Mwanaume unakaa na mkeo kila saa kama jiwe la honge

Mwanaume unakaa na mkeo kila saa kama jiwe la honge

Najua kila mmoja ana namna ya kuishi. Pamoja na hayo nimeona vema nikawakumbusha ndugu zangu waliofungwa na vifungo vigumu vya ndoa au uchumba.

Nimeamua kuandika huu uzi nikiamini kwamba rafiki yangu Bernard atapita huku na atajifunza kitu. Juzi tulikuwa kona fulani hivi tukila mbuzi katoliki maeneo ya California, Nyegezi jijini Mwanza huku tulivuta taswira ya mazingira ya Fiesta.

Mshikaji nilimpigia toka alhamisi kwamba nitakuwa Mwanza. Sasa ile jioni mishale ya saa kumi na moja nikampigia. Jamaa akaomba excuse eti hawezi kutoka home maeneo ya Pepsi maana mkewe hatomruhusu maana hajamzoesha kutoka mida hiyo.

Nikasema Fresh kama Fareed Kubanda.
Ile kuendelea na michapo Mara meseji mshikaji anadai sorry mwanangu natamani sana tuonane maana huu mwaka wa tano tangu tuachane chuo. Nikaona huyu siyo mchizi kama Mox, nikabadilisha line kuendeleza stori Tatu tofauti kama J Mo.

Nilichogundua ni kwamba wanaume wengine siyo Mashine kama alivyo Msaga Sumu ila wanaibiwa kama Rayvanny.

Wewe ni wa kuamka na kwenda kazini, ukirudi nyumbani tu.
Hunywi pombe, huchezi bao, huchezi draft, huchezi pool table, si mshabiki wa mpira n.k

Wewe unajitafutia ugonjwa mbaya sana kuliko hata ubaya wa Baba ubaya.
Yaani wewe ukifukuzwa kazi gafla utakufa mapema kama funza maana huna stamina kama za mchwa kwa kuwa unajitenga na wadau.
Suala LA kujumuika ni kikatiba. Hivi kila SAA wewe na mkeo mnaongea nini?
Kutana na kina mhogo mchungu huku kwenye draft upigwe supa au umpige MTU force king wote mcheke akili iwe poa.

Ndiyo maana mnahangaika Mara nguvu kiume zimepungua, zitaachaje kwa mfano?

Isitoshe kinachopungua hapo siyo nguvu za kiume bali AKILI YA KIUME.
Miaka ile ulikuwa machachari, pita huku na kule tazama maua akili inafurahi ukikutana na mpango wa kando saaafi kama Kenya lakini sasa unashinda nyumbani kila SAA kama jiwe la Honge umerogwa?

Hata mwenza wako mpe muda hata kama anakung'ang'aniza kimbia fasta kama Babuu wa Kitaa ila usichelewe sana kurudi walau SAA mbili na nusu au Tatu rudi home.
Akizoea atakufurahia vinginevyo utalazimishwa kuangalia Picha za kihindi ukiaminishwa mwishoni Kali sana lakini Mara zote utaishia pahala steringi anafia kwenye maua kama nyuki wa kwenye mashamba ya Tumbaku kule Kaliua!
Zamani ushauri kama huu nilikuwa nauza 250/= Tzs lakini saizi ni bureeee. Siyo bure kama ya mtandao wa simu kwamba nunua vocha ya 1000 upate dakika 15 za bure mitandao yote msg 500 na mb 10.
Huu ushauri ni bure kweli kweli. Ukiona unakufaa uchukue mapema kama CCM lakini ukiona haukufai upotezee kama Masanja.

Alarmed!
 
Ujue hata wewe wanakushangaaa unaowashangaaa. Sio lazima kila kitu kiwe kama unavyotaka kila mmoja ana namna ya! Kujumuika, wengine huenda church kujumuika na sio lazima kwenye starehe. Mnapishana mitazamo hilo halikuweki kua sahihi mkuu.
Umewaza vyema!
 
