Mwanaume anapodanganywa na msichana

Mwanaume anapodanganywa na msichana

@zinduna umenifanya nikumbuke mbali sana hii thread yako na umenikumbusha mbali sana na inatukumbusha machungu ambayo unayapata baada ya kuweka too much expectation kwa binti na siku ya siku unakumbana na kituko cha mwaka au aibu ya mwaka au hata kumwagiwa kinywaji au kutukanwa mbele ya kadamnasi kisa ulitegemea jibu positive linatoka negative .

Huwa sometime tunajipa matumaini kuwa hapa nilipo na nilipofika ni kama kumuangusha tembo kwa fimbo yaani sitakataliwa. Kumbe unakuta mwenzako yuko mbali kabisa na wala hana hilo wazo na wewe na tatizo ni ile wanaume tunaamini mwanamke hawezi kukukataa wala kukuaibisha mahali popote au kwa hii hatua niliyofikia mimi na yeye. Na kwamba hapa alipofikia ana asilimia mia ya hisia za kunipenda wala hatanikataa. Na yanayo tudanganya zaidi ni matendo na hisia wanazo onesha muda mwingine zinazo tupelekea tuzichanganye na hisia za mapenzi na unakuta hizi hisia wala sio za mapenzi ni za kukupenda tuu kiurafiki zaidi.

Nakumbuka ilikuwa 2006 kuna binti alitokea kunizoea sana kwenye mazingira ya kazi. Yaani kazini ilikuwa kama kumbikumbi kila swala analopata au analoambiwa lazima anishirikishe na kazi zangu zile ambazo zilikuwa zinahusu labda fani yake alikuwa hasiti kuzifanya kwa moyo hata kwa kuchelewa kuondoka kwenye mazingira ya ofisi. Muda ambao alikuwa free hana majukumu makubwa ofisini kwake ni lazima aje kwangu tunapiga story na muda mwingine anaona kwenda canteen mchana haina maana anaenda analeta msosi tunakula pamoja ofisini. Kwangu mimi niliona kwa kuwa alikuja mgeni ofisini na mtu wa kwanza kumzoea alikuwa mimi niliona ni just a friend na kutafuta kampani ya mtu wa karibu na kumfanya asijione mpweke kwenye mazingira ya ofisi mpya.

Tukitoka ofisi japo tulikuwa na usafiri wa pamoja ni lazima ahakikishe nimefika home kwanza na yeye anakuwa wa mwisho kwenda kushushwa na dereva na akifika lazima anitext kwamba amefika home kwake salama. Usiku baada ya msosi na akishajua na mimi nishamaliza kula ni lazima tunaanza mazungumzo kwa sms au simu na yanachukua muda mrefu sana kuongelea masuala mbalimbali mpaka ya ndani kabisa ya kimapenzi kuulizana mahusiano yetu na wapi tulijikwaa katika mahusiano na wapi tunapaswa kurekebisha katika mahusiano iwapo tutakuwa kwenye mahusiano mapya.

Mahusiano na urafiki huu uliendelea kwa kufikia kutoana out weekend na kupeana zawadi mbalimbali kwenye siku za kuzaliwa au Valentine na yeye alikuw aanaongoza sana kunipa zawadi siku yoyote akijisikia anakuletea zawadi. Kwa ofisi kila mtu alielewa kuwa hapa hawa ni zaidi ya marafiki ila siri ilikuwa ndani ya mioyo yetu. Wakati huo sikuwa kwenye mahusiano baada ya kuachana na mtu wangu wa karibu. Na ofisini walikuwa wamnaelewa kuwa kipindi hicho niko single sina mtu so walipoona ule ukaribu wakajua hapa ni penyewe hawa wameshakubaliana. Japo haikuwepo hisia mwanzoni kuwa anaweza kuchukua nafasi yoyote maishani mwangu nilianza kumpenda kutokana na kujali kwake na namna alivyonichukulia. Alikuwa hafanyi maamuzi yoyote bila kunishirikisha au kwenda mahali popote bila mimi kuwa na taarifa yuko wapi na anafanya nini kwa wakati huo. Mwanaume hisia zikawepo kuwa anaweza kuwa rafiki mzuri na niende zaidi ya hapo kuwa mpenzi wake na mwandani wa maisha yake ya baadae.

