Mabadiliko kutoka Building Better Tomorrow - BBT mpaka kuwa Building Bashe Tomorrow - BBT

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Mabadiliko kutoka π˜½π™π™„π™‡π˜Ώπ™„π™‰π™‚ π˜½π™€π™π™π™€π™ π™π™Šπ™ˆπ™Šπ™π™π™Šπ™’ - π˜½π˜½π™ mpaka kuwa π˜½π™π™„π™‡π˜Ώπ™„π™‰π™‚ π˜½π˜Όπ™Žπ™ƒπ™€ π™π™Šπ™ˆπ™Šπ™π™π™Šπ™’- π˜½π˜½π™. TUMEPIGWA BILIONI 13.

Kwa mujibu wa wizara ya Kilimo chini ya waziri @HusseinBashe ni kwamba serikali inatumia milion 16.4 kufadhili shamba la hekta moja kwenye mradi wa Building a Better Tomorrow kwa kifupi BBT. Gharama hizi hazina uhalisia wowote kwa mtu anayejua kilimo au mkulima yoyote. Na kama zingekuwa na uhalisia kwamba mkulima anaweza kutumia milioni 16 kuandaa shamba la hekta moja ambayo ni sawa na ekari mbili basi nchi hii hakuna ambaye angemudu gharama hizo.

Fikiria unalima nini kwenye shamba la hekta moja ambalo maandalizi yake mpaka kupanda mbegu yanagharimu milioni 16? Unalima dhahabu kwenye hilo shamba? Au unalima almasi? Ama tanzanite? Maana haiwezekani shamba lililoandaliwa kwa milion 16 upande mahindi, Mpunga au ulezi halafu utegemee mtaji wako milioni 16 kurudi achilia mbali kupata faida.

Naomba kujitolea mfano mwenyewe maana ni mkulima. Msimu wa kilimo uliopita nimelima ekari 2 na kidogo ambazo sawa na hekta moja na nilivuna tani 3 au gunia 30 za kg 100. Nilikodi shamba kwa laki moja. Vibarua wakanilimia kwa ng'ombe kwa shilingi laki moja. Gharama za mbegu, madawa ya kuuwa wadudu na kukausha nyasi pamoja na mbolea nikatumia laki tano. Kuvuna na kupukuchua pamoja na mifuko ya kuwekea mahindi nimetumia laki tatu. Jumla ya gharama nilizotumia ni milion 1. Nimeuza mahindi hayo December 2022 kwa milion 2 na nusu baada ya kuuza kwa kg Tsh. 800 hukohuko shambani. Hivyo faida ukawa ni milioni 1.5.

Sasa tukirudi kwa Bwana Bashe na wizara yake ya kilimo kwa hekta 1 au ekari 2 na kidogo bajeti yao ni kama ifutavyo:
  • Kulima shamba Tsh. 4,250,000/
  • Kumwagilia Tsh. 7,500,000/
  • Kupima afya ya udongo Tsh. 2,500,000/
  • Mbolea Tsh. 1,750,000/
  • Viuatilifu Tsh. 375,000/
  • Mbegu Tsh. 112,000/-
JUMLA Tsh. 16, 487, 500/ kwa hekta moja. Sasa hiyo milioni 16 ukizidisha mara hekta 812 za vijana waliochukuliwa tayari awamu ya kwanza na wizara ya kilimo chini ya waziri Bashe unapata bilioni 13.5. Yani dakika ya kwanza kabisa mpira unaanza tunapigwa bilioni 13 na hiyo tu ni awamu ya kwanza maana hatujui mradi huu utahusisha hekta ngapi.

Hapo sijajumlisha gharama za upimaji ardhi na hati miliki ambayo wameweka ni milion 2. Na hapo pia nina mashaka kama hizo ndio bei halisi za kupimia ardhi kwa hekta. Anyway tuachane na mambo ya hati miliki turudi kwenye topic yetu.

Mimi ni miongoni mwa watu ambao naunga mkono wakulima kuinuliwa hasa vijana. Mradi wa Building a Better Tomorrow au BBT lengo kuu lilikuwa ni kuinua kilimo kupitia vijana. Lakini kwa mchanganuo unaonekana ni π‘©π’–π’Šπ’π’…π’Šπ’π’ˆ 𝑩𝒂𝒔𝒉𝒆 π‘»π’π’Žπ’π’“π’“π’π’˜ - 𝑩𝑩𝑻 na kwamba mradi huu umesukwa kimkakati kuwatumia vijana kufanya ufisadi wa mabilioni. Pengine ndio maana vijana walio wengi kama sio wote waliobebwa au kupewa fursa katika mradi huo hawajui chochote kuhusu kilimo na hawajawahi kulima. Ni wakati sasa wa CAG kwenda kufanya ukaguzi katika mradi huo.

