Baadhi yetu tumefika hospitali. Tulikuwa na mmoja wa wana JF senior. Alinikuta pale. Alikuwepo mwandishi mwenzake na Shaban na mfanyakazi mwenzake mwingine. Kisha akaja mwandishi mwenzake mwingine na pia akafika Absalom Kibanda, Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima na Mwenyekiti wa TEF.
It is just another sad story kwa kweli kama wengine walivyokwisha kusema hapa. Waandishi tumeweza kuzungumza na mke wa Shaban, Mama Jay. Kitu ambacho hakiingii akilini eti polisi wa anti crime hawawezi hata ku spot exactly chumba cha mhalifu wanayemtafuta kwa mabunduki na mabastola, wanaanza kupita wanauliza uliza kwa wapangaji wenzake.
Wanaelekezwa mlango au chumba cha mtuhumiwa wanayemtafuta, Mama Jay. Bado wanakosea mlango, wanaenda kugonga kwa Mama Jay mwingine, bila tahadhari wala kujitambulisha wanaingia ndani wote kishari, kisha wanafyatua risasi kumuelekea Mama Jay (mke wa Shaban), ambaye ananusuriwa na kitendo kile cha wao kuingia kwa kasi kwa kupamia mlango kama wahalifu, anadondoka, risasi zinapigwa zinampata mwandishi wa habari, kama unavyoona kwenye picha, almanusura impate kwenye moyo. Fikiria nini yangekuwa matokeo yake. Risasi kupiga moyoni.
Kisha askari hao ambao tulitarajia wawe weledi hasa linapokuja suala la uhai wa mtu, wanaambiwa hapo si kwa Mama Jay mnayemtafuta, mbona tuliwaelekeza mlango ule pale. Kama hiyo haitoshi, askari mmoja akataka kuitoa ile risasi kwa Shaban kwa mikono. Kufuta ushahidi? Bahati nzuri Shaban aligoma, muda huu wangesharuka. Yangekuwa mambo ya kupigwa na vitu vizito. Imeshindikana.
Nane, maana hatujui filamu hii itageuzwa namna gani baadae hata kufikia tisa na kumi, wakati wanaondoka pale nyumbani kwa Shaban, akipelekwa hospitali, wakapishana na Mama Jay mtuhumiwa aliyekuwa anawindwa na hao anti crime police. Maana inasemekana wakati zogo likiendelea alikimbilia kibanda fulani mtaani hapo hapo. Wameoneshwa Mama Jay mliyekuwa mnamtafuta si huyo hapo, wala...hawakuwa na habari naye tena.
No body is safe. This is not an issue of somebody. Nchi inageuzwa pole pole, police state.