Mwanaume aliyempa talaka mke wake na kumuoa mfanyakazi wao wa ndani huko Zambia

Wanaume wa kiafrika ndo akili zenu zilipoishia..unafikiri ukishaoa mke umejipatia na mfanyakazi wa ndani, yeye huyo mume alikua amekamilika kwa lipi?? Sijaona sababu ya kuacha mke hapo na huyo msichana wa kazi ajiandae baada ya miaka kadhaa na yy atatafutiwa sababu., kama ninkazi wanawake kibao wanafanya kila kitu kwa waume zao bado wanaachwa na kufanyiwa ushenzi..bado tuna safari ndefu sana kwa mtindo huu Africa itabaki kuwa bara la giza milele na milele

Halaf cha ajabu hawa wanaume wanaoongea ongea amevunja ndoa yake na mikono yake mwenyewe anataka yeye apikiwe afuliwe afanyiwe majukumu yote ya mume ajabu muulize yeye kamnunulia lini mkewe hata chupi utasikia maisha ni kusaidiana mara na yeye ana kazi anunue mwenyewe, hapo analalamika hvo si ajabu wote wanafanya kazi na wote wanachoka kwa kiwango kile kile bado mtu ana thubutu kusema hafui mara hatandiki alafu zikija bili mwanaume mzima anaweka mezani agawane na mkewe nyie wanaume weusi mna shida jamani yani sijui mna akili za aina gani
Dada yangu ni kama vile umejibu kwa kupanic Sana; kama swala lilienda mpaka mahakamani na mahakama ikaridhia waachane kutokana na sababu za wazi kabisa ambazo ni rahisi kuzivumilia kwa muda mfupi lakini sio kwa kipindi chote mnachoishi, inafika mahala mpaka swala la mumeo mfanyakazi wa ndani ndio anawajibika hilo binafsi naliona ni tatzo.
Mwanamke anauyejitambua siku zote yuko makini na ndoa yake..
Hatukatai mapungufu ya
 
Mtu mke na mtu mme hukutana na kuanza mapenzi motomoto

Wakishazoeana ubunifu huisha, hakuna kujitoa kwa mwenzie kila mtu anamtegea mwenzie ndo awe na amsha amsha.

Na atayekuwa na kiherehere cha kuwa na amsha amsha ili mahusiano yasilege ataonekana msumbufu, mkabaji, hana shughuli za kufanya kazi kufatiliana na kubanana.....

Watu hubadilika kutokana na nyakati, mazingira, watu wanaowazunguka n.k.

Ukiona uko kwenye mahusiano na mtu na anakuheshimu huyo mtu mrejeshee heshima, nakwambia lazima mstaafu pamoja hata kama mapenzi yameisha.

Mpende mkeo...

Mpende mmeo.....

Mpende mwanao....

Alisikika Machinga mmoja akinadi mataulo ya mtumba maeneo ya Karume jijini Daslamu 😅.
Huyo machinga alikuwa sahihi...nadhani hayo mataulo yaliisha😂😂😂😂😂😂😂
 
Wanaume wa kiafrika ndo akili zenu zilipoishia..unafikiri ukishaoa mke umejipatia na mfanyakazi wa ndani, yeye huyo mume alikua amekamilika kwa lipi?? Sijaona sababu ya kuacha mke hapo na huyo msichana wa kazi ajiandae baada ya miaka kadhaa na yy atatafutiwa sababu., kama ninkazi wanawake kibao wanafanya kila kitu kwa waume zao bado wanaachwa na kufanyiwa ushenzi..bado tuna safari ndefu sana kwa mtindo huu Africa itabaki kuwa bara la giza milele na milele

Halaf cha ajabu hawa wanaume wanaoongea ongea amevunja ndoa yake na mikono yake mwenyewe anataka yeye apikiwe afuliwe afanyiwe majukumu yote ya mume ajabu muulize yeye kamnunulia lini mkewe hata chupi utasikia maisha ni kusaidiana mara na yeye ana kazi anunue mwenyewe, hapo analalamika hvo si ajabu wote wanafanya kazi na wote wanachoka kwa kiwango kile kile bado mtu ana thubutu kusema hafui mara hatandiki alafu zikija bili mwanaume mzima anaweka mezani agawane na mkewe nyie wanaume weusi mna shida jamani yani sijui mna akili za aina gani
Ninaamini nawe huna Ndoa
 
