Mwanaume aliyempa talaka mke wake na kumuoa mfanyakazi wao wa ndani huko Zambia

Wanaume wa kiafrika ndo akili zenu zilipoishia..unafikiri ukishaoa mke umejipatia na mfanyakazi wa ndani, yeye huyo mume alikua amekamilika kwa lipi?? Sijaona sababu ya kuacha mke hapo na huyo msichana wa kazi ajiandae baada ya miaka kadhaa na yy atatafutiwa sababu., kama ninkazi wanawake kibao wanafanya kila kitu kwa waume zao bado wanaachwa na kufanyiwa ushenzi..bado tuna safari ndefu sana kwa mtindo huu Africa itabaki kuwa bara la giza milele na milele

Halaf cha ajabu hawa wanaume wanaoongea ongea amevunja ndoa yake na mikono yake mwenyewe anataka yeye apikiwe afuliwe afanyiwe majukumu yote ya mume ajabu muulize yeye kamnunulia lini mkewe hata chupi utasikia maisha ni kusaidiana mara na yeye ana kazi anunue mwenyewe, hapo analalamika hvo si ajabu wote wanafanya kazi na wote wanachoka kwa kiwango kile kile bado mtu ana thubutu kusema hafui mara hatandiki alafu zikija bili mwanaume mzima anaweka mezani agawane na mkewe nyie wanaume weusi mna shida jamani yani sijui mna akili za aina gani
Usimlaumu mme, yeye alichofanya ni kuusikiliza moyo unaosukuma damu kisha nafsi yake ikaamua adondokee kwa beki tatu ambapo amemfunika mke wa ndoa kwenye uwanja wa kuiridhisha nafsi.
 
Mimi naona huyo house girl ndo wanaendana na huyo mke wake itakuwa alikuwa anamuogopa hata kumuuliza kushindwa kutandika kitanda Ili ajirekebishe, haya sasa ngoja apambane na house girl na isije kuwa kamupendea maisha mazuri akiishiwa anaachwa solemba anakuwa wa kuanza upya mpaka anazeeka.
Mwanaume pia atakuwa ameshatuliza nafsi yake vizuri kabisa mwanamke akiondoka hakuna shida kabisa kuliko hali aliyokuwa anaishi nayo....Alafu kukimbiwa ukichalala ni kawaida wanakimbia ndugu wa damu sembuse mke?
 
Mtu mke na mtu mme hukutana na kuanza mapenzi motomoto

Wakishazoeana ubunifu huisha, hakuna kujitoa kwa mwenzie kila mtu anamtegea mwenzie ndo awe na amsha amsha.

Na atayekuwa na kiherehere cha kuwa na amsha amsha ili mahusiano yasilege ataonekana msumbufu, mkabaji, hana shughuli za kufanya kazi kufatiliana na kubanana.....

Watu hubadilika kutokana na nyakati, mazingira, watu wanaowazunguka n.k.

Ukiona uko kwenye mahusiano na mtu na anakuheshimu huyo mtu mrejeshee heshima, nakwambia lazima mstaafu pamoja hata kama mapenzi yameisha.

Mpende mkeo...

Mpende mmeo.....

Mpende mwanao....

Alisikika Machinga mmoja akinadi mataulo ya mtumba maeneo ya Karume jijini Daslamu .
bibi bhana lol
 
Mtu mke na mtu mme hukutana na kuanza mapenzi motomoto

Wakishazoeana ubunifu huisha, hakuna kujitoa kwa mwenzie kila mtu anamtegea mwenzie ndo awe na amsha amsha.

Na atayekuwa na kiherehere cha kuwa na amsha amsha ili mahusiano yasilege ataonekana msumbufu, mkabaji, hana shughuli za kufanya kazi kufatiliana na kubanana.....

Watu hubadilika kutokana na nyakati, mazingira, watu wanaowazunguka n.k.

Ukiona uko kwenye mahusiano na mtu na anakuheshimu huyo mtu mrejeshee heshima, nakwambia lazima mstaafu pamoja hata kama mapenzi yameisha.

Mpende mkeo...

Mpende mmeo.....

Mpende mwanao....

Alisikika Machinga mmoja akinadi mataulo ya mtumba maeneo ya Karume jijini Daslamu 😅.
Kasie weee,

Uwapi nikutuze?
 
Wengi wa hivyo wanapenda vitu na hivyo vitu ndo vimemvuta kwa huyo mwanaume, ifike mahali wanaume wajielewe huwezi kuwa wewe niwakuanza upya kila siku maana hapo kuna kulea mimba upya, kulea mzazi upya, kutunza vichanga upya wakati wenzio wanaongoza na watoto wao wakubwa wanapanga maisha.
Hiki kilio hakitasaidia kitu, cha muhimu mtimize majukumu yenu ndani ya nyumba, the rest is porojo.
 
Back
Top Bottom