Mwanaume unashindwaje kumaliza sahani ya wali?

ELAFU

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
410
150
Labda mimi ni mlafi au mshamba, ila sijawahi kubakisha hata tonge moja la chakula cha Sh 2,000/= - 3,000/= cha kupimiwa kwenye sahani. Sasa napata maswali mengi na wakati mgumu ninapomuona mwanaume anashindwa kumaliza wali au ugali na wengine hata chipsi mayai hubakisha kiasi.

Hivi ni kwa nini? Au ndio ameshiba? Au ana haraka?

Ataweza kazi za kiume huyu za kufikisha watu kileleni kweli?
 
Hahaha anakula robo anashushia na tumaji wenyewe wanakwambia wanatengeneza figure.

Hii tabia wengi wanayo wana vyuo.

Binafsi si mpenzi wa wali
 
ELAFU

Shida unakula mlo mmoja so lazima ule sana,maana anakula milo mitatu sio lazima amalize sahani ya chips
 
Last edited by a moderator:
Mwenyezi Mungu hawapendi watu wenye kufanya Israf.
Kama uwezo wako vijiko 2 basi chukua vijiko 2, sio unachukua vijiko 3 matokeo yake kijiko 1 kinakushinda.
 
ELAFU

Hata na wewe kuna watakaokushangaa kula sahani moja tu eti umeshiba....Tatizo wewe unawaza ngono tu..
 
Last edited by a moderator:
Sio sahani ya wali tu. Hata pakiti ya karanga ya Tsh200 unaweza kubakisha vile, inategemea na mazingira....... Ngoja nikuachie katusi kadogoooo.-------mods hata kwa torch hawakaoni.
 
Ukila wakati njaa ishakupiga kumaliza chakula itakuwa tabu kidogo. Mimi asubuhi napiga chapati mbili na kokakola ml 350.

Mchana ugali wa kutosha kwa samaki na jagi LA maji.

Jioni mishkaki mi3 na bia mbili ml 375.

Shemeji yenu anapumzishwa kila baada ya siku moja, siku inayofuata anagongwa mzigo kama kawa.
 
Sahani moja unaachaje kumaliza mwanaume???
...ukiishia kupiga kimoja tu utalaumu.....kula chakula kingi muhimu sana hata bby Eshy m.s anajua.....kwanz huwa hanipi sahani moja!:D:D
 
Last edited by a moderator:
Unakuta hata hajashiba kujishaua tu mbele za watu. Kama hamalizi chskula kwanini alikinunua bwembwe za kisoro hzo
 
Labda mimi ni mlafi au mshamba, ila sijawahi kubakisha hata tonge moja la chakula cha Sh 2,000/= - 3,000/= cha kupimiwa kwenye sahani. Sasa napata maswali mengi na wakati mgumu ninapomuona mwanaume anashindwa kumaliza wali au ugali na wengine hata chipsi mayai hubakisha kiasi.

Hivi ni kwa nini? Au ndio ameshiba? Au ana haraka?

Ataweza kazi za kiume huyu za kufikisha watu kileleni kweli?

wewe unaekula wali sahani nzima au mbili na yule anaekula nusu sahani tofauti yenu ni kujaza choo tu! wewe unajaza sana choo kwasababu amount inayotumia na mwili ni kidogo sana ambayo haizidi nusu sahani!
 
Ebana hiyo menyu ya 2,000 au 3,000 ni kwa mama ntilie au..?

Nyani Ngabu Wewe Ni Wa Kishua Pande Za Obama Haya Mambo Huyawezi. Huku Uswazi Kwa Mama Ntilie Kuna Hadi Chakula Cha Sh 1,500/= Wali Maharage
 
Hao ni wanaume wa Dar, sio mimi na wenzangu wa kanda ya ziwa..

Haa Haa Haaaa...... Kuna Mtu Mmoja Na Mavazi Ya Kabila La Kwao Tulikutana Cafteria Ya Moi Pale Muhimbili Yeye Ndiye Mwisho. Alinunua Chipsi Kavu Sahani Moja Na Wali Sahani Moja Akala Vyote
 
Haa Haa Haaaa...... Kuna Mtu Mmoja Na Mavazi Ya Kabila La Kwao Tulikutana Cafteria Ya Moi Pale Muhimbili Yeye Ndiye Mwisho. Alinunua Chipsi Kavu Sahani Moja Na Wali Sahani Moja Akala Vyote

Huyooo ndo anaweza kukimbiza panya road... Wanaume wa dar vipi bhana,, utakuta mtu anakula slesi tatu,, badala ya kula mikate mitate,, slesi tatu utafanyeje kazi buana,, kazi kubwa kushinda kwenye vijewe vya kawaha kujianya wakina mwinyi mura,, mura story nyingi za ccm na ukawa sijui election.. Mbona nasikiaa dar gym kibao mura mnaenda gym ili body sivutie warembo eeeehhh.... ‘‘ umenikumbusha mbali sana mkuu““ heheh teh teh teh
 
Sio sahani ya wali tu. Hata pakiti ya karanga ya Tsh200 unaweza kubakisha vile, inategemea na mazingira....... Ngoja nikuachie katusi kadogoooo.-------mods hata kwa torch hawakaoni.

Hiko kitusi nimekiona nakusemea kwa mods. Mvivu wa kula wee
 
Nyani Ngabu Wewe Ni Wa Kishua Pande Za Obama Haya Mambo Huyawezi. Huku Uswazi Kwa Mama Ntilie Kuna Hadi Chakula Cha Sh 1,500/= Wali Maharage

Hii ni menu ya sh. 1,500 kwa mamantilie:

Ugali/Wali +..
1. Dagaa
2. Samaki kipande kimoja
3. Tembele
4. Kisamvu
5. Maharage
6. Mlenda
7. Mchuzi + nyanya chungu na bamia.

Ni hapa gongo la mboto ndo utapata msosi wenye vikorombwezo vyoote hivyo.

Hahahaha uswahilini raha sana.
 
Back
Top Bottom