Mwanaume, ukitumia nguvu kubwa/gharama kubwa kumpata mwanamke tambua hapo haupendwi

royal tourtz

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
255
325
Za mchana huu wadau hapo ulipo. na sisi mwenyeji wa hapa mwanza Kisesa kuna moto umetokea mda sio mrefu kwenye nyumba fulani karibu na hospitali ya kisesa ila jeshi la zima moto linafanya kazi kwa welendi mkubwa nawapongeza sana.

Turudi kwenye mada.... sio utafiti ila kwa wadada wengi ambao nimekuwanao karibu kwa maana ya kuitana kaka na dada au marafiki wa bila mapenzi. mara zote huwa wanajikuta kuwa wazi sana na kuongea mambo mengi ya moyoni na ikiwemo jamaa wanaongombea majibo hayo. na kwa vile mimi sio mngombea huwa wanakuwa wazi kunitajia msururu mrefu wa watu wanavyowapanga na kuwatumia kupata pesa.

Kitu pekee nilichogundua ni kuwa mwanamke kama anakupenda au anahisi unamfaa,huwa hatumii wewe kumuhitaji kama mtaji wa kipato chake. mfano, utakuta mnamfatilia mdada lakini katika kukuonesha kukubali anaweka kigezo cha dau kama vile ninunulie kiwanja kwanza ndio nitakufikilia, au nahitaji milioni kadhaa za biashara yangu ndio tutakuwa wote au mambo mengi kama hayo.. ukiona tu unawekewa mazingira hayo jua hapo hakuna mapenzi na utakuwa mtumwa wake kila siku na siku ukiacha tu ndio maumivu yako. kumbuka maisha hayana huruma na wewe na mwanamke hana huruma na pesa ya mwanaume.

Ukweli ninaoujua mimi ni huu. mtu yoyote anayekupenda utamuhudumia kwa hiari na yeye atakuhudumia kwa furaha na sio hadi apewe kitu...

LAKINI SIO KOSA LAO WANAWAKE ILA NA SISI WANAUME TUMEZIDI EAT AND RUN,.. NA SIKU HIZI TUMEKUJA NA STYLE YA AJABU YA KUTONGOZA.. KUWA NAKUPENDA NATAKA UNIZALIE MTOTO. NA WAO PIA NDIO WANAONA HAPA NI ATAKAYEWAHI KUPATA APATE MJIGA ATAACHWA ANALIA..

WAKATI UNATAKA MTOTO YEYE ANATAKA HELA YAKO. YEYE MWANAMKE ATAMEZA DAWA ZA KUZUIA MIMBA WEWE UTAKUWA BUZY KUTOA HELA YA MALENGO YAKE

MWANAUME UNATAKAIWA KUMUHUDIMIA MWANAMKE KWA UWEZO WAKO WOTE UNAOUWEZA HATA KAMA KUMNUNULIA NDEGE ILA UFANYE KWA HIARI NA UPENDO
 
Back
Top Bottom