Mwanaume anapomtaka mwanamke

Mwanaume anapomtaka mwanamke

Hakuna mwanamke anayekupenda bila sababu na ikitokea kakupenda jua ana lake jambo! Mara nyingi wanawake wanaficha maovu yao ili kumridhisha mwanaume kuwa ni mtu mzuri wa tabia na ana huruma mfano mvumilivu,msikitivu na anakusikiliza hata kama huna pesa . Ila anapoingia katika ndoa anabadilika na kuwa kinyume chake mfano anakuwa mkali na anataka umsikilize yeye hata kama hakina maana ili mradi ni yeye kwanza . Kingine mwanamke anajiachia sana mfano ananenepeana na wakati kupita kiasi wakati unamuoa alikuwa potable lakin sasa ni mnene acha sasa sio honey tena au dear bali sijui umuiteje maana maana ni kituko
Na mwisho mwanamke huwa hawapendi ndugu wa mwanaume lakin wakati wa uchumba alionesha kuwa familia/ndugu aliwaonesha upendo wa hali ya juu na akikubaliwa kuolewa basi anabadilika simtaki fulani akanyage kwangu mara hivi mara vile
Ushauri
Kuwa na sababu ya kupenda si vibaya cha msingi ni kumpenda yeyey na wanaomuhusu na mpende kwa dhati maana wakati unampenda ulimfanyia tathmini ndo maana ukamkubali maana Wanaume hawana ubavu wa kukufanya umpende na yeye hana ubavu wa kuchagua wa kuwa naye ila wanawake wanaweza sasa na wasiwe na tamaa sana na kutaka maisha ya haraka huenda mwanamke huyohuyo alichangia kumfili mmewe au hata kumdhuru ili aachiwe mali kwa hiyo wanaume wanaishi kwa taadhari nyingi
Kingine kutoa siri/unyumba/nk kwa rafiki wa mme je iman inakuwaje '' Badilikeni na tunzeni siri zenu na pia aangalieni miili yenu sio kunenepeana hovyo tu na kuweni wavumilivu maana wakati unamchagua uliona anakufaa na hakuna mwingine duniani kaama ulomchagua yeye na kuweni wakweli msifiche makucha/maovu yenu kwani mtawapata wanaopenda mnayoyafanya'' Pia fanyeni tafiti muda mrefu ili mpate kuwajua mnaowapenda maana tamaa mfano nikimkataa atachukuliwa na rafiki ni hatari maana unaingia bila kumfahamu
 
Tatizo
  1. wanawake wengine kabla hawajaolewa wanakuwa wanajipenda na wapo very smart, lakini wakiolewa wanakuwa wanajiachia tu hawaendelei kuwa smart.
  2. Wanawake wanahamishia mapenzi yote kwa watoto, hawaendelei kuwajali waume zao. Mume anajiona hana thamani tena.
  3. Wanawake wakishaolewa wanaanza kuwa na kiburi.
  4. Mwaka wa kwanza mwanaume anaongea mwanamke anasikiliza. Mwaka wa pili mwanamke anaongea mwanaume anasikiliza. Mwaka wa tatu mwanamke na mwanaume wote wanaongea, majirani wanasikiliza.
Tafakari, chukua hatua
 
Hahahahaha lol! Nimetetea Wanaume wote wenye mapenzi. Si umeona Mbu kafungua uzi kumkumbuka la azizi wake waliokula maraha ya dunia enzi zao kama wapenzi

ha haaa, rafiki ulivyojitetea!
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaha lol! Nimetetea Wanaume wote wenye mapenzi. Si umeona Mbu kafungua uzi kumkumbuka la azizi wake waliokula maraha ya dunia enzi zao kama wapenzi

nilikuwa nakuchokoza tu rafiki....
mbona "This video has been removed by the user"?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Mimi na marafiki zangu wengi tunaitwa baba nanihii na tuko proud kwa hilo.... kwanini wewe ukiitwa mama nanihii unamaindi sana??

Hommie tuna nini mimi na wewe? Hujui muda wangu bado haujafika? Huu mwezi mtukufu wakezo AshaDii na gfsonwin umewaacha wapi wapumuwe???

mwezi huu wanapumzika zaidi nyumbani hommie Asprin, hapana chezeya mfungo
 
Last edited by a moderator:
am not attension seeker EMT mawazo yenu ni muhimu kwangu kwani bado sijaingia huko kwenye ndoano ni vizuri kujua yanayojiri humo

So, kwa nini unataka uwe unaitwa "baby" badala ya jina lako au "Mama Kadadaa"?
 
mkwe hapa mna diskasheni gani?
nani hataki kuitwa bebi?
mimi ngoja aendelee tu kuniita, inasaidia kunifanya nionekane bado nipo kwenye mstari, lol!
Kuna siku moja mr alikua anaumwa mama mkwe akaja basi sijui alijisahau akaniuliza hivi darling wako anaendeleaje. Ni mama mtu mzima nilishindwa kushangaa maana jina hili huwa tunaitana toka uchumba sasa tumezoea sana kiasi kwamba hata tukiwa ktkt ya watu hujikuta tunaitana hivi. Kiukweli kuna raha yake bwana si vema kusitisha eti kisa msha oana au kwa kisingizio cha utu uzima.
 
So, kwa nini unataka uwe unaitwa "baby" badala ya jina lako au "Mama Kadadaa"?

majirani waniite mama kadadaa na yeye aniite hivo haikuji kabisa angalau kidogo jina langu kuliko mamaa kadadaa
 
zipo sababu nyingi zinazosababisha mambo haya katika ndoa, baadhi ni zifuatazo:-
1. kutumia uongo mwingi wakati wa uchumba wenu, yaani kutokuwa wakweli wakati uchumba
2. kushindwa kujipa muda mwingi na wa kutosha wa kufahamiana kati yenu
3. kwa makusudi, wakati wa uchumba kila mmoja anajitahidi kujiweka sawa ili aweze kumfurahisha mchumba wake kwa kila hali, zikiwemo kauli nzuri, mapenzi ya muda, kujipamba na kila aina ya madoido
4. kujenga imani ya mafanikio kubwa juu ya ndoa yao
yote mkishakuoana, mnayaona ya kawaida, na yafuatayo yanaanza kutokea.
1. care inapngua pande zote mbili kwa mwanamme na mwanamke, pengine hata nidhamu
2. madoido ya kujipamba, kauli zinabadilika, majibu ya mkato yanaanza kujitokeza
3. kujiamini kunakuwepo, wasiwasi wa kuachwa unapungua maana tayari ndoa imefungwa, pengine haina hata talaka
4. mbwembwe wakati wa tendo la ndoa zinapungua, malalamiko yanaongezeka, kama vile nimechoka, sitaki, naumwa,n.k
 
Hakuna mwanamke anayekupenda bila sababu na ikitokea kakupenda jua ana lake jambo! Mara nyingi wanawake wanaficha maovu yao ili kumridhisha mwanaume kuwa ni mtu mzuri wa tabia na ana huruma mfano mvumilivu,msikitivu na anakusikiliza hata kama huna pesa . Ila anapoingia katika ndoa anabadilika na kuwa kinyume chake mfano anakuwa mkali na anataka umsikilize yeye hata kama hakina maana ili mradi ni yeye kwanza . Kingine mwanamke anajiachia sana mfano ananenepeana na wakati kupita kiasi wakati unamuoa alikuwa potable lakin sasa ni mnene acha sasa sio honey tena au dear bali sijui umuiteje maana maana ni kituko
Na mwisho mwanamke huwa hawapendi ndugu wa mwanaume lakin wakati wa uchumba alionesha kuwa familia/ndugu aliwaonesha upendo wa hali ya juu na akikubaliwa kuolewa basi anabadilika simtaki fulani akanyage kwangu mara hivi mara vile
Ushauri
Kuwa na sababu ya kupenda si vibaya cha msingi ni kumpenda yeyey na wanaomuhusu na mpende kwa dhati maana wakati unampenda ulimfanyia tathmini ndo maana ukamkubali maana Wanaume hawana ubavu wa kukufanya umpende na yeye hana ubavu wa kuchagua wa kuwa naye ila wanawake wanaweza sasa na wasiwe na tamaa sana na kutaka maisha ya haraka huenda mwanamke huyohuyo alichangia kumfili mmewe au hata kumdhuru ili aachiwe mali kwa hiyo wanaume wanaishi kwa taadhari nyingi
Kingine kutoa siri/unyumba/nk kwa rafiki wa mme je iman inakuwaje '' Badilikeni na tunzeni siri zenu na pia aangalieni miili yenu sio kunenepeana hovyo tu na kuweni wavumilivu maana wakati unamchagua uliona anakufaa na hakuna mwingine duniani kaama ulomchagua yeye na kuweni wakweli msifiche makucha/maovu yenu kwani mtawapata wanaopenda mnayoyafanya'' Pia fanyeni tafiti muda mrefu ili mpate kuwajua mnaowapenda maana tamaa mfano nikimkataa atachukuliwa na rafiki ni hatari maana unaingia bila kumfahamu

hapo kwenye kufanya tafiti ni pazuri zaid ni vizuri kumjua mpenzi wako vizuri kabla hujamuweka ndani hayo yoye utayaepuka,na unapoona mkeo anabadilika kunenenepa ni mahomones tu pengina kabla hujamuoa alikuwa na stress kibao sasa amerilax ndo mwili wake halisi unakuja,hapendi ndugu zako sijui matumizi yasiyo ya lazima mkalishe chini mweleze mabadiliko unayoyaona na ajirekebishe kuliko kuumia roho
 
mi nahisi sisi wanawake ndo tunasababisha, unakuta mdada ameolewa akiwa mrembo with definite shape lakini baada ya kuzaa mtoto mmoja tu hali inabadilika, hajijali kuanzia mwili mpaka usafi! mdada anajiachia tu ananenepeana hadi anatisha worse still yeye anaona kawaida tu, usafi ndo kabisa wala hazingatii akili yooooote kwenye mtoto! sasa hapo mume ataacha kupunguza mapenthi! mtu umezeeka ghafla aibu hata kukuita "baby", "honey" ,"darling" inabidi tu uitwe mama fulani coz linaendana na ulivyo......wanawake tubadilike tuige wenzetu wa majuu, lea mwanao after 3 months anza jitihada za kuloose "baby weight" ili urudi kwenye mstari na usafi wa hali ya juu.
 
Nahisi pengine mtu alipokutana na mwenzi wake alikua overwhelmed kiasi kwamba kuna vingi hakuaweza kuviona . Sasa mnapokua mmekaa pamoja kwa muda ndo anapata nafasi ya kumtazama vema mpenzi na kugundua hakua ametaka wa aina hii. Ingefaa mtu akaoa/kuolewa na anaempenda na si anaemtamani ie watu waongozwe na mapenzi hapo lbda itasaidia
''

Pia na wanawake wengine huchangia maana wanaume wengine huwa wanampenda mrembo ila sometimes wanakuwa wanajali mambo yao, kinachotokea mwanamke anaanza kulaumu mara ohoo unijali mara unachukua muda mchache na mie ohoo mara una lugha sio nzuri, kwa kuwa msela anampenda mrembo wake anaamua kujibadili na kufuata mwelekeo wa mrembo wake mwisho wa siku mbele ya safari anashindwa kuendelea kwa kuwa amejiingiza kwenye utamaduni sio wake, kikubwa ni pande zote kuwa real maana issue ya mapenzi kupungua huwa kwa pande zote especially kwa wale ambao wanapenda kukaa muda mrefu kwa pamoja wanasahau kuna kipindi kila mmoja atakuwa na mishe mishe kiasi kwamba kupiga simu mara kwa mara inakuwa ngumu
 
Mbona nje ndio wanavyoitwa wababa mpaka wanasahau kulipa ada za watoto.
huko ni nje,
na kwa kuwa persistence ya kuita "bebii" ni ngumu ndo mana divorce rate iko kubwa.
Ukiacha kuita tu anajua humpendi, talaka.
 
''

Pia na wanawake wengine huchangia maana wanaume wengine huwa wanampenda mrembo ila sometimes wanakuwa wanajali mambo yao, kinachotokea mwanamke anaanza kulaumu mara ohoo unijali mara unachukua muda mchache na mie ohoo mara una lugha sio nzuri, kwa kuwa msela anampenda mrembo wake anaamua kujibadili na kufuata mwelekeo wa mrembo wake mwisho wa siku mbele ya safari anashindwa kuendelea kwa kuwa amejiingiza kwenye utamaduni sio wake, kikubwa ni pande zote kuwa real maana issue ya mapenzi kupungua huwa kwa pande zote especially kwa wale ambao wanapenda kukaa muda mrefu kwa pamoja wanasahau kuna kipindi kila mmoja atakuwa na mishe mishe kiasi kwamba kupiga simu mara kwa mara inakuwa ngumu
Uko sahihi mkuu lkn mimi wangu hajaacha kabisa kuniita jina alilokua ananiita kipindi kile hakuna hata simu wala internet. Cha msingi wanandoa wapendane na wajitahidi kuboresha mawasiliano pia wasiache kwenda na wakati. Si unajua mkuu mambo mengi yamechange hasa sisi wa miaka ileeeeeee lazima twende na teknolojia inavyotaka kama sms basi jizoeze kutuma
 
Back
Top Bottom