Mwanaume kubeba mimba

Mwanaume kubeba mimba

Habari za asubuhi mabibi na mabwana. Kichwa cha hbr cha husika.
Naombeni msaada, usiku wa kuamkia Leo kuna jambo limenitokea ambalo nashindwa kbsa kulielewa japo sio Mara ya kwanza ni Mara ya pili sasa. Jambo lenyewe liko hivi
Usiku nimeota kuwa nimebeba mimba yaani ni mjamzito tena cha kushangaza kbsa mimba mapacha ilihali mm ni jinsia ya kiume. Hili jambo limenisikitisha kabsa mpka na kukosa usingizi baada ya kushtuka kutoka usingizini
Ndoto hii ilinikuta majira ya saa kumi alfajiri ya kuamkia Leo. Kimsingi ndoto ya aina hii ilishawahi kunitokea mwaka juzi miezi kama hii lakini mwaka huo ndoto haikuwa ya mapacha nilichukulia kama jambo LA kawaida tu kuota lakini Leo limenishtua sana sijui kwa nini. Ikiwa usiku naota niligusa tumbo nikakuta kitu kimetuna ambacho kinacheza, Mara nikajikuata Niko wodi ya wazazi huku hao mapacha wakicheza na wale wamama pale wodin wakasema mimba yangu ni mapacha
Lakini cha kushangaza ni pale wanapocheza wanatoa mikia nje ya tumbo ndipo niliposhtuka na kujiuliza ni viumbe gani hawa ndani ya tumbo langu kama ni watoto wa kawaida inakuwaje wanamikia? Kiukweli niliogopa sana ndipo usingizi ukashtuka kutoka usingizini. Binafsi nahisi sio jambo LA kawaida kwa mwanume kuota ndoto za aina hii. Nahisi ni jambo LA kiiman zaidi
MSAADA. Najua humu jf kuna wajuvi wenge wa haya mambo wenye uwezo wa kutafsiri ndoto wanisaidie na kuniondolea hofu kama kuna jambo linaloendelea pasipo mm kujua mpka sasa nawaza sipata jibu hasa ni kitu gani kinachoashiria ndoto za aina hii hasa kwa jinsia ya kiume ingekuwa wa kike may be ingesound kidgo sasa wa kiume?mmmmmh hapna NAOMBENI MSAADA
Nimefanikiwa kuupata huu uzi.. Je tuendelee hapa hapa ama kule? Usikwazike na negative replies
Ndoto huwa ni jambo la kiroho zaidi na maono pia... Hasa zile ndoto halisi vivid dreams yani hata ukiamka utaikumbuka mwanzo MWISHO
Ndoto huja kinyume kwahiyo sio ajabu kutokea umebeba mimba japo kuna feeling ya ukakasi kidogo
Mimba ni kiumbe kilichomo tumboni na umri wa kukaa tumboni ukiisha kitakota
Kwenye kutoka kuna mambo matatu au mane yanaweza kutokea
. kujifungua salama mtoto asiye na kasoro
. kujifungua mtoto mwenye kasoro
. kujifungua kiumbe mfu
. kujifungua lakini mama akafariki
Ukiyatafsiri haya kidunia ni Changamoto na mambo tunayokutana nayo kila siku mipango yetu kushindwa kwetu na kushinda
Mimba ya mapacha ni kiwakilishi cha mambo mawili kwa pamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kila mtu hapa jamii forum. akianza kuongea pointi ni shida kwani majukwaa yatapoteza ladha halisi. huu mchanganyiko wa komenti za kilokole, kihuni, wasio na dini. wavulana wasichana mabibi na mabwana ndio utamu wa jf yani unakuta id za waheshimiwa wanatoa michango ya chooni yaani safi tu jf raha sanaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana mkuu kama nakuelewa hivi maana nimeliota leo mida hiyo hiyo anayoisema jamaa sasa nikaona nitafute kwa mitandao ndo nakutana na hiki na michango ya wenye akili timamu pamoja na wenye akili
Hope upo serious ktk hilo ulilolieleza hapa. Mara nyingine mimba huonesha kuwa umebeba maono au vision fulani ndani yako ambayo bado haijafanyiwa kazi yaani bado iko ndani yako. Ni muhimu kuomba kujua umebeba nini na lini unatakiwa ufanyie kazi hicho ulichobeba. Kinyume na hapo jaribu kucheki mawazo yako huwa muda mrefu unawaza nini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom