Mwanaume anapodanganywa na msichana

Mwanaume anapodanganywa na msichana

Sitaki kusikia una urafiki na kiumbe kiwacho chochote cha jinsia ya kiume. Wivu wangu mpaka kwa kaka zako.

Nishawadelete wote, toa shaka my darling, kwa jinsi unavyonijali mzee wewe, vijana nishatupa tupa kuleeeeee.
 
kweli kuna vitu mtu.unaezafanya afu.mwenyewe usivielewe....
kuna braza man 1 alikua rafiki angu tulikutana harusini tukapeana namba miaka ilee tukawa tunachat tukazoeana sana yani akituma.msg nisipojibu atanimind huyo na.mie pia hvo hvo, tukipata chance tunatoka tunakula na kunywa narudi home tunachat hadi mambo yetu yaleee...nlikuaga naenjoy sana.kukaa nae harufu ya perfume yake.mi hoi akiniaga ananihug...siku alokuja.kuniomba nilimchukua na ndo ikawa mwisho wa mawasiliano mweh.hata sijui kwanini!!!

Teh Teh Mwl ulifanya ukatili kwa nini?
 



Hebu wanaume leo mnipe ushuhuda, kama hamjawahi kukutana na hiki kizungumkuti cha wanawake.

1.
Unakutana na binti anakuchangamkia na kila mnapokutana anakusalimia kwa bashasha huku akikupa tabasamu maridhawa linalokushawishi kumtongoza kutokana na kuvutiwa naye, lakini unapothubutu kumwambia ya moyoni anakutolea nje kifedhuli kiasi cha kukuumiza moyo wako


2. Inatokea kila asubuhi uendapo kazini na urudipo kazini unakutana na binti huyu mnayeishi naye mtaa mmoja na kila mkutanapo anakutupia macho ya mahaba huku akikusalimu kwa heshima na upendo, mara mojamoja mnapata fursa ya kuongea mawili matatu kuhusu maisha na pilika za mjini na anaonekana kuvutiwa na wewe kwa jinsi unavyozungumza naye kwa upendo,anaonekana dhahiri kukupenda na haachi kujipitisha pitisha pale inapotokea uko kibarazani kwako ukipunga upepo, moyo unakulipuka kwa mapenzi unaona huyu ndiye, lakini unapojaribu kumtupia nyavu anachomoa na kukupotezea mazima humuoni tena na anaanza kukukwepa. Unajikuta ukijiuliza huyu mwanamke ni mzima kweli au ana wazimu?


3. Mnakutana kwenye Party au Klabu, wakati wakucheza mziki anakufuata na kukuomba mcheze,unapocheza naye anakuchezea kwa manjonjo ya kimahaba huku akikushika shika nakukugeuzia makalio yake na ma hipps yaliyojazia jazia na wewe ukipata fursa yakuyashika na kuufurahia utukufu wa Muumba kiasi cha kusababisha maumbile yako ya chini kututumka kwa ashki na tamaa ya kimwili huku akili yako ikikwambia,’leo lazima nikaufaidi huu utukufu wa Mungu.’ Mara muda wa kufunga mziki umefika na kwa kuwa ni usiku wa manane kila mmoja sasa anatoka kutafuta usafiri wa kurudi kwake. Ukiwa umefuatana naye kutoka nje ya Klabu huku ukijiamini utamudu kumshawishi uondoke naye kwenye Ki Vitz chako cha mkopo, mara anakuonyesha jamaa aliyepaki Toyota MarkX akimsubirina anakujulisha,

‘Yule ni mpenzi wangu amenifuata, ahsante kwa kampani, uwe na usiku mwema…!‘

Anakuaga hivyo na kukuacha ukiwa umeduwaa. Unabaki ukisaga meno na kung’ata midomo kwa hasira……



4.
Mnafanya kazi katika jengo moja, na mara kwa mara mnakutana kwenye mghahawa kwa chakula cha mchana na wakati mwingine kwa evening coffee, wewe unakuwa ni mtu wa utani mwingi na masighara, na kila unapofanya utani anacheka na anaonekana kuufurahia utani wako na pia anaonekana kuvutiwa na uwepo wako kila mnapokutana, kwa kifupi ni kwamba anaonekana dhahiri kukupenda. Jambo hilo linakufanya utake kumvuta ili awe mpenzi wako, si kajilengesha…! Unapojaribu kumuomba mtoko ili upate wasaa wa kumtongoza anakutolea nje na kukwambia hayuko interested na wewe… unabaki unashikwa na mshangao, ni kitu gani hiki kinakutokea…


Hebu wanaume nipeni mauzoefu yenu kama mlishawahi kukutana na moja kati ya hivi visirani nilivyovieleza hapo juu

CC:
Kaizer, Asprin Kiranga The Boss, Nyani Ngabu, Mwita Maranya, Preta, snowhite, gfsonwin, King'ast, Ruttashobolwa, lara 1, Mr Rocky

Mkuje mtoe maushuhuda yenyu

duhhhh xo alikuchungulia?
 
Last edited by a moderator:
Wengine wanafaa tu kuwa marafiki ila hawanogi kuwa wapenzi
 
unaponikataa unategemea nini. nmekupa wakati wangu na kukuonyesha kuwa nmevutiwa kimapenzi na wewe mpaka naamua kukutamkia.
then kutokana na sababu unazozijua wewe unajikuta umenikataa, ok no sweaty kidume najipanga upya nakuja na mistar mipya bado unakataa.
then hamna shida kidume naamua kumpa chance demu mwengine unaanza kulalamika ohh sijui nakuchukia oohh sijui nmekukasirikia !! so wewe ulitakaje eti.
muda wako umeisha siwezi kuendelea kupoteza muda wangu kwako cos nilikupa chance ukaikataa.
 
Unakutana na
binti hapa Jamii Forum. Anakupm kila saa. Anakupa like hatakama umepost
utumboo,anakusifia jukwaani mpaka unahisi mzIgo utapewa hata kabla ya
kuomba.Ila siku unamcheki pm anakupa namba za simu. Mnaanza kuchati
kwenye simu unamtongoza halafu anakutosa kama vile sio yeye hapa
JF.

tena huku jf ndo kabisaaa. kiukweli sisi ndivo tulivo. binafsi
ntakuchangamkiaaaa, storii, utumbo, yaan haya mambo napenda, siku mtu
akinitamkia mapenzi hawezi amini macho yake.

sisi tuna enjoy ule ukaribu ambao unatufanya tuwe kama kaka na dada na
si vinginevyo.
 
tena huku jf ndo kabisaaa. kiukweli sisi ndivo tulivo. binafsi
ntakuchangamkiaaaa, storii, utumbo, yaan haya mambo napenda, siku mtu
akinitamkia mapenzi hawezi amini macho yake.

sisi tuna enjoy ule ukaribu ambao unatufanya tuwe kama kaka na dada na
si vinginevyo.

Kumkataa mwanaume wa JF ni haki yako.maana humu tunaishi ulimwengu wa mtandaoni sio halisi.

Jina uongo.
Picha uongo.
Kazi uongo.
Elimu uongo.
Umri uongo.
Makazi uongo.

We are not real.ila uso kwa uso kumchangamkia mtu wa jisia tofauti bila kiambatanisho chochote ni maajabu.
 
Mr Rocky hata wewe uliuvaa mkenge. mwee!

Kusema kweli sio fair, hawa viumbe hawapaswi kututengenezea mazingira ya kuwadoea then wakatutolea nje. Urafiki unamipaka.

Mbaya zaidi hawaheshimu hisia zetu, wengi wao hawana njia mzuri za kumkataa mtu huyo, mtu anakujibu jibu la maudhi kupata usingizi hadi ujibust, mkionana confidence inarange kwenye 20% na kushuka chini. teh teh teh!
:focus:

Tena rafiki uliwajibu vipi walipokuuliza kuhusu kupungua ukaribu wenu?

Mkuu Mashaxizo huwezi kosa sababu na mkiwa mbele ya washkaji mnajifanya kama vile bado mko karibu ila ukweli unaujua mkuu
 
Last edited by a moderator:
sometime inatokea tu unapenda company na mtu Fulani yani unakuwa unaenjoy ukiwanae karibu ila hutaki awe mpenzi wako, sasa akija kukutokea tu kaharibu unaanza kumuona sio na urafiki unaanza kufa, ni kitu cha kawaida...
 
Back
Top Bottom