Nakumbuka ilikuwa birthday yangu na ni yeye alinifanyia surprise. Alitayarisha kila kitu sehem ambako tulikuwa tunapenda sana kwenda. Aliwaambia baadhi ya marafiki zake na baadhi ya marafiki zangu ambao nilishawatambulisha kwake. Tulipotoka ofisini jioni akaniomba niende home nibadilishe siku hiyo ananitoa out. Nilikubaliana nae na nikaenda nyumbani kujiandaa na wakati nampigia kumuuliza yuko wapi nimpitie yeye alinijulisha sehemu ya kukutana so nisihangaike nimkute sehem ile yeye ameshatangulia.

Kwa kweli alipendeza katika siku ambazo nilikuwa natoka nae out siku hiyo alivunja sanduku. Alikuwakatika ubora wake na bora zaidi ya siku zote. Kukutana tena na ile surprise ya birthday aliyoniandalia nilijikuta moyoni nawaza today will be my date nivunje ukimya au nitajikuta nachelewa kuomba jamvi.

Wakati sherehe inaendelea nilivunja ukimya na kumweleza hisia zangu juu yake............................. to my surprise ilikuwa pigo kubwa sana na sherehe yote iliharibika. Kwanza alipata mshtuko na kuongea maneno ambayo yaliniumiza sana. Alinichukulia kama rafiki yake wa karibu na mshauri wake na kamwe hakutarajia hata siku moja nivuke huo mstari. Machozi yalimtoka na ikawa ni kazi kumbembeleza ili nisije nikaharibu sherehe. Japo alitaka kuondoka nilifanikiwa kumtuliz ana akabaki ila sio katika uchangamfu tena kama wa awali.

Iliishia pale pale kurudi ofisini mazoea yakapungua na ule ukaribu ukatoweka na tukabaki kama friends. Hadi niandikapo ameolewa na ana mtoto mmoja kwa sasa ila still we are friends japo sio tena maana ni mali ya mtu nisije kumtibulia kwa mume wake.
 
Hahaha hiyo ilishawahi nitokea wakati nipo chuo but nikajifunza kutokana na makosa,akatokea nyingine sikufanya makosa nilikuwa naishi mwenyewe nimepanga nje ya chuo kuna wadada walikuwa marafiki zangu so wkend wakaja nichukua kwenda club,usiku wakati wakurudi kwa vile chuo kipo mbali wakaja lala kwangu wote wawili tena kitanda kimoja Mimi wameniweka kati hehehe tena wamevaaa zile nguo zao laini za ndani usiku nilishindwa pata usingizi Mara nilaliwe Mara nipandishiwe miguuu but sikujaribu kuwashika,kulipo kucha wakaishia kucheka tu huku wakisema duuu wee kiboko angekuwa mvulana mwingine hapa tungejikuta tumechafuka hahaha kumbe hawakujua Mimi nilikuwa nawavuta mdogo mdogo mwishowe wakanizoea balaaa unajua kilicho tokea niliwala wote wawili na maisha yakasonga so ushauri wangu wanaume tusiwe tunakurupuka tuandae mazingira kila kitu kitajipaaaaaa
 
kweli kuna vitu mtu.unaezafanya afu.mwenyewe usivielewe....
kuna braza man 1 alikua rafiki angu tulikutana harusini tukapeana namba miaka ilee tukawa tunachat tukazoeana sana yani akituma.msg nisipojibu atanimind huyo na.mie pia hvo hvo, tukipata chance tunatoka tunakula na kunywa narudi home tunachat hadi mambo yetu yaleee...nlikuaga naenjoy sana.kukaa nae harufu ya perfume yake.mi hoi akiniaga ananihug...siku alokuja.kuniomba nilimchukua na ndo ikawa mwisho wa mawasiliano mweh.hata sijui kwanini!!!
 
kweli kuna vitu mtu.unaezafanya afu.mwenyewe usivielewe....
kuna braza man 1 alikua rafiki angu tulikutana harusini tukapeana namba miaka ilee tukawa tunachat tukazoeana sana yani akituma.msg nisipojibu atanimind huyo na.mie pia hvo hvo, tukipata chance tunatoka tunakula na kunywa narudi home tunachat hadi mambo yetu yaleee...nlikuaga naenjoy sana.kukaa nae harufu ya perfume yake.mi hoi akiniaga ananihug...siku alokuja.kuniomba nilimchukua na ndo ikawa mwisho wa mawasiliano mweh.hata sijui kwanini!!!
Usinifanyie hivyo...
 
Hahaha hiyo ilishawahi nitokea wakati nipo chuo but nikajifunza kutokana na makosa,akatokea nyingine sikufanya makosa nilikuwa naishi mwenyewe nimepanga nje ya chuo kuna wadada walikuwa marafiki zangu so wkend wakaja nichukua kwenda club,usiku wakati wakurudi kwa vile chuo kipo mbali wakaja lala kwangu wote wawili tena kitanda kimoja Mimi wameniweka kati hehehe tena wamevaaa zile nguo zao laini za ndani usiku nilishindwa pata usingizi Mara nilaliwe Mara nipandishiwe miguuu but sikujaribu kuwashika,kulipo kucha wakaishia kucheka tu huku wakisema duuu wee kiboko angekuwa mvulana mwingine hapa tungejikuta tumechafuka hahaha kumbe hawakujua Mimi nilikuwa nawavuta mdogo mdogo mwishowe wakanizoea balaaa unajua kilicho tokea niliwala wote wawili na maisha yakasonga so ushauri wangu wanaume tusiwe tunakurupuka tuandae mazingira kila kitu kitajipaaaaaa
Una moyo wa chuma...
 
Kuwa na urafiki na mtoto wa kike.......ni sawa na kuwa na kuku kama pet.......mwisho wa siku lazima umnywe supu.......

hii mbinu ya kivita aliitumiaga S.........anyway........mwisho wa siku tulibatizwa Samaki na Paka........if you know wora am saying..........ha ha ha.......halafu weee dereeeeee...........

watu wazma tumeshaelewa,,,,, nafkiri hapo ukawa unauliza ww S.... Unataka nn? Huku unatanua upaja kidogo kidogo..... Jaman S... Subir kwanza basi nivue mwenyew wakat huo unaruhusu anavyokuvua... Mpaka ukajikuta joka limeingia shimon hahahaaaa!
 
Sijui huwa inakuwaje lakini ndio hivyo..........binafsi washkaji zangu wengi ni wanaume........na huwa tuna uwezo wa kufanya mambo mengi sana ya heshima na ya kipuuzi kwa pamoja........lakini akitokea akanza kunitongoza.........huwa tunaleteana mbaya........lakini urafiki haufi...........nikiona mazoea yanazidi naua urafiki.........nauibua tena siku nyingineeee........maisha yanaenda...........

heheheee! Hapo kwenye kuleteana upuuzi hapo..... Hapo lazma maji yamwagwe kitandan na shuka lichanwe.... Naomba namm niwe rafik yako teh!teh teh
 
Sijui huwa inakuwaje lakini ndio hivyo..........binafsi washkaji zangu wengi ni wanaume........na huwa tuna uwezo wa kufanya mambo mengi sana ya heshima na ya kipuuzi kwa pamoja........lakini akitokea akanza kunitongoza.........huwa tunaleteana mbaya........lakini urafiki haufi...........nikiona mazoea yanazidi naua urafiki.........nauibua tena siku nyingineeee........maisha yanaenda...........


na suala la kutongozwa lpo upand gan kati ya heshima....ama...upuuzi????
 
