Mwanaume wa namna hii awekwe kundi gani

Mwanaume wa namna hii awekwe kundi gani

bahati mbaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
578
Reaction score
193
Habari za mchana wana JF, Jamani Duniani kuna mambo, Majuzi nilikutana na rafiki yangu wa kike wa siku nyingi akanipa habari za shemji yangu yaani mmewe.

Mwanaume hahudumii familia kwa lolote lile, bibie yalivyomshinda akaamua kuwaambia watoto wapike chakula chao wale kabla baba hajarudi maana haleti mboga wala kimbo la unga kwa muda mrefu tu.

Baba baada ya kurudi nyumbani kwa siku mbili mfurulizo bila kukuta chakula akamua kuanza kupika chakula chake mwenyewe, anakwenda gengeni ananua fungu la mchicha, unga, koroboi ya mafuta ya kula nk. Au naye anakuja amekula kabisa na kulala tu.

Ni kipindi cha miezi 11 sasa tangu Januari mwaka huu 2014.

Maisha haya tuyaweke kundi gani?
 
hakuna mwanaume mwenye akili duniani ambaye atafanya kitendo hicho kwa watoto wake mwenyewe huyo karogwa
 
Hivi ndoa ndo zimefika hukuuu!Mungu nisaidie nisighairi kuwa singleboy milele Amina.
 
Dah asee!!
Nyumba zingepewa vinywa mmmmmh watu tungekimbiana barabarani
 
Mwanaume hajitambui kabisa anaona yanayoendelea ni sahihi maana vikao vya usuluhishi vilishafanyika sana tu ila bwana yule akiwa machoni pa watu anajifanya kuwa anawajibika kwa kila kitu kumbe usanii tu.

Dada wa watu kachoka mpaka kuamua kufanya hivyo.
 
Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe
 
Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe

Aendelee kumuhudumia mme ambaye hafanyi mchango wowote katika familia wa kuthamini kile anachokifanya mkewe?

Kwa utaratibu huu ndoa ni ngumu tu.
 
Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe

Ulitaka huyo pakashume ale? ale watoto na mke? wakati hajaacha ki2 hata mim nisingempa hata maji.kidogo cha mama watoto hukula hilo dubwasha pepo kabisa ASHINDWE NA AKONDE MIGUU nuksi tupu!!
 
hivi ni kweli wanawake hamuwezi kututunza eehe??? mbona siye twawatunza hadi kiama??? nawauliza tu!!!
 
hivi ni kweli wanawake hamuwezi kututunza eehe??? mbona siye twawatunza hadi kiama??? nawauliza tu!!!

Mwanaume aliambiwa kuwa atakula kwa jasho siyo mke. Mbona yeye anawaza ale nini baada ya mke kumfungia huduma? Kwa nini haifikirii familia yake? Tena ukimuona ni mme wa haja machoni kwa watu kumbe ni mwili tu na mme kama binti.
 
ulitaka huyo pakashume ale? Ale watoto na mke? Wakati hajaacha ki2 hata mim nisingempa hata maji.kidogo cha mama watoto hukula hilo dubwasha pepo kabisa ashindwe na akonde miguu nuksi tupu!!
si mnataka usawa?
 
Sasa unafurahi au unasikitika hapa?
 
hana kwao huyo dada?
au ndo kung'ang'ania mpete kidoleni
 
Kwa hiyo unataka avunje mji? Hayo yanamwisho, mwenzio kavumilia, wewe bado unaishi kwenu unaona ananyanyasika!!!!

kuna watu walikuwa wanaletewa wanaume/wanawake hadi ndani lakini leo wanacheka na kufurahi

Nyie watoto wa digital vp?
Ndoa na iheshimiwe na watu wote
 
Kama huyo mwanaume anaona akiacha hela ya matumizi anamfaidisha huyo mama, basi awahurumie hata hao watoto wake.
Ila hana haya huyo haoni aibu hata kwa wanae?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom