Kosa kubwa utakalolifanya mwanamke ni kujilinganisha na mwanaume!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,892
Anaandika Robert Heriel.

Wanawake wengi waliokosa malezi na kufundwa wameingia katika tabu na madhila makubwa kutokana na kujilinganisha na mwanaume. Hilo ni kosa kubwa mno. Kosa ambalo wengi limewaacha kwenye matatizo makubwa.

Taikon ninawalea mabinti zangu kwa kuwafundisha kuwa wao ni sawa na wanaume lakini kamwe wasijilinganishe na wanaume. Sijui kama ninaeleweka? Mimi kukuambia haki sawa baina ya mwanamke na mwanaume haimaanishi haki zinazolingana, zinaweza kuwa sawa lakini hazilingani. Hiyo ni lugha.

Kimahesabu, kwa mfano Mungu anaposema watu wote watoe Zaka sawa kwa fungu la kumi. Ni Zaka sawa, lakini hazilingani. Fungu la kumi la mtu mwenye milioni moja halilingani na yule mwenye laki moja, lakini zote ni Zaka sawa kwani ni fungu la Kumi. Tupo sawia?

Taikon ninaposema, haki sawa baina ya mwanamke na mwanaume haimaanishi haki zinazolingana lingana. Wanasema same but not similar.

Wapo wanaopinga haki sawa (huenda wanakosea) lakini makosa yao yanatokana na wanawake wanaodhani haki sawa baina ya mwanamke na mwanaume zinalingana. Hapo hata mimi nitapinga, na siku zote nimekuwa bayana kwa mambo haya. Ni ngumu sana kunielewa ikiwa hautatumia upeo mkubwa.

Wanawake wanaojilinganisha na wanaume kwa usawa wengi wameishia kupata madhara makubwa. Kwenye mahusiano, mwanaume atabaki kuwa mwanaume na mwanamke atabaki kuwa mwanamke.

Hata hivyo mwanaume anabeba role mbili, hapohapo ni mwanaume na hapo hapo ni mwanamke. Hii ni tofauti na mwanamke ambaye hubeba role moja ambayo ni ukike tuu. Mwanaume anabeba role mbili kwa sababu ndani yake kuna ukike na ukiume (Gamete X na Y) wakati mwanamke anaukike tuu (gamete X).

Mwanamke unapoingia kwenye mahusiano lazima ujihami zaidi kwa sababu wewe ni mwanamke. Wewe ni Prey (muwindwaji) wakati mwanaume ni mwindaji (Predator).

Mwanaume anapolala na mwanamke kamwe hafikirii mambo ya mimba kwa sababu yeye sio mwanamke. Ni mwanamke mjinga pekee ambaye hatafikiria mimba wakati wa kujamiiana, ati anamtegemea mwanaume.

Huko ni kujilinganisha na mwanaume. Sijui mwanaume anarudi usiku kwa kuchelewa na wewe unataka kumuiga, vizuri muige, halafu utaona matokeo. Sijui mwanaume anachepuka na wewe unataka kuchepuka. Chepuka halafu tutaona matokeo.

Elewa kuwa kwa mwanaume mimba na mtoto sio jambo la maana kwake ikiwa hakuwa na mpango na hayo mambo, na ikiwa hakupendi ndio kabisa hata umletee mtoto anayefanana naye hiyo kwake haina maana yoyote. Hakuna uhusiano wa karibu baina ya baba na mtoto ukilinganisha na mama na mtoto.

Wewe unaona mwanaume anatia mimba wanawake wengine na wewe unamuiga kubebeshwa mimba na wanaume wengine. Halafu baadaye unasema wanaume wamekutelekezea watoto. Walikuambia wanataka watoto kutoka kwako?

Wanaume huwa hawana kitu inaitwa kumbukumbu hasa wakiachana na wewe hata kama ulikuwa unakata mauno kama feni. Wanaume hatutegemei viuno vya wanawake kufika mshindo. Yaani hakuna jitihada yoyote ambayo mwanamke utafanya ili mwanaume amwage lakini hii ni tofauti na upande wenu. Ili mwanamke afike kileleni ni lazima mwanaume afanye jitihada. Tupo sawa lakini hatulifanani au kulingana.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Unapoanzisha mada kama hizi asubuhi asubuhi, Je mapovu yatakayowatoka ma-feminist wa JF utayapeleka wapi?
 
Wanawake wanapenda maua, kusifiwa na kuambiwa maneno mazuri ...isipokuwa ukweli

Kutana na mwanaume mwenye maneno mengi halafu mmbeya uone anavyosutwa na wanawake

kila mtu asimamie uhalisia wake (ke vs me)
 
Wanawake wanapenda maua, kusifiwa na kuambiwa maneno mazuri ...isipokuwa ukweli

Kutana na mwanaume mwenye maneno mengi halafu mmbeya uone anavyosutwa na wanawake

kila mtu asimamie uhalisia wake (ke vs me)

Siku hizi wanaume ni wambeya kuliko Wanawake.
 
Back
Top Bottom