Huyo mume anahitaji dish washer, washing machine, smart-kitchen!, si aseme tu kafuata hilo guu, hakuna masufuria, ugali katika law of attraction!!! Asimbambikizie tope mke wake wa zamani, kuachwa kunauma ila to be told you are responsible for such a mess is soo UNFAIR
Utakuwa na wewe ni muagizaji siyo mwajibikaji
 
Endelea kushupaza shingo. Habari yako kwanza mkuu? Ukoje na hali?

Mke ni mlezi wa familia ninaposema mlezi nazani naeleweka.. baba ni mtafutaji na mtunza familia ndio maana akaitwa kichwa cha familia. Majukumu yote yanayousu nyumba ni ya mke, baba kazi yake ni kutafute mpate kupata maitaji yote muhimu hapo nyumbani.

Kwa mtazamo wako sina hakika kama umeolewa ( niwieradhi kama nitakukwaza) na kama umeolewa kama huna nguvu ya ziada kumzibiti huyo mwanaume jiandae kulimwa taraka, vinginevyo ziwe story za kijiweni tu umeleta hapa

Habari yangu nzuri mkuu... I’m happily married nashkuru sana na nimeolewa na mwanaume anajielewa sana labda ndio sababu nashupaza sana shingo. Mume wangu amezaliwa na kukuzwa kwnye familia ambayo nikikwambia utaona kama ni imaginary family lakini amini usiamini ni hapa hapa bongo sio mzungu but he’s super smart nilichokua nakisema hapo juu pamoja na kwamba mke ni mlezi ulezi haumuhusu yeye pekeyake, huyo mwanaume mpaka anafikia kumpa talaka mkewe kisa hafui ni mwanaume mpumbavu sana.. nikatolea mfano kwamba si ajabu wote mke na mume wanafanya kazi lakini mume anachoangalia yeye ni kutimiziwa yake na ukite yeye majukumu yake anataka pia asaidiwe

Dunia imebadilika sana sikuhizi hakuna kazi za wanawake wala wanaume wala majukumu same way mnataka msaidiwe sijui kulipa school fees na kodi na mambo mengine na wewe inapendeza ukimsaidia mkeo ukikuta hajatandika tandika wewe mana hata wewe unalala hapo kama ukikuta hajapika pika wewe.. wanawake hawawezi kuzaa kwa uchungu at the same time wale kwa jasho, ila kama umeoa mwanamke anakutegemea kila kitu huyo hata ukimgeuza punda wako ni wewe na yeye makubaliano yenu tu
 
Hahah sio ajabu nawe utapata wanaokuunga mkono na hizi hoja zako!
soma vizuri mstari kwa mstari utetezi wa huyo mume wala hajazungumzia maswala ya kununua chupi hapo!
mbona tunawahi kupaniki??
hii inshu imewatokea wengi sana ni basi tu nyumba zina siri nyingi mno!

HUYO JAMAA HUO NI UAMUZI BORA NA HUO NDIYO UANAUME
Kama mahakama ambayo mwanamke anajua kuwa inatoa haki, busara zinapatikana hapo akaikimbilia nayo imemuona boya tu
sisi ni nani hata tujipendekeze kuwa Jamaa nae ana makosa???

Majukumu ya mke kazini??
SASA HIYO NDIYO SABABU???
usitekeleze wajibu wako ktk ndoa!!!!

Mbona Makamu wa Rais
hivi unaijua hii nafasi kweli???
Yule mama Samia alishawaambia kuwa pamoja na nafasi yake hiyo ya umakamu
ila MAJUKUMU YAKE KWa MUME WAKE na Familia
YAPO PALE PALE

jifunzeni na mnayo mengi sana ya kujifunza
mnatafuta justification sasa!!!
Kuchat
Kufuga kucha (kwanza mwanamke yeyote aliyefuga kucha mikono yote miwili NI MCHAFU HUYO BALAA)
hebu waza anavyojisafisha na hayo makucha kama shetani
mkono mmoja ni sawa ila yote miwili????
Hahah

Badilikeni Jamani tunawependa sana na tunapenda ndoa zetu pia!

