwa Mwandosya anamfitini asirudi bungeni ili nafasi yake aichukue Hilda Ngoye lakini huwezi kuwakuta Mwakyusa na Mwandosya wana bifu za waziwazi. Wanapanda gari moja, wanakula pamoja na wanatembeleana.

na Mwakyembe ni maadui wakubwa.
Mwakyembe na Mwandosya ni MAADUI wakubwa wa Mtandao wa JK ambao Mwakipesile ni mmoja wao. Uadui wao hautaisha. Uliza kilichotokea wakati wa uchaguzi wa wajumbe ya NEC ya CCM kisha pima intensity ya mgogoro wao.

za chuki na visasi ndizo hata zimesababisha kupungua sana kwa uhusiano kati ya Prof. Mwandosya na Dr. Mwakyembe. Inasemekana prof hapendi hizo siasa za jino kwa jino na anaanza kujiweka pembeni ili asionekane wazi kwamba yuko upande mmoja.
Uongo uliokubuhu, fanya utafiti kisha futa kauli yako.

alivyoenda Mbeya katika sehemu alizotembelea na kufungua miradi ya maana ilikuwa jimbo la prof. Mwandosya. Sidhani kama itakuwa busara eti kumpeleka rais nyumbani kwa waziri? Ataenda nyumbani kwa prof kufanya nini?
Alienda kijijini kwa Mwandosya na hii ilitokana na ombi maalumu la Mwandosya kwa Bosi wake ambapo mara ya kwanza Mwakipesile aliipunch lakini mara ya pili alichemsha.

tujihadhari sana na hawa watu ambao wanataka mkoa uwake moto shauri ya visa vyao binafsi. Huyu Kubenea anatumika sana kuchapisha habari ambazo zinaandikwa na watu wengine na yeye faida kwake ni kuuza hilo gazeti lake.
Ni suala la muda tu, Mbeya moto ulishawaka siku nyingi, Kumbuka ugomvi uliokuwapo kati ya Mulla (Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya) na Mwandosya mwaka 2008.

Mimi ni mfuasi mkubwa wa prof. Mwandosya na naunga mkono strategy yake ya kukaa kimya na kufanya mambo kwa vitendo kule kwake. Hii inamjengea sifa mkoani na hata hao wanaotaka kumwondoa hawatafanikiwa.
Hayuko kimya kama unavyomfikiria, huyu bwana ni hatari. Anaendesha mapambano kisayansi na watu alionao wanaomsaidia vita sio aina ya MAKAMBA.

Kyela Rhoda wala haungwi mkono na mkuu wa majeshi. General Mwamunyange ameamua kuwa pembeni kabisa inapokuja siasa za Kyela maana anajua madhara yake. Huyo Mwakalinga naye anatajwa kuwa mwanafunzi, mbona wote tunajua hapa kwamba ni mfanyakazi tena wa siku nyingi sana? Makosa mengine yanaharibu habari kabisa.
Hapa kidoooooooooooogo umejaribu kuwa mkweli.

MZITTO
 
sasa kama mkuu wamkoa anahangaika kumaliza watu... hizo kazi za maendeleo anafanya saa ngapi???

halafu nadhani mwakipesile ndiye mkuu wa mkoa aliyekaa zaidi mkoa mmoja... naomba kusahihishwa wakuu... sometimes staying in one place [tena kwa huyu ambaye ni kwao] may be adversarial
 
Sikonge,
Mkuu wangu hata mimi nina bifu la Mwandosya - maanake imeshakua kupakana tu hadi watu waondolewe ktk Ubunge....
 
Back
Top Bottom