Mwandosya ahujumiwa na wana CCM wenzake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandosya ahujumiwa na wana CCM wenzake?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Jun 19, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Lowassa amhujumu Mwandosya

  Na Saed Kubenea

  NYARAKA za siri zinazoonyesha mpango wa kumtokomeza kisiasa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya zimevuja.

  MwanaHALISI limepata nyaraka hizo zinazomtaja mkuu wa mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa katika njama hizo.


  Katika andishi rasmi, Mwakipesile anasema kwamba anatuhumiwa kushirikiana na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na swahiba wake mkuu, Waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kumwangamiza Mwandosya kisiasa.


  Profesa Mwandosya ni mbunge wa Rungwe Mashariki (CCM). Alikuwa miongoni mwa waliokuwa kwenye mchakato wa kugombea urais mwaka 2005.


  Mwingine anayetajwa katika njama hizo ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mbeya, Nawab Mulla. Katika orodha hiyo, yumo pia mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa taifa, Cornel Apson Mwang’onda.


  Kwa mujibu wa mawasiliano yaliyopo kati ya Profesa Mwandosya, Mwakipesile, Mwalimu wa Shule ya Msingi Lufilyo, Alisto Gideon Mwangungulu na Stephen Merali Mwakajumilo, wafadhili wakuu wa mkakati ni Rostam na swahiba wake Lowassa.


  Taarifa zinasema Profesa Mwandosya huenda akagombea urais mwaka 2015, mwaka ambao pia imetajwa kuwa Lowassa angependa kuingia kwenye kinyang’anyiro.


  Kuanguka kwa Profesa Mwandosya, taarifa zinaeleza, kunaweza kuwa ni kumsafishia njia Lowassa katika kuwania urais mwaka 2015.


  Mwaka 2005 Profesa Mwandosya alikuwa mmoja wa wanachama wa CCM waliotoa ushindani mkubwa kwa rais Jakaya Kikwete katika kinyang’anyiro cha kutafuta mgombea urais kupitia chama hicho.


  Tangu wakati huo, taarifa zinasema, kumekuwa na madai ya kutaka kumuangamiza kwa maelezo kuwa anaweza kutamani kugombea tena nafasi hiyo mwaka 2015.


  Aidha, taarifa zinasema Mwandosya amekuwa akikabiliwa na upinzani mkali kutoka ndani na nje ya chama, kutokana na kutokuwa mfuasi wa kundi maarufu la “wanamtadao,” lililomuingiza Kikwete madarakani.


  Mkakati huo wa siku nyingi umevuja mwezi mmoja uliopita, baada ya Mwalimu Mwangungulu “kuungama” kwa Mwandosya akiwa na viongozi wengine wa dini.


  Alisema aliitwa na Mwakipesile na kutakiwa kusaidia harakati za kumtokomeza Mwandosya.


  Kwa mujibu wa mawasiliano ya siri kati ya viongozi hao wawili, Mwakipesile, anatuhumu Mwandosya kuwa mtu anayejisikia na asiyethamini viongozi wake wa mkoa na kitaifa.


  Mwalimu Mwangungulu anasema katika ungamo lake kwamba Mwakipisile alimueleza, “…Mwalimu ngoja nikuambie yafuatayo: Mbunge wenu ana kiburi, ana dharau. Sijui ni kutokana na elimu aliyonayo?


  Anasema, “…Nasema ana dharau na ana kiburi kwa kuwa akitoka Dar es Salaam anatakiwa kuripoti kwangu na wilayani. Yeye huwa anapitiliza moja kwa moja kwenda kijijini kwake Lufilyo.”


  Mwangungulu alimnukuu Mwakipesile akisema, “Yeye (Profesa Mwandosya) amemwambia rais anihamishe kutoka mkoa huu, eti sina maendeleo yoyote.”


  Alisema, “Mimi ndiye mkuu wa mkoa. Ndiye ninayepanga ratiba ya rais ya mkoa huu. Kwa hali hiyo, Rais Jakaya Mrisho Kikwete hatakanyaga Lufilyo labda niwe marehemu au niwe nimehamishwa kutoka mkoa huu.”