Acha hizo zote sasa kuna hii yangu.
Nimekutana na mtoto mahali fulani, mtoto kanichangamkia na mimi bila kupoteza nafasi nikamchangamkia zaidi, tukaongea mengi kwa sababu mimi nilikuwa nimefikia hotel moja kali sana, ilivyofika usiku nikamwambia mimi naenda kulala ila ningependa tuende wote, bila hiyana akakubali. Na ukimcheka mtoto yuko vizuri, choo kipo vizuri, mguu ni tembo style na sio Flamingo style. Basi tulipofika room mimi nikaenda kuoga then naye akaenda kuoga tukapanda kitandani huku tukitaniana maneno ya kimahaba, sasa si mimi nikamvua boxer then ikachukua buti nikavaa, ile nataka kumchojoa kufuli ili niue, si akasema yeye hawezi kuduu na mimi eti it was just a company. Yaani mpaka asubuhi nikatoka patupu, dah siwezi kusahau ile pua niliyoangukia.
Sijawahi kuona mwanamke mwenye roho ya ukatili kama yule mweeee!

daaah hii kali....hapo hata matumizi ya ubavu inaruhusiwa kama unammudu......lkn mkuu labda size ya mtwangio ilimtisha ...
 
Huu uzi umenikumbusha matukio mawili yaliyoniumiza sana,ILA baada ya kuwagundua wanawake siku hizi sijiaminishi kwao Kaaabisa kuondoa stress zinazozuilika na zilizo ndani ya uwezo wangu.
 
Sio kila mwanamke akikupenda usifikirie amekupenda kimapenzi.Tatzo ss wanaume tunafikiria mbali sana halafu tunafiria wrong,
unaweza kupendwa tu kwa ucheshi, upole,ukarimu, maneno yako ya faraja kwakke na mengne mengi lakini wakati huo hana hisia yoyote kimapenzi,

Kama sio dada yangu wala ndugu yangu yeyote hata akinipendaje najiandaa kutumbukiza tu ile mambo...hakuna cha kunipendea sijuu ucheshi,ukarimu...
 
Tatizo wengi wakishakataliwa ndio urafiki unavunjika, ila mimi siwezi kuwa mshika pembe!

unataka kuniambia unikatalie halafu tuendelee kuwa marafiki?mwanaume hakuumbwa hivo.....kwanza kukataliwa tu najiona nimedhalilishwa aiseee!!halaf et niendelee kuwa mshika pembe?THUBUTU

Huu sasa ni wivu aisee, koloni halita ulitawale wewe unakasirika, hutaki hata wengine walitawale khaa!! mnanichekesha kwa kweli

Hivi kwanini unamkatalia rafiki yako? Unapungukiwa nini ukimpoza kiu rafiki yako

Makubwa haya, sasa tumkubali kila rafiki ili hali mtu unamarafiki wengi basi tufanye maonyesho, au tuzianike kwenye mabango kwaajili ya marafiki

halaf umenikatalia,ukinikuta na mwingine nikakwambia mpenzi wangu unanuna?HAPA TATIZO LINAKUWA NINI ATI?

Wasiwasi wako tu, nikikukataa nakukataa jumla wala sigeuki tena ikibidi nakukuwadia ili usinisumbue.
 
Teh Teh Zinduna umenifanya nicheke sana na hii thread yako na umenikumbusha mbali sana..na umenikumbusha hasira nilizo zipata baada yakukumbana na hiyo hasa namba nne!

Muda mwingine sisi wanaume huwa tuna kosea sana tena sana maana huwa tunaamini mwanamke hawezi kukukubali au kukupenda bila kuwepo na hisi za mapenzi ndani yake kumbe sivyo!Na yanayo tudanganya zaidi ni matendo na hisia wanazo onesha muda mwingine zinazo tupelekea tuzichanganye na hisia za mapenzi!

Na kumbuka ilikuwa 2008 kuna binti alitokea kunizoea sana na ilikuwa haiwezi kupita siku bila kunitafuta au kuonana tukapiga story na muda mwingine alikuwa hadi aniletea zawadi na ikifika muda wa chakula cha mchana ananishitua tukale..na uwezi amini mimi mwanzo nilimchukulia kama rafiki wa kawaida kabisa..lakini baadhi ya watu walifikiri nina uhusiano nae.

Huyu binti ilikuwa hawezi kulala kabla hatujaongea au kuchati na kutakiana usiku mwema na alikuwa anaonekana mwenye furaha sana hadi marafiki zake wakawa wanasema huyu lazima umuoe kabisa hapo hata sitamtongoza hata sikuwa na fikiri kufanya hivyo maana nilimuona kama rafiki tuu!

Baadae nilianza kupata hisia za kutaka kumtongoza na nilipata msukumo zaidi kutoka kwa marafiki zangu wakiniambia hatuamini kama huna uhusiano na fulani...na anavyo onekana anakupenda ...acha uongo wewe..haiwezekani..daaa

Baadae nilifikiria nikasema lazima nifunguke sasa na haitakuwa shida maana ni wazi ana nipenda kabisa kwanza ataanzie wapi kukataa? niliangalia mazingira yote nikaona hayampi nafasi kukataa kabisa na haiwezekani!

Sasa kwakuwa ulikuwa ndio mwezi wa Valentine nilisema nitaitumia siku hiyo kumsprise na kumfungukia...nilikwenda dukani nikanunua card,mau na zawadi ya pochi..nikavianda vizuri hii ilikuwa siku tano kabla ya Valentine(nilifanya maandalizi mapema sikujua yatakayo nikuta)
Ilipo baki siku moja kabla ya tukio nikamtumia sms kuwa leo jioni nataka tuka kae sehemu tupige story..akasema "poa tena nitakuwa wa kwanza kufika utanikuta" daa nilifurahi sana na nikajisemea moyoni daa tayari nimepewa ushindi wa mezani.
Ulipo fika muda nilia andaa zawadi zangu nilijongea eneo la tukio na kuanza kunywa soda.. baada ya dakika ishirini alifika na kukaa ..cha kwanza akaniambia "Siamini hujaniletea zawadi nika mwambia usiwe na wasi wasi... nikashika kifurushi nika mkabidhi akachunguliaa akacheka akasema nimezipenda lakini nitaziangalia baadae asante...daaa..nikasema nisichelewe nikaanza kufunguka..duuu nikamweleza kila kitu...

Niliishiwa nguvu alipo niambia ruttashobolwa samahani kakaangu mimi "nilikuwa na kuheshimu na nitakuheshimu na upendo nilio nao kwako ni wadada na kaka tuu na sikutegemea kama tutafika huku na siwezi kabisa maana kweli wewe ni muhimu kwangu lakini si jinsi ulivyo fikiri...na zawadi zako siwezi kuzichukua maana haitakuwa fair..samahani naomba niende" nilijaribu kubembeleza wapi ndio kwanza alibadilika na kuchukia na sikuwai kuona amechukia kiasi kile..aliondoka na kuniachia zawadi zangu duuu..niliishiwa nguvu kabisa na kumbuka pale bar nilikuja kuondoka saa 5 na huwezi amini urafiki ulikufa na akabadili namba kabisa....sikuamini kilicho nitokea na ilikuwa funzo kwangu....

Hakuna kazi iliyo ngumu kama kujua mwanamke anataka nini...kwakweli nilipatwa hasira sana na aibu juu

Inaumaga sana hiyo...kwanini hakukuita kaka siku zote? Hao ndio huwa wanatukanwa,au labda kalikuwa bikra.
 
Last edited by a moderator:
Ndo maana huwa sitongozi msichana, huwa nawavutia kwa kile wapendacho. Tunajikuta tayari
 
Unakutana na mwanamke, unamtongoza anakubali, unamuomba mtoko anakubali, mnaenda kuvunuja amri ya sita na wote mnafurahia na masifa kibao mnamwagiana kwa ufundi mliouonesha pamoja. anafurahia kila kitu chako. Ukimuambia nataka nikuoe anakuambia hapana wewe siyo chaguo langu.

Hahaha...acha tu mkuu
 
Back
Top Bottom