Mwanaume hawajibiki chochote katika familia

Mwanaume hawajibiki chochote katika familia

bahati mbaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
578
Reaction score
193
Habari wanajamii forum,

Mimi ni mama, mme wangu hawajibiki kwa chochote katika familia. January aliniambia nikope pesa ili mtoto aweze kwenda shule na baadaye atarudisha kwa kusema kuwa mambo yake hayajakaa sawa.

Mpaka ninapoandika ujumbe huu pesa hajarudisha na July ndiyo hii ada inatakiwa tena. Je mme huyu yuko sawa kweli? Au kuna shida nyingine. Maana yuko kimya kabisa.
 
ni mfanya biashara au mwajiriwa?..unahisi hela anazo ila hataki kutoa?
 
Mwanamke una roho mbaya ww, umeshindwa kumuambia mwenyewe mpaka uje useme huku?
Unahisi ukimsema huku ndo atabadilika?
Nyie ndo type ya wanawake ambao mwanaume akiporomoka kimaisha,mnabaki kuwasengenya na kuanzisha fujo za kipuuz!
 
wanaume wengine wanapendwa kulelewa..sasa ukichepuka hapa ili kupata mkwanja atamlaumu nani...vumilia tu kwa maana ushaapa kwa shida na raha..msitiri kwa kumsaidia majukum maana ndo zigo lako hilo ulilolipenda bibie...valentina pita hapa mama terry
 
Kwanini huo ushauri usingeomba waliokuwa mashahidi wenu wakati mnafunga ndoa? au kama hamkufunga ndoa hakuna wazee wa busara au familia mjadili hayo mambo?
OK. Nimeenda mbali sana kwanza pole. Hapo ch kufanya mchunguze mumeo anatatizo gani kikazi au kibiashara. Baada ya kugundua tatizo lake tafuta suluhu kwa kukaa naye chini ukiwa umempa haki yake kinyumba muongee nini tatizo kwa mazungumzo ya kubembeleza lazima akuambie. Hayo mambo ni ya ndani kweni si jf
 
vunja ukimya mwambie AWAJIBIKE kwa namna utakayoona ni sawa mume ni wako mwenyewe ko ongea nae... but maisha kusaidiana
 
bahati mbaya aisee kweli unabahati mbaya.... we somesha watoto tu achana na maswala ya kumkopa mumeo off course huna mwanaume una mtoto mwingine ndani.............mpige vibao ukiona mazungumzo hayafahi
 
wanaume wengine wanapendwa kulelewa..sasa ukichepuka hapa ili kupata mkwanja atamlaumu nani...vumilia tu kwa maana ushaapa kwa shida na raha..msitiri kwa kumsaidia majukum maana ndo zigo lako hilo ulilolipenda bibie...valentina pita hapa mama terry

Oyaaa... rudi kwenye jukwaa lako kule. Mods Evelyn Salt na Madame B wanakuita.
 
Last edited by a moderator:
Mwanamke una roho mbaya ww, umeshindwa kumuambia mwenyewe mpaka uje useme huku?
Unahisi ukimsema huku ndo atabadilika?
Nyie ndo type ya wanawake ambao mwanaume akiporomoka kimaisha,mnabaki kuwasengenya na kuanzisha fujo za kipuuz!

Nimemkumbusha mara nyingi hatoi ushirikiano.
 
Back
Top Bottom