Na wanawake wasipendeze? Akitaka kuweka kucha napo inawakera halafu mahawara zenu wote huko nje wanaweka makope wanafuga makucha. Kisa umemuoa ndio umfanye kama ajuza for what? Yaani nyie wote mliopanik Mungu amewapa wake wa kuendana na nyie hao wanawake muwashike sana sana siku akikuponyoka ulie na usage meno, makamu wa rais anatimiza wajibu wake kwakuwa labda na mumewe anatimiza ya kwake. Nilichokuwa nakitolea mfano ni nyie wanaume wa kulia lia kusaidiana majukumu na wake zenu habari za hela zikija ndo unajifanya kama wewe kuwa responsible huwezi, ndio mana nikauliza hapo juu huyo mwanaume anaemuacha mkewe kisa hafui yeye alikua amekamilika kwa lipi? Majukumu yake yote anafanya? Nikaenda mbali zaidi kuuliza kama hata huwa anakumbuka kumnunulia mkewe nguo za ndani au anadhani ni wajibu wa nani??
 
Kuna ME humu naye alifikiria kuacha MKE ili aoe beki tatu wake. Kisa beki tatu ndiye anamshughulikia zaidi tangu anapoamka asubuhi kujiandaa kwenda kazini mpaka anaporudi kutoka kazini.
Pia beki tatu alikuwa anawajali sana watoto wake na kuonyesha upendo wa hali ya juu kuliko nama yao saa zote yuko kwenye simu yake, TV au kujiremba.

Beki tatu pia alikuwa ni mtamu mno kuliko mke na mautundu kede kede na jamaa hakuwahi kunyimwa UCHI kila alipotaka ukilinganisha na mke na visingizio vyake vya kila mara vya kuchoka.

Beki tatu baada ya kupata chakula cha uhakika na kimono kila siku kulala pazuri na kujipiga soap soap na kujisiliba mafuta na nazi kuanzia kwenye Nywele hadi unyayoni 😜😜😜akawa MLIMBWENDE kuliko mama mwenye nyumba.

View attachment 1713163
View attachment 1713185
Mwanaume huyu toka jamii kutoka Ndola aliamua kumuacha mke wake waliyeoana miaka saba iliyopita na kufanikiwa kupata watoto wawili. Mwanamke huyu alienda mahakamani ilikutafuta suluhu ya ndoa yake na maridhiano na mume wake, akiomba mahakama imsaidie kunusuru ndoa yake na kuongeza kuwa hajui kwanini mume wake aliamua kuchukua uamzi wa kumuacha na kuoa mfanya kazi wao wa ndani.

- Mwanamke huyu aliiambia mahakama kuwa anampenda mume wake na haamini kama kweli ameamua kufanya kitu kama kile na kutaka kujua sababu zilizopelekea mume wake afanye hivyo.

- Mahakama ilipomuuliza mwanaume juu ya suala hilo alisema hawezi kubadili msimamo wake na hawezi kumuacha mke wake mpya wala hawezi kumrudia mke wake wa zamani maana maamzi yake ndio yalikuwa yameshafika mwisho na kushukuru kumpata mtu sahihi kwake na kusema mwanzo alifanya makosa kwenye kuchgua mke bila yeye kumjua mwanamke huyo vizuri.
Akaendelea kuaiambia mahakama kuwa mke wake huyo wa zamani alikuwa mzembe kupita kiasi, hakuweza hata kufanya kazi za ndani zinazomhusu kama mama wa familia na badala yake hata yale majukumu yake kwa mumewe aliyaacha mikononi mwa mfanyakazi wao wa ndani ambaye alijikuta kuwa ndio msaada mkubwa kwa mwanaume huyu , mfanyakazi wao wa ndani ndio aliyefua nguo zote za mwanaume huyo huku mke wake akiwa hana habari nae, hakutaka hata kukaa na kuongea na mume wake isipokuwa mfanyakazi wa ndani alikuwa akimuona amerudi toka kazini anampokea na kumuandalia maji ya kuoga, kisha anampa chakula na kukaa na kuongea nae sebuleni huku akimpa pole kwa uchovu na kumtia nguvu pindi anapoonekana kuchoka sana au kuwa na mawazo.

