Mwanaume Unalichukuliaje hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume Unalichukuliaje hili?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mamanalia, Sep 13, 2011.

 1. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2011
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Unachukuliaje kumuoa binti aliyekwisha kuzaa labda akiwa O level huko.

  Au unamsimamo gani kwa mwanamke aliyekwisha kuzaa, utaweza kumuoa akikwambia ana mtoto baada ya wewe kukaa naye wiki kadhaa kwenye uhusiano?
   
 2. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mapenzi yako kwake yatajibu swali hili.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,350
  Likes Received: 22,207
  Trophy Points: 280
  ukimpenda utamuoa tu
   
 4. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  watoto ni baraka kutoka kwa Mungu kwa hiyo kama unaupendo na mama basi penda hata watoto
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kama kuna uwezekano wa kutumua mbio nitasepa.

  mwanamke mwenye mtoto ni noma (sorry kwa wale watakaokwazika)!!

  Babu DC (1947)
   
 6. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ukipenda boga .......................................................................!!!!!!!
   
 7. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0

  UMENIKWAZA.

  kwan mwanamke aliyezaa shida yake ninin?
  nini kinabadilika?
  let say alizaaa olevel . ...as u know that tym utoto mwng so ata kujikinga sio kiivo..kapata mimba kazaa na akaendelea na shule mpk univerdty ...na hana mawasiliano na yule aliyemtia mimba sema ni dent mwenzake na wote walikuwa na miaka 18 kipindi kile...

  kumshutumu msichana peke yake na kumuacha yule aliyemtia mimba naona si haki ...au mimba aliipata choon wakat anakojoa?
  blame wote basi km ivo na mseme pia MWANAUME ALIYEZAA NA MWANAMKE UKOO NYUMA B4 KUOA ni noma..si husband material...


  2me;
  utu wa mtu aubadiliki et kisa kazaa..km ni mwema atabak ivo ivo..ever human human being anafanya mistake...sasa kumnnyanyapaa uyu kisa kazaa ahh ist fair

  kuna ambao hawajazaaa lakin dahh ni km kazaaa ..kimuonekano na kwa kila kitu

  km ni tabia kaka tabia ya mtu aibadilik et kisa kazaa bas ahh afai....


  we mchek uyo dada km yaliyomo yamo oa..ni maelewano tu baina yenu...waweza oa asiyezaa na akakuletea sarakas mpk ukamwita mungu shemeji....
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuzaa sio sababu kama unampenda kweli utapenda na kila chake sio watoto2 mpaka nduguzake, na huwezi kujua hao watoto wa mke wanaweza kukuheshimu na kukuthamini kuliko ulio zaa na huyo mwanamke au inawezekana Mungu hakukujalia mtoto na hao watoto wakakustiri.
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mpendwa sanaaana Rose,

  Nilitegemea feelings za namna hii na ndiyo maana nikaanza kwa kuomba msamaha. Maadam umeshanisamehe...nijariby kueleza niliyomaanisha katika post yangu ya awali.

  Sisi (especially wa miaka ya 1947) ni Watanzania na Waafrika, na bado tunaenzi mila zetu ambazo bahati mbaya zina mrengo wa kiume....Naamini hapo tunakubaliana.....Na kwa makunzi yetu (labda mimi binafsi), tumekuwa na imani kuwa mwanamke ni wa mtu mmoja tu (ingawa tunajua kuwa si kweli) hadi hapo tunapo-prove otherwise....Sasa kuwa na mtoto ni ishara kwamba huyo si wako peke yako! Na hilo linawauma wanaume wote hata kama hawasemi!!! ....Mimi babu yao nawasemea kwenye hili (samahani tena kama kuna atakayeguswa)!!

  Pia jamii humwona vibaya mtu anayelea mtoto wa mwenzake...Nina office mates kama 3 wana ndoa za namna hiyo ila siku zote hawana amani!

  Na jambo jingine ni matatizo yanayojitokeza mara nyingi linapokuja suala la kumlea mtoto (hapa ni nina mifano mingi ila nitaishia hapa)!!

  Nitarudi baadaye kidogo,

  Babu DC (1947)!!
   
 10. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Unaonaje na wewe ukiwa na mtoto tayari halafu ukataka kumuoa binti ambaye hajazaa?
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu J'Bonge,

  Hapa kuna mambo mawili ambayo inabidi kuyaangalia.

  Kwanza ni mtazamo wa jamii....ambapo inaonekana kwamba mwanamume kuwa na wanawake wengi hata watoto ni sawa ila kinyume chake ni jinai...Unaweza usiamini ila huo ndio ukweli wenyewe!

  Pili ni mtazamo wangu binafsi...Kwa vile sina mtoto wa nje, basi siwezi kuwa na mwenzangu (na ki ukweli sina) ambaye ana mtoto wa nje. Kama ingenitokea wakati ule bado natafuta mchumba ningeweza labda kuwa na msimamo huo au tofauti. Kwa sasa nitabaki kusema hayo!!
   
 12. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  kwangukuwa na mtoto
  Mkuu Dark City, Majibu na mtizamo wangu ni kama huo hapo juu alioutoa Likwanda. kwangu kuwa na mtoto aukutokuwa naye kwa mwanaume au mwanamke siyo kigezo. kigezo kikubwa ni mapenzi. kama kweli umempenda, mtoto huwa siyo kigezo. Nina mfano hai kabisa ambapo jamaa alioa kwa mara ya kwanza kabisa lakini huyo aliyemuoa alikuwa tayari ana watoto wawili na jamaa mpaka sasa ana watoto wa kuzaa mwenyewe na wale wa kufikia lakini anawatunza wote kama watoto wake na anawasomesha private schools na ndoa yao ina amani kabisa
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mradi alomzalisha asiwe anakula chinichini
   
 14. SaraM

  SaraM Senior Member

  #14
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jibu lako halijitoshelezi, ongeza point nyingine ili tuone na tujue kosa la mwanamke liko api, coz kumbuka kitendo kafanya na mwanaume
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sawa mkuu,

  Hakuna jinsi ambayo mambo ya maisha yanaweza kuwa generalized. Kwa hiyo kutakuwa na tofauti kati ya mtu na mtu. Pia sina tatizo na huo msimamo wako.

  Ila kwa sababu ya mjadala huu...naomba kukueleza kuwa mila zetu zinaamini kuwa kuna tofauti kubwa kati ya ndoa na mapenzi. Kwa hiyo wapo ambao wameoana wakiwa na watoto na ndoa ikawa nzuri. Pia wapo ambao wana watoto wa nje ya ndoa na maisha ni karaha tupu. Kote kote kuna mifano ya kutosha!

  Hata hivyo, neno mapenzi sina hakika kama limo kwenye mambo ya ndoa zetu (kadri ya mila tunazoziishi)...Ndoa inaangaliwa kama kitu independent ambacho kina vigezo vyake tofauti na mambo ya mapenzi ya kisasa. Ndiyo maana wazazi wanaweza kumkataa mchumba wako kwa vigezo ambavyo kwa watu walio wengi huona kama upuuzi!

  Itoshe tu kusema kuwa ndoa inaenda mbele zaidi ya mapenzi na matamanio ya ngono...kwa sababu inategemewa kuwa nanyi (mke na mume) hadi muende kwenye makazi yenu ya milele!
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Binafsi sijasema mwanamke ana makosa,

  Nimetoa mtazamo wangu na ule wa jamii...Kama hukubaliani nao ni poa tu!
   
 17. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mkuu nadhani hapo kwenye red ni suala la lugha tu. maana yangu haikuwa ya kuhusisha mapenzi na matamanio ya ngono nilikuwa na maana ya kupenda
   
 18. m

  mamanzara JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Kama suala la kuzaa ndilo linakufanya kuona kuwa huyo mwanamke si wa peke yako, unalichukuliaje suala la kuoa mwanamke ambaye sio bikra? Hiyo siyo issue, anaweza akawa hana mtoto na akawa si wa peke yako vile vile. Kinacho-matter ni upendo wa kweli - Kama kweli unampenda ......., Na wanawake nao wawachukuliaje wanaume wenye watoto wa zamani.
   
 19. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  wakikutana tu!.........,kuna jamaa alioa mke ambaye alizalishwa,baada ya muda yule mume akawa anakuja kumchek mtt.cku moja walifumaniwa wanamegana.
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nakuelewa sana ndugu,

  Ila haya mambo tumeshayaongea sana hapa JF na kwingineko. Kupenda ni jambo gumu sana na kuna watu wameishi maisha yao yote blla kujua kama wanawapenda wenzi wao au pia wao wanapendwa. Na ndiyo maana suala la ndoa linahusisha na vigezo vingine tena vile ambavyo siyo vya msimu!

  Labda tu pia nikueleze...kwa uzoefu wangu na kwa masimulizi kwamba ni nadra kwa wanaume kupenda kweli kweli...Ndiyo maana wanahanja hanja kama kuku wa kienyeji...Kwao kutamani kunachukua sehemu kubwa katika mambo ya ngono! Bahati mbaya, wenzetu wanawake huwa wanakuwa na mapenzi ya kweli kwenye mahusiano. Ndiyo maana hizi hukumu za jamii na watu binafsi zina waumiza sana.

  Ila huo ndio ukweli wenyewe...Wanawake ni wahanga wa mfumo wetu wa maisha...Labda ukibadilika!
   
Loading...