Creatively written..'

Bigi Apu sio chini kama Ukitaka cha Uvunguni.'

Vipi alikuja lakini Mshikaji? au alibadilika jiwe la chumvi akawa analambwa tu na Ng'ombe akikamuliwa Maziwa..
 
Mwanaume mashine hawezi pata kila kitu kwa mkewe.
Usione watu wanapack magari na kujumuika kwenye vijiwe vya bao,draft,bar au kahawa ukadhani wajinga.
Hili ni suala LA kisaikolojia na afya ya akili
Mkuu nakubaliana Na wewe 100%
 
Unamuongelea kaka yangu mie maana ndio maisha yake [emoji38][emoji38][emoji38] haya yaani hujakosea
 
Mwanaume mashine hawezi pata kila kitu kwa mkewe.
Usione watu wanapack magari na kujumuika kwenye vijiwe vya bao,draft,bar au kahawa ukadhani wajinga.
Hili ni suala LA kisaikolojia na afya ya akili
Nothing iliandkwa mme na mke watawaacha wazaz wao na kuambatana pamoja, hamna sehem iliyo andkwa atakuwa na marafik
 
Huwezi ukapata kila kitu kwa mke wako,never ever mkuu.

Huwezi pata vitu vyote kutoka kwa binadamu cha muhimu ni kujua the desires of ur heart. Kama kaamua kushikana na mkewe au mmewe acha washikane na kufuatana kama kumbikumbi marafiki ni wapita njia tu utawajua wa kweli siku ukiwa kitandani unaumwa hata mavi huwezi jifuta.
 
Daah yani wewe nimekupenda bure.. Good girl. Sasa kuna wengine hawataki hayo yani muda wote mpo pamoja tu si ndio mwanzo wa kuchokana mapema huo. Yani kunakua hakuna kipya ndani miezi 9-12
ndo hivo maana na make kuna mda atatoka he mwanaume atamwacha na nani?
 
Well said.

Siku hizi vijana tumekuwa walegevu sana. Mababu zetu waliyapatia sana haya maisha. Sasa kijana wa kiume unakuta anabeba pochi ya mkewe au wanaongozana kwenda clinic.
Mkuu tatizo ni ule mkutano maarufu aliokwenda kutuwakilisha mama Getrude Mongela.
 
Well said.

Siku hizi vijana tumekuwa walegevu sana. Mababu zetu waliyapatia sana haya maisha. Sasa kijana wa kiume unakuta anabeba pochi ya mkewe au wanaongozana kwenda clinic.
Mkuu kama yeye kambeba mtoto na wewe ukabeba pochi yake kuna ubaya gani?
 
Mkuu kama yeye kambeba mtoto na wewe ukabeba pochi yake kuna ubaya gani?

Uanaume ndio unaanzaga kuishia hapo.

Msidanganywe na tamthilia za sijui wapi zile...Peru au wapi huko Amerika Kaskazini.

Mwanaume ni Kichwa cha nyumba na MWANAKMKE

1. MSAIDIZI TU

2. PAMBO LA NYUMBA

3. MTAMBO WA KUFYETULIA WATOTO

Na Mungu alimuumba hivyo, yaani awe Msaidizi wa Adamu.

Tusiwape vyeo hawa viumbe.
 
Wanawake hawawezi kukuelewa na wanaume wachache hawatakuelewa pia...lkn mwanamke mjanja ni lzm amuhamasishe mumewe ashiriki hii michezo vinginevyo... ni kuchokwa mapema sana
 
Hata baadhi ya wanawake hatupendi mwanaume anaekaa nyumbani tu 24/7 chaaa..ninini Mae?toka kachangamke na wenzio huko mtaani ilimradi tu usichelewe kurudi home
 
Tatizo hajawahi kutendwa na mwanamke katika maisha yake hivyo anawaamini 1000000% but IPO cku yakimkuta hatotamani hata kukaa nao zaidi ya wakati wa mgegedo tu?
 
Back
Top Bottom