  Habari zinasema Mwakipesile aliona kuwa iwapo rais atakwenda kijijini Lufilyo, nyumbani kwa Profesa Mwandosya, basi waziri huyo angeweza kupata ujiko wa kisiasa.


  Hata hivyo, Rais Kikwete alifika kijijini hapo mwaka jana baada ya kuombwa binafsi na Profesa Mwandosya wakati huo wakiwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani.


  “Wakiwa Marekani (Mwandosya na Kikwete), Profesa alimuomba rais atembelee kijijini kwake kwa mwaliko wa mkewe, Mama Mark Mwandosya kwa ajili ya kufungua kituo cha watoto yatima cha Lufilyo. Ndipo Mwakipisile alipotaka kuhujumu ziara hii,” anasema kiongozi mmoja wa serikali aliyeulizwa iwapo anafahamu lolote kuhusiana na suala hilo.


  Alisema, “Katika ziara yake ya kwanza mkoani Mbeya baada ya kurejea kutoka Marekani, viongozi wa mkoa hawakumpangia kutembelea Lufilyo. Lakini katika ziara ya pili, rais aliagiza kutoka Dar es Salaam, kwamba anakwenda Mbeya na anataka akifika tu, aende Lufilyo.”


  Baada ya maelezo ya Mwangungulu, ndipo Profesa Mwandosya alipochukua hatua ya kumuandikia Mwakipesile kutaka kuweka kile alichoita, “kumbukumbu na matumizi ya baadaye.”


  Katika barua yake ya tarehe 16 Aprili 2010, Profesa Mwandosya anasema, “…Naambatanisha kumbukumbu (transcript) ya kikao ulichokifanya (Mwakipesile, Mwalimu Mwangungulu na Mwakajumilo) Jumatatu ya Pasaka 3 Machi 2008 pale Mbeya Hotel. Somo la mazungumzo linajieleza lenyewe…ikiwa ni pamoja na washiriki wengine.”


  Anasema kiini cha kupeleka kumbukumbu hizo zinazodaiwa kuandikwa na Mwalimu Mwangungulu, ni ili azipitie “na kufanya marekebisho” atakayoona yanafaa.


  Barua ya Mwandosya kwenda kwa Mwakipesile ilikuwa na kichwa cha maneno kisemacho, “Kumbukumbu ya mkutano wa tarehe 3 Machi 2008.” Ilikuwa na Kumb. Na. MJM/JIMBO/RM/02.


  Hata hivyo, Mwakipesile hakufanya marekebisho katika waraka wa siri aliotumiwa, badala yake aliandika barua ya kurasa mbili iliyojaa tuhuma, shutuma na lawama kwa Profesa Mwandosya.


  Aidha, ni katika barua hiyo, Mwakipesile anaingiza hata watu ambao hawakutajwa mahali popote na Mwalimu Mwangungulu wala na Mwandosya.


  Barua ya Mwakipesile ya tarehe 20 Aprili 2010 iliyotumwa kwa Profesa Mwandosya, kwanza inakiri kukutana na Mwalimu Mwangungulu na Mwakajumilo.


  Mwakipesile anasema mkutano wao haukulenga kumuangamiza Profesa Mwandosya, bali kuzungumzia maandalizi ya semina ya SACCOS.


  Akionyesha hasira katika maandishi yake, Mwakipesile anasema, “Nimeelezwa mengi juu ya masimango yako dhidi yangu, kwamba mimi John Mwakipesile nimemtafuta Mwakajumilo akuondoe ubunge.”


  Anasema anadaiwa “…kupokea pesa kutoka kwa Lowassa na Rostam ili nikuondoea ubunge wewe na Mwakyembe. Kwamba mimi, Apson, Mwambulukutu, Mulla mwenyekiti wa CCM mkoa …ni adui zako ambao tuna lengo la kukuondoa uongozi na kuharibu malengo yako ya kisiasa. Unazungumza yote hayo na mengine mbele ya wananchi huko Mwakaleli ambao mimi ni kiongozi wao.”


  Mwakipesile anasema, “Sitaki kuingia katika malumbano na wewe. Mimi bado nakuheshimu. Lakini sipendi kuniingiza katika mambo ya kijinga na ya kitoto.”


