Mwanaume usimwachie mkeo hela chumbani

Mwanaume usimwachie mkeo hela chumbani

Fact usitegemee watoto waje kukusaidia ukizeeka, wew kama umekaa miaka yote hiyo bila kujipanga then usubiri msaada kwa watoto huo ni ujinga, pambana na watoto wapambane kivyao. Kwani nani alikuwa na shida na mwingine? Wew au yeye? So be responsible kwa ulicholeta duniani na siyo ulichokileta kiwe responsible na wewe
watoto kukusaidia siyo pesa tu, kuna kulala kitandani hujiwezi akatuma hata mjukuu kukugeuza, kumbuka pesa siyo kila kitu.
 
Kila mtoto wako atakuja kuishi maisha yake ayapendayo na usizoee kutegemea watoto kwa maisha yako ya uzeeni.
Mkuu support ya watoto sio fedha, utakapokuwa mzee utahitaji zaidi uwepo wao kuliko fedha yao. Jifunzeni kutafakari
 
Sawa nimekuelewa nitakuwa natoa matumizi mbele ya watoto na nitampangia hadi idadi ya nyanya za kununua na bei ya kila fungu kama ulivyoelekeza.
 
Siwezi kufanya hayo, kuna mengi zaidi ya kufanya kumuonesha mwanangu kuwa namjali, mambo ya kutoa hela hadi ya chakula mbele ya watoto siwezi.
Kikubwa ni wewe unesha upendo kwa mama yao na kwao, hayo unayoyasema hayatakupo. Mambo ya kuwaonesha watoto bila Mimi mama yenu hata chakula kuwanunulia siwezi.
Lazima nijali heshima ya mke wangu kwa wanaye pia kuliko kuwa selfish hivyo.
 
Fact usitegemee watoto waje kukusaidia ukizeeka, wew kama umekaa miaka yote hiyo bila kujipanga then usubiri msaada kwa watoto huo ni ujinga, pambana na watoto wapambane kivyao. Kwani nani alikuwa na shida na mwingine? Wew au yeye? So be responsible kwa ulicholeta duniani na siyo ulichokileta kiwe responsible na wewe
Msaada si lazima Fedha.ukishakuwa mzee ukiwa umezungukwa na wanao inaleta faraja.
 
Msaada si lazima Fedha.ukishakuwa mzee ukiwa umezungukwa na wanao inaleta faraja.

Ni kweli kama kupewa faraja na watoto hilo ni jambo la msingi na wewe kama mzazi una haki ya kulipata kutoka kwa watoto ukiwa kijana au emezeeka
 
MWACHIE MBELE YA WATOTO NA UMWAMBIE NA MATUMIZI YAKE, NA WATOTO WASIKIE USIJE KUISHI MAISHA YA UPWEKE UZEENI

[emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427]

MWANAUME
Unamwachia mkeo hela ya Chakula Chumbani, Mke Anatoka na Kapu anaenda kununua Chakula, Anapika, Anawaambia watoto, Njooni Wanangu Mle Nimewapikia Chakula Kitamu, Watoto wakishakula Wanasema Asante Mama.

MWANAUME
Unamwachia Mkeo hela ya Nguo za Sikukuu Chumbani,
Kesho Yake mkeo Anatoka kwenda Kununua Nguo, Akirudi Anawaambia Wanangu Nimewanunulia Nguo za Sikukuu Njooni Mjipimie, Watoto Wakishajipima, Anawaambia Wanangu Mmependeza Eeee, Simnaona Ninavyowapenda
Watoto wanafurahi na Kusema Asante Mama,

MWANAUME
Kila Aina ya Pesa ya Matumizi Unamwachia Mkeo Hela Chumbani,

MWANANUME
Ukifika muda wa kutoa Ada Unamkabidhi Mkeo Hela Chumbani,
Kesho yake Mkeo Anawaambia Watoto kuwa Anaenda kuwalipia Ada ya Shule, Akirudi Anawaambia Wananhu nimeshawalipia Ada, Na gari za Shule Zitakua Zinawapitia, Nataka Msome Wanangu ili Baadae Mje Mnitunze, Watoto Wanasema Asante Mama.

KIBAYA ZAIDI
Ukifika muda wa kutoa Adhabu, Mkeo yeye hatoi Adhabu, Anawaambia Watoto, Ngoja Babayenu Arudi, Nawewe Ukirudi Unaelezwa na Mkeo matatizo ya Wanao, Unachukua Bakora Unawaadhibu Watoto, Bila kujua kuwa Unazidi Kujenga Uhusiano M'BAYA na Wanao.

NGUMU KUMEZA
Ukifika Uzeeni, Watoto wako Hawana KUMBUKUMBU Yoyote Ya Mema Uliyowafanyia.

NA
UKUMBUKE KUWA-->>
MTOTO ANAANZA KULISHWA SUMU YA MANENO KUTOKA KWA MAMAYAKE KUANZIA UMRI WA MIAKA 9 --- 15

MWANAUME KUWA MAKINI SANA

ZINGATIA HAYO KWA MAISHA YA UZEENI
Ni sahihi kabisa
 
Cha msingi umpende na kumjali mama yao hiyo itakua zawadi kubwa kwa wanao hawatakuja kusahau kamwe!
 
Back
Top Bottom