Mwanaume kutawaliwa na mwanamke

Mwanaume kutawaliwa na mwanamke

upupu

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2008
Posts
614
Reaction score
198
Eti utakuta baba mzima baba mwenye nyumba ila amri na sheria zote nyumbani anapanga mama, ndugu akija kusalimia nauli ya kurudi anaomba kwa mke pesa yote ya mshahara kaisarenda kwa mama.

Yeye hana kumi mfukoni, mi sifanyi upuuzi huo, mpe pesa yake ya matumizi ya mwezi, na bajeti za nyumbani, fungu lako kubwa baki nalo mwenyewe, huwezi kukaa kwenye nyumba yako mwenyewe unakuwa kama zuzu.

Yaani ni bora kutoroka nyumbani ukiona kuwa mkeo amekushinda kumtawala, ila kwanini akushinde.

Epuka kuwa mume zuzu.
 
Ni maelewano tu ndani ya nyumba, ingawa mwanaume pia kumkabidhi mshahara wote wife dah??? Inategemea ntu na ntu.
 
maelewano tu ndani ya nyumba ilanayo kugawa mshahara wote kwa mke yataka moyo na ni kipaj hasa!!
 
Hakuna tatizo kama mmekubaliana na unapata amani full percent, maisha ni matamu umetulia na mkeo bila kelele. Kazi kwenu ninyi mnaozurula kwenye vijumba vya watu na kuchunguza nani anatawala na kutunga sheria. Tengeneza ya kwako.
 
sio kila wakati haitoshi inategemea na budget ya mwezi against priorities,,,,,,mara nyingi inatosha ukiondoa matumizi yasiyo ya lazima
 
Hao wapo wengi sana,
Ukute anaongea tu huko mtaani, home kama vile kanyeshewa, aibu.

Katika kupangilia budget na matumizi wenzetu mmetuzidi sana akili.

Nikiwa na 50000 naweza kufikiria kuwapa offer ya bia rafiki zangu, ww ukafikiria kununua mchele na unga???
 
Eti utakuta baba mzima baba mwenye nyumba ila amri na sheria zote nyumbani anapanga mama, ndugu akija kusalimia nauli ya kurudi anaomba kwa mke pesa yote ya mshahara kaisarenda kwa mama.

Yeye hana kumi mfukoni, mi sifanyi upuuzi huo, mpe pesa yake ya matumizi ya mwezi, na bajeti za nyumbani, fungu lako kubwa baki nalo mwenyewe, huwezi kukaa kwenye nyumba yako mwenyewe unakuwa kama zuzu.

Yaani ni bora kutoroka nyumbani ukiona kuwa mkeo amekushinda kumtawala, ila kwanini akushinde.

Epuka kuwa mume zuzu.

Mume ni kichwa cha familia, mke ni shingo ya familia na shingo ndio inaiendesha kichwa.

Unataka ubaki na pesa wewe za nini? Utaishia kuweka heshima baa. Tunawajua nyie
 
Mkuu muombe mungu tu unafikiri kumtawala mwanamke ni ujanja wako.
 
Eti utakuta baba mzima baba mwenye nyumba ila amri na sheria zote nyumbani anapanga mama, ndugu akija kusalimia nauli ya kurudi anaomba kwa mke pesa yote ya mshahara kaisarenda kwa mama.

Yeye hana kumi mfukoni, mi sifanyi upuuzi huo, mpe pesa yake ya matumizi ya mwezi, na bajeti za nyumbani, fungu lako kubwa baki nalo mwenyewe, huwezi kukaa kwenye nyumba yako mwenyewe unakuwa kama zuzu.

Yaani ni bora kutoroka nyumbani ukiona kuwa mkeo amekushinda kumtawala, ila kwanini akushinde.