  Akiandika kwa njia ya kumwonya Profesa Mwandosya, Mwakipesile anasema, “Nisingependa tena kuchezewa kiasi hiki.”


  Wakati hali ikiwa tete katika jimbo la Mwandosya, Rhoda Mwamunyange, dada mkubwa wa mkuu wa sasa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Davis Mwamunyange, amekuwa mwanamke wa kwanza kujitosa kuwania ubunge katika jimbo la Kyela, mkoani Mbeya.


  Rhoda ni mfanyakazi wa Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) jijini Dar es Salaam na mtumishi wa siku nyingi wa vyama vya wafanyakazi nchini. Jimbo la Kyela linashikiliwa na Dk. Harrison Mwakyembe.


  Wengine wanaotajwa ni George Mwakalinga mjasiriamali na mwanafunzi anayeishi Uingereza na Vincent Mwamakimbula ambaye vilevile ni mjasiriamali anayeishi Dar es Salaam.


  Habari kutoka jimbo la Urambo Mashariki zinasema Ali Karavina, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo, ametajwa kujitosa kupambana na mbunge wa sasa, Spika wa Bunge, Samwel Sitta.


  Mwingine aliyejitosa kupambana na Sitta ni Ali Kalimauganga.


  Taarifa zinasema tayari “kadi feki” 36,000 zimeingiza jimboni humo. Haikufahamika nani ameziingiza, lakini Sitta alipoulizwa kwa simu kutoka Dodoma, alikiri kuwapo kwa kadi hizo na kusema kwa ufupi tu, “Sibabaishwi na majizi.”


  Chanzo: Mwanahalisi
   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mmmh..hawa waheshimiwa wa mkoa wa Mbeya fitina tupu..ni kambi hiyo hiyo ya akina Victor Mwambalaswa Mbunge wa Chunya (wafa maji)
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kuna Wadosi wawili ambao wameji-immerse katika sakata hili, Rostam Aziz na Nawab Mulla, ambao inadaiwa wanahusiana kifamilia. Wawili hawa ndiyo wenye mafweza (ya ufisadi tu) ambayo wakiyamwaga tu, basi ni mvurugano mtupu miongoni mwa wazalendo. Ni kama vile ukiwatupia mchele kuku. Ni uchafu mtupu!
   
 4. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tutasikia mengi mwaka huu,te te te te teh
   
 5. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Poleni waheshimiwa wabunge huo ndio ukubwa tunapambana na donda ndugu lililoota mizizi, halitatoka kirahisi litapigana mpaka dk ya mwisho! Njia pekee ya kupambana nalo wekeni mambo hadhari kila yanapopatikana tuwaweke hadharani mafisadi hawa na hawa viongozi wenye njaa zao! Shame on the you Mwakipesile, Rostam, Lowasa Mulla na Mwang'onda! Mijitu mizima hovyo!
   
 6. M

  Msharika JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  jAMANI MNAYEMPIGA VITA NI PROFESSOR, AMEBOBEA KATIKA KUTAFITI NA KUCHUNGUZA MAMBO? NINYI NA MBIO ZENU ZA KIFISADI MTAKIMBIA TU , ILA SIKU AKIJA CHANGANUA MAMBO ADHARANI MTAKOMA. ITS SHAME WAZIRI MKUU MSTAAFU ANYEISHI KWA KODI ZA WATANZANIA KULETA VURUGU. ATAOSHEKI NA RICH MONDULI? NA VINGINE VINGI ALIVYOIBA? LOL SHAME ON HIM MAMVI.
   
 7. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Nina wasiwasi sana na ukweli wa habari hii. Kubenea anatumiwa na kundi la Mengi na wafuasi wake akiwemo Dr. Mwakyembe.

  Kwa muda mrefu Mwakyembe anafanya juhudi kubwa kutumia Nipashe na Mwanahalisi kuwagonganisha kati ya Mwakipesile na Prof. Mwandosya.

  Prof. Mwandosya alichukua uamuzi wa maana wa kutokumshambulia Mwakipesile waziwazi pamoja na kwamba alikuwa anajua kwamba aliachwa pale Mbeya ili amwangalie prof. Mwandosya.