-Kuhusiana na suala hilo wazee walishawakalisha chini na ili kuwapatanisha bila mafanikio yeyote kwa wanandoa hao.

Alichokuwa akikifanya mwanamke huyu nyumbani ni kuwa bize kutoa maelekezo kwa mfanyakazi huyo wa ndani na kumfokea muda wote na kuwa bize na simu huku mfanya kazi wa ndani akiwa bize na mwanaume baba wa familia, hivyo niliona kila mtu abaki na kitu anachopenda kuwa bize nacho muda wote, mfanyakazi wa ndani anapenda kuwa bize na baba wa familia basi ni vyema awe nae aliatimize majukumu yake kwa baba wa familia vizuri, na mke wake kwa sababu yuko bize na simu basi nimuachie nafasi akae na kuchati kwa uhuru ili kila jambo liende sawa pia kwa upande wake.
Mume aliendelea kusema hata siku za mwisho wa juma (weekends) akiwa hayuko kazini mwanamke hakuona umuhimu wa kupika chakula kwa ajili ya mume wake kama alivyokuwa akifanya siku za mwanzo wa ndoa yao,badala yake alikuwa akifanya maandalizi ya kwenda kwenye sherehe za harusi na kamati za Kitchen Party, anarudi amelewa kitu ambacho mwanzo alikuwa hafanyi, na kama angekuwa anafanya nisingemuoa kabisa.

-Mume akaenda mbele zaidi na kuiomba mahakama iangalie kwa makini kucha ndefu za mwanamke huyo kama kweli zinaonesha mwanamke anayeweza kujishughulisha na shughuli za nyumbani kama mke wa mtu, muulizeni ana miaka mingapi hajawahi kupika chakula, kufanya kazi za nyumbani zaidi ya kuagiza, nani amekuwa akitandika kitanda changu kwa muda wa miezi nane sasa ?, Ni lini amejishughulisha hata kutunza na kuangalia watoto kama kweli ni mwanamke anayefaa kuwa mke, hayo yote mfanyakazi wa ndani ambaye ni mke wangu sasa ndio amekuwa akiyafanya siku zote.

Baada ya mahakama kujiridhisha na maneno ya mume ikatengua ndoa hiyo ili sasa mwanamke aendelee kuchat bila kikomo, ahudhurie sherehe za fungate, harusi na kufuga kucha huku mfanyakazi wa ndani akiwa boss ndani ya nyumba mwenye kujua na kujali majukumu yake kwa undani.

Wanaweke wengi huyajua makosa yao na ukimya wa mwanaume humfanya ayaendeleze bila kujua mwanaume muda mwingine yuko kimya akiwaza hatima ya jambo hilo na mwisho anaweza kuja na uamzi mwingine

Kuna la kujifunza.
 
Kuna ME humu naye alifikiria kuacha MKE ili ape beki tatu wake. Kisa beki tatu ndiye anamshughulikia zaidi tangu anapoamka asubuhi kujiandaa kwenda kazini mpaka anaporudi kutoka kazini.
Pia beki tatu alikuwa anawajali sana watoto wake na kuonyesha upendo wa hali ya juu kuliko nama yao saa zote yuko kwenye simu yake, TV au kujiremba.

Beki tatu pia alikuwa ni mtamu mno kuliko mke na mautundu kede kede na jamaa hakuwahi kunyimwa UCHI kila alipotaka ukilinganisha na mke na visingizio vyake vya kila mara vya kuchoka.

Beki tatu baada ya kupata chakula cha uhakika na kimono kila siku kulala pazuri na kujipiga soap soap na kujisiliba mafuta na nazi kuanzia kwenye Nywele hadi unyayoni 😜😜😜akawa MLIMBWENDE kuliko mama mwenye nyumba.
Poleni sana
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom