Mwanaume Unalichukuliaje hili?

Kama suala la kuzaa ndilo linakufanya kuona kuwa huyo mwanamke si wa peke yako, unalichukuliaje suala la kuoa mwanamke ambaye sio bikra?

Zamani ilikuwa ni kasheshe sana...Huko kwetu ilikuwa ni aibu mwanamke kuolewa bila bikra. Bi harusi alikuwa anasindikizwa na shangazi yake ambaye alimtandikia shuka jeupe na kama shuka halikubadilika rangi baada ya kukutana na mume wake...badi hiyo ndoa ilikuwa inabatilishwa na mahari inarudishwa mara moja...

Siku hizi mambo yamebadilika sana na hayo mambo hayafanyiki tena. Ila mwanamke kuwa na mahusiano kabla ya ndoa kunasumbua wanaume wengi na huumia ndani kwa ndani ingawa siyo jambo gumu kama anapokuwa na mtoto!

Hiyo siyo issue, anaweza akawa hana mtoto na akawa si wa peke yako vile vile. Kinacho-matter ni upendo wa kweli - Kama kweli unampenda ......., Na wanawake nao wawachukuliaje wanaume wenye watoto wa zamani.

Haya nimeshayatolea maelezo kwenye post zangu zilizotangulia. Pitia pitia na kama bado una swali rudi tuendelee kujadili!

Wanaume kwa kujipendelea, kufaidi mfaidi wote, then kulaumiwa analaumiwa aliyehifadhi kiumbe kwa miezi tisa

Kuwa na mtoto hakumpunguzii mwanamke kigezo cha kupendwa.

Kama kuna uwezekano wa kutumua mbio nitasepa.

mwanamke mwenye mtoto ni noma (sorry kwa wale watakaokwazika)!!

Babu DC (1947)

duh! Ila wanaume wa siku hizi hata amkute mwanamke ana watoto wawili yupo tayari kuoa. Nyie mababu wa kale vipi?

duh! Ila wanaume wa siku hizi hata amkute mwanamke ana watoto wawili yupo tayari kuoa. Nyie mababu wa kale vipi?

Enzi zile kwa kweli ilikuwa ni jambo gumu sana...

Pia ukweli kutoka kwenye jamii zetu ni kwamba mwanamke ambaye amezaa kabla ya ndoa ananyanyapaliwa sana....Na hii ndiyo inawafanya watu wengi waogope kuoa wanawake wa namna hiyo.

Ingawa wanawake huwa wanawakubali wanaume wenye watoto..ila uzoefu unaonesha kuwa ama au watoto au na ndoa kwa ujumla huwa zinakuwa na matatizo!

Wanaume kwa kujipendelea, kufaidi mfaidi wote, then kulaumiwa analaumiwa aliyehifadhi kiumbe kwa miezi tisa

Ndiyo matatizo ya mfumo dume...mwanamume kuwa na wake wengi (hata watoto nje) ni sifa ila mwanamke akithubutu kutoka nje ya ndoa na akafumaniwa anaambulia adhabu ambayo haitabiliki.

kama kweli unampenda itakubidi tu ulee mwana wa mwenzio, besides, that poor kid has nothing to do with what happened bach then though ndo tokeo....ila itakuwa ni issue nyingine kama the lady/ man ambaye hakuwa na mtoto kabla hamjawa na uhusiano... then mkiwa katika uhusiano yeye akatungisha "kitu na box" ...hapo sasaa kiukweli bwaga manyanga.

Back
Top Bottom