  Dr. Mwakyembe hakufurahia hilo, yeye alitaka kuendelee kuwa na mikiki mikiki kati ya hao viongozi ili ile vita yake na Mwakipesile nayo ipambe moto.

  Alivyofariki mama yake prof. Mwandosya, mkuu wa mkoa alienda na prof alimpokea bila vinyongo vyovyote.

  Alivyofariki mama wa Mwakipesile, prof. Mwandosya naye alienda kumwona.

  Hawa watu wawili sio marafiki lakini pia sio maadui kama gazeti linavyotaka kuonyesha. Ila Mwakipesile na Mwakyembe ni maadui wakubwa.

  Siasa za chuki na visasi ndizo hata zimesababisha kupungua sana kwa uhusiano kati ya Prof. Mwandosya na Dr. Mwakyembe. Inasemekana prof hapendi hizo siasa za jino kwa jino na anaanza kujiweka pembeni ili asionekane wazi kwamba yuko upande mmoja.

  Rais alivyoenda Mbeya katika sehemu alizotembelea na kufungua miradi ya maana ilikuwa jimbo la prof. Mwandosya. Sidhani kama itakuwa busara eti kumpeleka rais nyumbani kwa waziri? Ataenda nyumbani kwa prof kufanya nini?

  Mbeya tujihadhari sana na hawa watu ambao wanataka mkoa uwake moto shauri ya visa vyao binafsi. Huyu Kubenea anatumika sana kuchapisha habari ambazo zinaandikwa na watu wengine na yeye faida kwake ni kuuza hilo gazeti lake.

  Mimi ni mfuasi mkubwa wa prof. Mwandosya na naunga mkono strategy yake ya kukaa kimya na kufanya mambo kwa vitendo kule kwake. Hii inamjengea sifa mkoani na hata hao wanaotaka kumwondoa hawatafanikiwa.

  Kwa Kyela Rhoda wala haungwi mkono na mkuu wa majeshi. General Mwamunyange ameamua kuwa pembeni kabisa inapokuja siasa za Kyela maana anajua madhara yake. Huyo Mwakalinga naye anatajwa kuwa mwanafunzi, mbona wote tunajua hapa kwamba ni mfanyakazi tena wa siku nyingi sana? Makosa mengine yanaharibu habari kabisa.
   
 8. mawazotu

  mawazotu Senior Member

  #8
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 27, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  asante kaka mimi mwenendo wa kubenea unanitatiza sana sana anapokua anamshambulia mtu mmoja karibia kila toleo
   
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ata huyo Mwandosya ni the same, sema tuu yupo kambi nyingine.
   
 10. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35


  Heko mkulima, Kubenea anatumiwa kuenea propaganda, watu wa Mbeya msipokua makini mtaacha kufanya shughuli za maendeleo na kushughulikia bifu za watu kutaka kuneemesha matumbo yao na familia zao...
   
 11. K

  Keil JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkulima,

  Kwenye siasa huwa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu. Unaposema Mwakipesile na Mwandosya walitembeleana baada ya kupatwa na misiba, huo sio ushahidi kwamba wanaiva. Siasa za Bongo zina mambo makubwa na ndio maana watu husema siasa ni mchezo mchafu sana. Ukikutana na mpinzani anaweza asikuonyeshe kinyongo, lakini ukimpa kisogo anakuwa wa kwanza kujadili namna ya kukumaliza. Kwenye huo mgogoro wa Mwakipesili vs Mwandosya, kuna ushahidi wa nukuu za barua. Kwa hiyo nina amini kwamba habari hizo ni za kweli.

  Tatizo lipo kwenye connection namna ambavyo Lowassa anaingia mpaka akawa headline kwenye gazeti. Nadhani ungeanzia hapo ningeweza kukuelewa zaidi. Pamoja na hayo inawezekana Lowassa akawa anaingia kwa kuwa "mtandao" haujafa, bado uko hai na vinara wake ni wale wale. Kubenea alitakiwa aweke wazi zaidi. Hata hivyo Lowassa ana nafasi ya kwenda mahakamani kama ana uhakika kwamba kapakwa matope.