Hawa watu ambao Rais Samia aliwapa ruhusa ya kula kulingana na urefu wa kamba zao imefika mahari sasa wanataka kukata mpaka kamba ili waitafune nchi yote ibaki na mashimo. Kuna wingu zito la ufisadi kuanzia wizarani mpaka nje ya wizara ukiachilia mbali fisadi mmoja mkongwe kupewa tenda ya kusambaza mbolea katika mradi huo.

Imekuwa ngumu sana kumtenga bwana Bashe na ufisadi kwa sababu ya watu waliomlea na kumkuza katika siasa ambao kwa kiasi kikubwa wananuka ufisadi wa nchi hii. Bado nina file zake nazipitia kupata uhakika. Miongoni mwa file hizo zinahusisha baadhi ya viwanda kikiweno kiwanda cha Mbolea ya minjingu somewhere.

Kwa mazingira haya tusitegemee kama kutakuwa na uwajibikaji wowote kwa sababu wazazi wa kisiasa wa Bashe ambao wanazo kashfa nzito nchi hii wameshinda vita dhidi ya mafisadi wa Sukuma Gang ambao nao walitesa kwa miaka mitano.

Cha muhimu sasa bila kujali tofauti ya vyama vyetu na dini zetu tuungane kudai #KatibaMpya ili angarau tuokoe chenji na maliasili zilizobakia nchi hii. Tofauti na hapo tutapigwa mnada nchi hii pengine tutakosa mpaka sehemu ya kuishi.

𝑴𝒅𝒖𝒅𝒆 π‘΅π’šπ’‚π’ˆπ’‚π’π’Š πŸ• 𝒙 πŸ•πŸŽ π‘Ίπ’–π’Žπ’– π’šπ’‚ π‘΅π’šπ’Šπ’ˆπ’–

IMG-20230510-WA0002.jpg
 
Bashe awamu hii anajiona untouchable na wizara imemshinda Hadi bidhaa za vyakula vimepanda kuliko uwezo. Ningekuwa na uwezo ningemtumbua hata hyo sera yake ni usanii tupu angeenda kusaidia wakulima vijijini na sio huu usanii wa kuacha wataalamu wa SUA.

Hafu kingine huyu ni baba haambiliki anajiona anajua.
 
Inaonekana awamu hii matatizo yapo kwenye wizara nyingi, kuanzia ya Nishati, Fedha, na sasa hiyo ya kilimo, hebu tujiulize, chanzo cha yote hayo ni nini?

Kama unakuwa na kiongozi asiyetaka kuisumbua akili yake kwenye ufuatiliaji wa mambo, anawaachia wasaidizi wake wafanye kila kitu, na wasaidizi wenyewe ndio hao wenye mawazo ya upigaji, sioni tutapona vipi.

Hapa tusidanganyane, kama Samia hatabadilisha style yake ya kuongoza serikali, awe strict kwa vitendo, asiendelee kuwaita wezi stupid hawatazikwa na pesa, basi tujue tutaendelea kupigwa kwa miaka yote ijayo atakayoendelea kuwa Rais wa nchi.
 
Inaonekana awamu hii matatizo yapo kwenye wizara nyingi, kuanzia ya Nishati, Fedha, na sasa hiyo ya kilimo, hebu tujiulize, chanzo cha yote hayo ni nini?

Kama unakuwa na kiongozi asiyetaka kuisumbua akili yake kwenye ufuatiliaji wa mambo, anawaachia wasaidizi wake wafanye, wasaidizi wenyewe ndio hao wenye mawazo ya upigaji, sioni tutapona vipi.
Mawaziri wote hawana ubunifu wanachukua papers walizozikuta na kuangalia ipi itamnufaisha

Kwa mfano hii ya Bashe ilishafanywa kwenye Makanisa ya Walokole na waumini walipigwa haswa!
 
ingawa na wewe ni walewale wa sukuma gang, genge ambalo sasa linajiona liko nje ya mfumo. Sasa mnakuja hapa kuonesha mna umia na fedha za umma, ni chuki na wivu wa kukosa. Ila km kweli huo mchanganuo ndiyo hali halisim hiyo siyo kilimo hicho ni kitu kingine. Ni kwanini serikali iwagharimikie hao wakulima kana kwamba hayo mashamba ni ya serikali?

Na wakulima wengine ambao ni wengi nani anawaandalia mashamba yao, nani anawapa mbegu na gharama zingine zote. Na km ni hivyo mama ameshapigwa na vijana, na mzanzibari mpaka aelewe wengine tumeshazeeka.
 
Mimi ni miongoni mwa watu ambao naunga mkono wakulima kuinuliwa hasa vijana

Vibarua wakanilimia kwa ng'ombe kwa shilingi laki moja.

nimelima ekari 2
Uliwafinya hao Wakulima unaodai unawaunga mkono...kwa kuwalipa Shilingi laki Moja. Yaani uliwatumia kitumwa. Ni Vibarua, ikiwa ina maana walikuwa zaidi ya wawili kwa hiyo elfi hamsini kila mmoja, wakati huo huo unategema hao waishi vipi kwa hizo hela kiduchu? Walilipa kodi? Ulilipa Kodi?

Mkuu, Wasukuma ni Kabila. Wewe kama Mwanaharakati au sijui ni Kiongozi usiwe mmoja wa watu wenye kupromote lugha za Kibaguzi. Sukuma Gang ndio nini? Watanzania hatutaki Siasa za kubaguana, na nina kushauri ukome na Kuacha kutumia msamiati Huo.

Turudi kwenye mada, Ulilipa kodi?
 
ingawa na wewe ni walewale wa sukuma gang, genge ambalo sasa linajiona liko nje ya mfumo. Sasa mnakuja hapa kuonesha mna umia na fedha za umma, ni chuki na wivu wa kukosa. Ila km kweli huo mchanganuo ndiyo hali halisim hiyo siyo kilimo hicho ni kitu kingine. Ni kwanini serikali iwagharimikie hao wakulima kana kwamba hayo mashamba ni ya serikali?

Na wakulima wengine ambao ni wengi nani anawaandalia mashamba yao, nani anawapa mbegu na gharama zingine zote. Na km ni hivyo mama ameshapigwa na vijana, na mzanzibari mpaka aelewe wengine tumeshazeeka.
Mdude ni sukuma gang?
Nacheka tu hapa na sasa huenda ni kweli hii kitu haipo
 
Inaonekana awamu hii matatizo yapo kwenye wizara nyingi, kuanzia ya Nishati, Fedha, na sasa hiyo ya kilimo, hebu tujiulize, chanzo cha yote hayo ni nini?

Kama unakuwa na kiongozi asiyetaka kuisumbua akili yake kwenye ufuatiliaji wa mambo, anawaachia wasaidizi wake wafanye kila kitu, na wasaidizi wenyewe ndio hao wenye mawazo ya upigaji, sioni tutapona vipi.

Hapa tusidanganyane, kama Samia hatabadilisha style yake ya kuongoza serikali, awe strict kwa vitendo, asiendelee kuwaita wezi stupid hawatazikwa na pesa, basi tujue tutaendelea kupigwa kwa miaka yote ijayo atakayoendelea kuwa Rais wa nchi.
Matatizo yalikuwepo siku zote na awamu zote, labda tu awamu hii watu wanaweza kuzungumza zaidi kuliko awamu iliyopita.
 
Hii nchi ngumu kweli kwahyo unataka vijana wakalime na ng'ombe???. tunataka tuachane na kilimo Cha 1960 mkuu
 
Uliwafinya hao Wakulima unaodai unawaunga mkono...kwa kuwalipa Shilingi laki Moja. Yaani uliwatumia kitumwa. Ni Vibarua, ikiwa ina maana walikuwa zaidi ya wawili kwa hiyo elfi hamsini kila mmoja, wakati huo huo unategema hao waishi vipi kwa hizo hela kiduchu? Walilipa kodi? Ulilipa Kodi?

Mkuu, Wasukuma ni Kabila. Wewe kama Mwanaharakati au sijui ni Kiongozi usiwe mmoja wa watu wenye kupromote lugha za Kibaguzi. Sukuma Gang ndio nini? Watanzania hatutaki Siasa za kubaguana, na nina kushauri ukome na Kuacha kutumia msamiati Huo.

Turudi kwenye mada, Ulilipa kodi?
Acha ushamba kodi kwenye kilimo inatoka wapi??
 
Back
Top Bottom