Mwandishi akimhoji mkulima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi akimhoji mkulima

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Che Kalizozele, Nov 24, 2009.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkulima amehojiwa na Mwaandishi wa magazeti kuhusu maisha ya shambani. Mkulima huyu hawapendi Waandishi wa habari, akaona vyema amchoshe katika kujibu maswali, na mambo yakawa hivi:

  MWANDISHI: Wewe unawalisha ng'ombe chakula gani?
  MKULIMA: Ng'ombe yupi? Mweupe au Mwekundu?
  MWANDISHI: Ng'ombe mweupe.
  MKULIMA: Ninamlisha nyasi na viguta vya mahindi.
  MWANDISHI: Na mwekundu?
  MKULIMA: Vilevile nyasi na viguta vya mahindi.
  MWANDISHI: ahaa sawa, na sehemu ya kulala ni wapi?
  MKULIMA: Ng'ombe yupi? mweupe au mwekundu?
  MWANDISHI: Mweupeee!!!! XXCCCZZZZHH!
  MKULIMA: Mweupe ninamlaza bomani kulee...
  MWANDISHI: na mwekundu?
  MKULIMA: Vile vile namlaza na mwenzie.
  MWANDISHI: Hii sehemu yote majumba mengi, wakati wa kulisha unafanyaje?
  MKULIMA: Yupi? mweupe au mwekundu?
  MWANDISHI: Woooteeee!!! ! [akifuka kwa hasira]
  MKULIMA: Mweupe ninamfunga kamba na kumzungusha malishoni na kumrudisha.
  MWANDISHI: na mwekundu vilevile?
  MKULIMA: Mwekundu? Mwekundu yeye namfunga kamba na kuzunguka nae kama mwenzie tu.
  MWANDISHI: Kwanini kila mara nikikuuliza huduma za ng'ombe wako unaniuliza mweupe au mwekundu halafu inatokea kuwa kazi zao wote ni sawa?????
  MKULIMA: Kwa sababu ng'ombe mweupe ni wangu.
  MWANDISHI: na mwekundu?
  MKULIMA: na mwekundu ni wangu vilevile.
   
Loading...