  Facts nyingine za Rhoda na Mwakalinga zina utata mwingi, Kubenea alitakiwa kuzifanyia kazi ya ziada na siyo kuunganisha dots hata zile ambazo ziko nje ya straight line.

  Mwisho, ushauri kwa ndugu yangu Steve Mwakajumilo, kwa jinsi alivyoingizwa kwenye hayo mawasiliano, tayari anajiweka kwenye siasa za makundi na inaweza kumpa wakati mgumu sana kupambana na Prof. Mwandosya. Siasa za Mbeya zina mambo ya uzawa. Unapoanza kumtumia Mwakipesile kama godfather kwenye primaries, ni kosa kubwa na wajuaji wa Mbeya walivyo wataanza kuhoji. Hii habari ina damage kubwa sana kwa Mwakajumilo na aliyemuua ni huyo Mwalimu ambaye ameenda kutoa taarifa ya vikao vyao siri. Mwakipesile anajitetea kwamba walikuwa wanajadili mambo ya SACCOs, yaani Mkuu wa Mkoa unajadili mambo ya SACCOs na Mwakajumilo kama nani? Kwanini Mkuu wa Wilaya na Afisa Ushirika wa Wilaya ya Rungwe hawakuhusishwa kwenye hicho kikao? Hao ndio wahusika wakuu na pia wataalam wa hayo mambo. Kikao cha kujadili SACCOs kinahudhuriwa na watu 3? Utetezi wa Mwakipesile unazaa maswali mengi sana na ndio maana alijibu barua kwa maneno makali.

  Ndugu yangu Mwaka, pamoja na kwamba wewe ni mzawa wa Rungwe lakini nahisi siasa za Mbeya huzielewi vizuri, hivi kweli wapiga kura wa Rungwe unategemea wakuunge mkono kwa kumtumia godfather ambae ni mzawa wa Kyela? Bado ni mapema, rudi kwenye drawing board ili utengeneze upya mikakati ya ku-win nominations. Andaa timu ya wazawa wa Rungwe kwa ajili ya nominations na uwe na uhakika kwamba hawatakusaliti kama alivyofanya huyo mwalimu. Wazawa wanaelewa zaidi politics na matatizo ya wananchi so ni rahisi kukufanyia kampeni.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Jun 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kama nyie hamkubaliani na hizi habari ebu tuambieni ukweli ni Upi?......Je, mmekwenda kuwahoji watu waliosema maneno haya na kukuta ni Uongo au mnakisia tu kwa sababu yameandikwa na Kubenea.. maanake kila kinachotokea against Mwakipesile kuna watu wa kutetea pasipo kutueleza kilifanyika kitu gani kinyume cha madai hayo. Hivi huyu Mwakipesile hawezi kula njama zozote yeye ana utume gani?...

  Hata huyo Mwakyembe mbona chuki na ubaya wake umeanza tu kuzungumzwa baada ya sakata la Richmond, ndipo sisi wengine tumeanza kusikia ati majigambo yake kuwa ni udhaifu na uzembe....Mwakyembe hakuwahi kusema lolote ndani ya magazeti dhidi ya Mwakipesile, mara ghafla tukaanza kusikia Ubaya wa Mwakyembe na maelezo mengi yanayomhusu Mwakyembe from nowhere..Alipojitetea tu na kusema ni mbinu za wabaya wake kila Mwakipesile kosa!...akarushiwa madongo yeye hadi akashika adabu kulitaja jina la Mwakipesile..

  I mean jamani hivi hizi tabia za kunyenyekea watu zitakwisha lini?..Hii tabia ya kitumwa ya UNYENYEKEVU kwa binadamu ni ugonjwa mbaya sana wala sio sifa. Na Tanzania watu woote wanataka sana kunyenyekewa ati ndio sifa na ubora wa kiongozi..Maadam Mwakipesile hakutaka kumnyenyekea Mwakipesile basi imekuwa kosa..

  Mwandosya ni waziri pekee nchini (mwenye Uraia wa nchi mbili) aliyeletwa na Mkapa kinyume cha mipango ya wanaCCM - Rukwa, Mbeya..Na yawezekana kabisa uwezo wake ktk Uongozi unatishia mfumo na utaratibu mzima wa Ulaji Mbeya..Na kulingana na navyowafahamu mila na desturi za Wadanganyika wooote, chuki binafsi (inda) zinaweza kuwa sababu kubwa ya matukio yoote haya kwani mgeni yeyote unapoingia mjini toka nje, usipokwenda kuwatembelea (salimia) nyumbani kwa mtu/watu wanaokufahamu basi wewe unajenga chuki na Unalinga..

  Ati ni jukumu la mgeni kutembelea nyumba zoote za watu wanaokufahamu kuonyesha unyenyekevu wako kwao pasipo kualikwa nyumbani kwao. Ni utamaduni mbaya sana unaoonyesha ubwana na uchovu wa akili kwani mtu mmoja hawezi tembelea nyumba 20 wakati ni rahisi wa wenyeji 20 kumtembea nyumba moja (mtu mmoja)...Na wao wataalika tu yule wanayeweza kumchinjia kuku au mbuzi kama mgeni wa heshima.. Huu upuuzi gani?..Mila chafu na za kitumwa kabisa.
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mnaompinga Kubenea na gazeti lake ni mawakala au sympathisers wa mafisadi.

  Gazeti la Mwanahalisi hata siku moja halijaandika habari za kutunga, hasa ukilinganisha na yale yanayomilikiwa na yule fisadi aliyebobea Rostam.

  Ni gazeti la kwanza nchini (mengi yaliogopa) kutoa listi ya majina ya watuhumiwa wa ufisadi ya wale 11 yaliyotangazwa na Dr Slaa, list ambayo iliongozwa na JK mwenyewe. Utafunaji katika EPA, Radar, Meremeta, Mwananchi Gold, Richmond imedhihirisha yale yaliyosemwa. Jee, huo ulikuwa uzushi?

  Mtuhumiwa mmoja, Gray Mgonja hata alitishia kushitaki gazeti lakini baadaye alinywea na hatimaye akatinga kizimbani. Huo ni uzushi?

  Mimi nakubali gazeti hilo limejijengea uhasama mkubwa na wale wanatuhumiwa ufisadi, ambao wanatumia kila mbinu, pamoja na mapesa kulidoofisha gazeti na yeye mwenyewe (aliwahi kumwagiwa tindikali, alifungiwa gazeti bila sababu ya msingi na kusachiwa ofisini kwake kinyume cha sheria) -- juhudi ambazo zimegongwa mwamba kwa sababu gazeti linazidi kupendwa na kukua kila siku.

  Ukiacha yale magazeti ya udaku, Mwanahalisi lionachapisha nakala nyingi kuliko gazeti lolote hapa nchini. Kuhusu hili fanyeni utafiti nyie wenyewe.

  Hivyo wanaolipinga ni wachache mno na ni rahisi kuwapuuza tu – maana wanajitia aibu wenyewe.
   
 14. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mkuu nakubaliana na wewe. Lakini pia napenda niseme ukweli kwamba kwa mtizamo wa haraka haraka, Kubenea an bifu na Lowassa. Karibu kila gazeti atakalotoa kubenea huwa anajitahidi kutafuta kisa cha kumlima Lowassa. Na ukiangalia habari hii, vita ipo kati ya Mwandosya na Mwakipesile, sasa Lowassa, ameingiaje kwenye title ya habari wakati yeye siyo main player wa hiyo game?
   
 15. R

  Ramos JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pamoja na malengo mazuri na ushupavu anaokuwa nao Kubenea, lakini ukweli unabakia kuwa ana agenda ya siri dhidi ya Lowasa. Sioni ni kwa vipi Lowasa alistahili kubeba kichwa cha habari hii. Mi nadhani mwanahalisi wanaweza kupotosha umma kwa kuonyesha kuwa ndani ya nchi hi ufisadi=Lowasa. Wapo wengi mafisadi ambao bado wapo na nyadhifa zao ambao gazeti linaweza kuwavalia njuga, na si Lowasa tu ambaye by the way hayupo tena madarakani...
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Asante Mkuu.
  Hili bifu kati ya Kubenea na Lowassa (na swahiba mwenza Rostam) lina sababu yake, na labda nidokeze tu ninachokisikia. Unakumbuka kesi ya tindikali? Imefikia wapi?

  Imekwama kwa sababu washukiwa wakubwa behind kumwagiwa Kubenea tindikali ni wawili hao, EL na RA. Imekwama kwa sababu mtuhumiwa mmoja muhimu haonekani – mtuhumiwa ambaye ndiye mhusika mkuu wa shambulio hilo la tindikali dhidi ya Kubenea.

  Inadaiwa kasafirishwa nje baada ya tukio kama ilivyogundua timu ya Tibaigana iliyopewa jukumu la kupeleleza kesi tukio hilo. Mafweza mengi yalitembea kwa polisi kufanikisha hilo.

  Kwa uchache kabisa habari ndo hiyo. Fikiria mtu anataka kukupofua macho unamfanyaje? But don't quote me! Mwenye habari zaidi azitoe.
   
 17. P

  Paul S.S Verified User

  #17
  Jun 19, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Unacho kisema kinaweza kuwa na ukweli mkubwa ndani yake, lakini sio kila issue ya ufisadi ui connect na mbaya wako, unaweza kuanza kupoteza zana nzima. haiwezekani kila habari ya ufisadi EL au RA wahusikentu hata kwa kutunga,
  hakuna anye watetea EL, RA isipkuwa kubenea afuate taaluma yake ya habari inasemaje kama habari ni RA its ok, lakini kama sio yeye hakuna haja ya kulazimisha kumchomekea
   
 18. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Hizi siasa za Mbeya zinaumiza vichwa sana. Kwa mfano kwenye siasa za Kyela, ukija Kyela ukaona zinavyoendeshwa utashangaa huyu Mwakipesile ambaye kila siku wanasema anaingilia siasa za Kyela yuko wapi? Wanampa sifa bure Mwakipesile, kwanza sio mtendaji mzuri na hata hawezi ku contribute mawazo ya maana kwenye hao wagombea uongozi.

  Lakini unashangaa kila siku magazeti yanamwunganisha yeye na Lowassa pamoja na wagombea wengine.

  Mzee Apson ndio kabisa, amezira hata kutembelea Kyela eti mpaka baada ya uchaguzi maana akikanyaga Kyela tu, kesho yake atakuwa magazetini.

  Wote mliona jinsi Mwakalinga alivyounganishwa na Lowassa mwaka jana. Ghafla wameacha na wanaendelea kutaja jina tu. Kosa kubwa walilofanya ni hilo la kuanza kumshambulia Mwakalinga mapema maana lilitoa nafasi ya watu wengi kuanza kuchunguza kama kuna uhusiano wowote kati ya huyo Mwakalinga na Lowassa, inaelekea hawajapata chochote. Sasa mambo ya Lowassa yamehamia kwa Mwanjala na hapo juzi tumeanza kusoma yanahamia kwa Rhoda Mwamunyange.

  Hata kama Kubenea anamchukia Lowassa lakini kweli ndio kila toleo la gazeti lake amwandame mtu mmoja tu? Inafika mahali hata wasomaji wanaanza kujiuliza maswali.

  JK alifanya makosa makubwa sana kumwacha Mwakipesile pale Mbeya. Inatakiwa aletwe mtu ambaye hana upande katika makundi ya Mbeya. Prof. Mwandosya ni mtu makini sana lakini hata yeye anayumbishwa mpaka anajikuta anaingia kwenye hivi vita.
   
 19. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2010
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli muda mrefu sana mie nimesikia habari hii,toka EL akiwa Pm,kwani kuna mtu anamuandaa kuwa mbadala wa mark ni mfanyakazi bot,hana sera wala nini ni kibaraka tu.Atumtaki sie na MARK TU
   
 20. b

  buckreef JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkandara,

  Huyu profesa Mwandosya mbona alikuwepo hapa hapa? Alikuwa katibu wa wizara muda mrefu kisha akarudi kufundisha kuanzia 1994 mpaka 2000 alipogombea ubunge na kushinda.

  Hilo la uraia wa nchi mbili linatoka wapi? Toka miaka ya 80 alikuwa katibu wa wizara mbalimbali.
   
Loading...