Epuka kuwa mume zuzu.
Mkuu ni jambo jema sana kumwachia mkeo pesa ingawa si zote
Na ni jambo jema pia ndugu zako wakikuomba fedha unawambia waende kwa mkeo hata kama utampa fedha wewe mkeo mkiwa ndani then unampa maelekezo kwamba fedha hii mpe fulani kwa ajili ya shule yake au nauli au kitu chochote
Zipo faida nyingi sana za kufanya hivyo nitazitaja baadhi
Kwa kufanya hivyo unamweka karibu sana mkeo na ndugu zako ambao wengi wao huwa wana madharau kwa wake zetu
Pili unaweka dhana ya uwazi ndani yanyumba bila kificho na hivyo kuepuka makelele ya mkeo kukuhisi kwamba unatumia fedha vibaya
Tatu unamfanya mkeo awe na nidhamu ya matumizi ya fedha kwa sababu atakuwa anajua kipato chenu vizuri na unamweka wazi kabisa kwamba ukitumia vibaya hiyo hela usinishike shati
NAKUSHAURI JARIBU LEO UTAONA RAHA YAKE
KUMBUKA USIMPE FEDHA YOTE ILA MPE UHURU WA KUWA NA FEDHA
 
Angel
nimeipenda sana post yako.

Ni kweli mume ni kichwa cha familia na mke ni msaidizi wake kama yasemavyo maandiko katka vitabu vya dini.But believe me not hawezekani katu kumtawala mume kwa kutumia akili zetu. Mpende, muombee, muombee tena na tena, communicate na kuonyana. Nafasi ya mke katika mahusiano na iheshimiwe.
 
Hii nayo ngumu kumeza. kuna jamaa alikuwa akimpa hela mkewe ashike akapata safari ile kuondoka tu mke akamnunulia mchepuko wake bodaboda, jamaa kurudi mke hana hela zikabaki story, jamaa kufuatilia akaonyeshwa bodaboda ya mme mwenzie, kwa kua jamaa alikuwa mbabe akaenda kumpa kisago na kuchukua piki. hadi leo ile ndoa imebaki tulee watoto. mumu anachepuka huku, mke anachepuka huko
 
Umeangalia aina moja tu ya familia
Kuna familia zingine mama ndo mtafutaji kwa hiyo na yeye akifika home anamkabidhi mzee zote sababu ndiye kichwa cha familia?!
 
Hii nayo ngumu kumeza. kuna jamaa alikuwa akimpa hela mkewe ashike akapata safari ile kuondoka tu mke akamnunulia mchepuko wake bodaboda, jamaa kurudi mke hana hela zikabaki story, jamaa kufuatilia akaonyeshwa bodaboda ya mme mwenzie, kwa kua jamaa alikuwa mbabe akaenda kumpa kisago na kuchukua piki. hadi leo ile ndoa imebaki tulee watoto. mumu anachepuka huku, mke anachepuka huko
 
Umenigusa sana MwanajamiiOne. Natamani wakuelewe. nilitaka nihighlight ila naona nitahighlight yooote kabisa.
Angel
nimeipenda sana post yako.

Ni kweli mume ni kichwa cha familia na mke ni msaidizi wake kama yasemavyo maandiko katka vitabu vya dini.But believe me not hawezekani katu kumtawala mume kwa kutumia akili zetu. Mpende, muombee, muombee tena na tena, communicate na kuonyana. Nafasi ya mke katika mahusiano na iheshimiwe.
 
Last edited by a moderator:
Mwanamke akiwa ndie mtafutaji haimuondoi kwenye nafasi yake kama msaidiza wa mume katika familia. Atafute ashirikiane na mume katika kupanga maendeleo ya familia.... after all ni FAMILIA yake na mumewe..... sio ya jirani wala rafiki na ndio maana tunaambiwa siri za ndani ya ndoa zibaki ndani. Usipojinadi nani atajua kuwa wewe ndo unatunza familia??

Haya mambo yenu ya uzungu ya pesa yako ni yetu au mshahara wako ni wa maendeleo ya familia na pesa au mshahara wangu ni wangu yanawapotosha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom