Upishi ni hobby kama nyingine tu.
wanaume wanaotetea hapa hawatumii kuni kongosho.........ila kila mwanaume lazima apike siku moja.Kumbe reference point yako ni mijini
more than 80% ya watanzania wanaishi kijijini
mie reference point yangu ni Tanzania
eti baba anaenda chota maji kisimani, chochea kuni, bandika maharage, subiri hadi yaive, pepeta mchele, pembua, pika wali
duh, binti na mama yao wako wamekaa, siielewi.
Miimi huwa napika sana tu............. nakumbuka hata nilipokwenda ukweni kwa mara ya kwanza niliingia jikoni kupika, mama mkwe akamfokea mke wangu sana kwa kuniacha nipike, lakini nikafanikiwa kumtuliza na maisha yakaendelea......
....aaaaahhhhh, kamanda huko mbona umeenda mbali bana,
hujawahi kula mahanjumati ya mzee Ali Mapilau nini wewe?
hao wanaoishi wenyewe inabidi tuwaite wagumu
mila zinatuharibu,mi kupika sijui na ni mvivu but sioni tatizo kwa wenzangu wanaojua na wenye kupenda kupika kufanya hivyo...ukiangalia hata the best chefs in the world are men
hahaha naona hili picha mpaka mzee wenger mwenyewe kaja kukugongea like lol, uskute na yeye yupo kwenye hiyo food chain hapo anasubiria
kwetu uhayani mwanaume anayeishi mwenyewe anaitwa 'nyeite' meaning 'suicidal' kama mimi bishanga abashaija.
Hehehehe,mama anaogopa kuambiwa "ahhh chakula cha leo mbona sio kizuri kama cha jana?" Kwahiyo ameona bora wazoee hicho hicho anachopika yeye.Kusema kweli ni ujinga tu na kung'ang'ania yale ya 47.
Kuna rafiki yangu mmoja tulikutana masomoni, alikuwa mpishi
mzuri sana. Tulipomaliza kila mmoja akarudi kwao.
Yule jamaa akaoa, mwaka fulani nikaenda kumtembelea, wiki mbili.
Sikuona hata siku moja kuingia jikoni (na kwa kweli alivyokuwa anapika
mke wake havikuwa vitamu kama nilivyozowea kula vyake). Nilipomwuliza
kwa nini hapiki, aliniambia mwanzo alijaribu lakini ikwa ugomvi na mke wake
hataki kabisa akaribie jikoni. Sasa nahisi huu mgando wa mawazo kuwa
mwanamume na jiko ni kama paka na maji.
Uanaume wa mtu hauna husiano wowote na kupika. Kama uanaume wa mtu ungekuwa unapunguzwa kwa kupika tusingekuwa na ma-chef wanaume kabisa.
Mwanamme kutopika imetokana na utamaduni wetu wa zamani kwamba mama zetu walikuwa hawafanyi kazi kwhaio walikuwa wanafanya kazi zote za ndani.
Mda umekwenda na maisha yamebadilika sasa; wakina mama nao wanafanya kazi nao na sio familia zote zinaweza kuwalipa wafanyakazi wa ndani.
Kwahio hakuna tatizo kama mwanaume kawahi kurudi nyumbani kabla mke
wake akaingia jikoni kutayarisha chakula. Mke akirudi nyumbani mnakula na mnakuwa mmeokoa mda ambao mngepoteza kumsubiri mama wa nyumba apike. Hapo mnakuwa mmepata mda mwingi wakutumia pamoja kujenga mapenzi yenu.
Kwahio Dada Lizzy mie sioni tatizo kuingia jikoni kabisa. Kama mke hafanyi kazi hilo mtu unaelewa lakini maisha ya sasa wote tunafanya kazi na ni vizuri kujaribu kugawana kazi za nyumbani kama hakuna mfanyakazi hili tupate mda mwingi wa kupumzika pamoja na kujenga uhusiano wetu.
Mila zilizopitwa na wakati tuachane nazo lakini zile za kukataa ushoga pamoja na shinikizo la wakubwa akina 'Bama na 'Roun tuendelee kuzipinga kwa nguvu zetu zote.
Ndio maana wengine hua mnao ili "mfuliwe". . . siuajiri mfanyakazi?
Mada inahusu kupika, ushoga ni mjadala unajiotegemea.baada ya muda si mrefu we will give in
kwani ni vitu vingapi tumevipokea?
Gender roles zipo tu
hata kama ni za 47 lakini zipo
sasa hivi kijana kusuka, toga maskio, zaa hereni, weka dawa kichwani, piga mkorogo jamii imeshanza kukubali
hata u.s.h.o.g.a tumeukubali japo tunashindwa kuukiri hadharani
Kaaazi kweli kweli.Tafsiri nzuri ya mke ni msaidizi,huwezi kutoka kwenye pilika umechoka halafu uje upike,na usiniambie na yeye alikua kwenye pilika kwani hilo sio jukumu la msaidizi,akishakuwa na pilika anakua sio msaidizi,ninapooa ninaoa coz nahitaji msaidizi na kupika ni moja ya majukumu yake!
Ahsante sana AW. Maneno mazito sana hayo.
Mada inahusu kupika, ushoga ni mjadala unajiotegemea.
Ahsante sana AW. Maneno mazito sana hayo.